Tatizo la makelele kwenye nyumba za ibada

Mti wa Chuma

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
331
99
Habari wanajukwaa. Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa nimerejea jukwaani.
Twende kwenye mada.

Kuna tatizo moja kubwa sana kwa baadhi ya nyumba za ibada kupiga miziki kwa sauti ya juu huku wakiwa wameweka maspika makubwa.

Tabia hiyo huleta usumbufu na kero kwa wanaokaa eneo lililo karibu na nyumba hizo za ibada.

Hii hali inatakiwa ibadilike, ninavyojua mahali pa faragha na Mwenyezi Mungu si vyema kuwepo na makelele za miziki isiyo na maana, kama ni kusifu basi sauti za maspika ziwe chini.

Dhumuni langu kuandika uzi huu ni kero ambazo hutokea kwenye nyumba za ibada (makanisa) kupiga miziki.
 
Sio muziki tu..Hata mapastor nao wakati wa kutoa mahubiri uwa wanashout sana..Hivi hawawezi kuongea taratibu??...Huu utaratibu wa kupiga kelele wameutoa wapi sijui
 
na bado,mapando yote asiyoyapanda baba ndo muda wa kung'olewa hata kwa nguvu
 
swali ni moja tu....ni nyumba pekee za ibada zinapiga hizo kelele?..what about baa za uswazi,sherehe za mitaani.nk..au ni nyumba za ibada tu....maana kunya kanya kuku ....akinya bata eti kaharisha!
 
hii kwangu imekuwa sehemu ya ibada hususani SAA 11 alfajiri swalaa swalaa
sio siri jamaa wanna mawaidha mazuri sana wamekosa tenzi tu na mapambio
 
Habari wanajukwaa. Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa nimerejea jukwaani.
Twende kwenye mada,
Kuna tatizo moja kubwa sana kwa baadhi ya nyumba za ibada kupiga miziki kwa sauti ya juu huku wakiwa wameweka maspika makubwa. Tabia hiyo huleta usumbufu na kero kwa wanaokaa eneo lililo karibu na nyumba hizo za ibada.
Hii hali inatakiwa ibadilike, ninavyojua mahali pa faragha na Mwenyezi Mungu si vyema kuwepo na makelele za miziki isiyo na maana, kama ni kusifu basi sauti za maspika ziwe chini.
Dhumuni langu kuandika uzi huu ni kero ambazo hutokea kwenye nyumba za ibada (makanisa) kupiga miziki.
Wale ni wa utawala wa giza
 
ASANTENI WATANZANIA wenzangu sasa ni wasomaji wazuri wa biblia,...tunatambua kwamba mabaya ni yepi...inapigwa midundo mpaka mtu anapandwa na midadi ya disco na kusahau neno la msingi...na hata wachungaji wanakuwa hawana mtiririko wa mahubiri, ataanza na watoto kuheshmu wazaz,mara utajili,mara mapenz na ndoa, mara sadaka, mara kufunguliwa kwa tasa...hayo yote ndan ya masaa2 ya ibada
 
ASANTENI WATANZANIA wenzangu sasa ni wasomaji wazuri wa biblia,...tunatambua kwamba mabaya ni yepi...inapigwa midundo mpaka mtu anapandwa na midadi ya disco na kusahau neno la msingi...na hata wachungaji wanakuwa hawana mtiririko wa mahubiri, ataanza na watoto kuheshmu wazaz,mara utajili,mara mapenz na ndoa, mara sadaka, mara kufunguliwa kwa tasa...hayo yote ndan ya masaa2 ya ibada
Umenena sahihi mkuu
 
PIA TUFIKIRI SANA KUHUSU KUNENA KWA LUGHA...(hapa akili yatakiwa) HEBU ONA!
1.walokole(TAG,EAGT, SILOAM,.... nk) wananena
2.wasabato wananena
3.RC kuna kundi linanena(wanaitwa classmatic kama cjakosea, naomba kusahihishwa hapa)
kwa hao wachache wote wanadai wameshukiwa na ROHO TAKATIFU...HEBU JIULIZE
1.Hayo makanisa yanapatana? yanapendana?
2.roho takatfu moja inashuka toka kwa MUNGU mmoja kwenda kwa watu wasio na umoja?
3.je,yeye anenaye kwa lugha anajua akiombacho? au ahubiricho-!!
4.roho takatifu yule anayewashukia wasabato, ndo yule awashukiao wa TAG, EAGT, siloam, KKKT n.k...full gospel,.wa upako, na bado roho moja toka kwa MUNGU mmoja inazdi kuwatenganisha!?
 
Pole Mti wa Chuma, mwenzako nimeshakuwa sugu hivi sasa! Hapa nilipo nimeishi kwa miaka 6.5 sasa! Description ya mazingira ni hii hapa:
  • Dirisha langu la chumbani na sebuleni yapo takribani meta 20 toka kanisa la Walokole! Hawa jamaa kila wiki wanakesha kwa siku 3! Spika na vinanda vyao ni exceptional-- usipime!
  • Nipo kiasi cha meta chache toka kwenye ukuta wa kambi moja ya jeshi! Siku hizi wameanzisha mtindo-- tizi sharti kwa bongo flavor kwahiyo ikifika saa 11:15 alfajiri, kama masikio yako hayajaota sugu, wallah lazima uamke hata kama hutaki kutokana na pini zinazoporomoshwa!
  • Kiasi cha meta 20 kuna msikiti-- lakini afadhali hawa manake adhana yao haidumu hata dakika moja tena, ama spika yao haina nguvu au wanaamua kupiga adhana kwa sauti ya chini manake labda uwe macho ndo unaweza kuisikia.
  • Kiasi cha meta 50 toka ninapoishi kuna ukumbi mkuuuuubwa wa muziki! Lakini umaarufu wa ukumbi huu unatokana na kutumiwa kwa ajili ya harusi na kila wiki, at least sherehe 2 za harusi hufanyika kwenye huu ukumbi na muziki wa juu kama kawa!
  • Meta chache sana kutoka hapo kuna sehemu watu wanalaza daladala! Ikiwa hujajenga sugu masikioni, wana wanapokuja kuamsha daladala zao (usually saa 10 alfajiri) lazima na wewe uamke!
  • xxxxx Hii sitaisema! Lakini hili nalo ni jipu lingine ambalo miaka ya awali limenitesa sana! Jipu hili ndo limenikalia vibaya kweli kweli manake lipo chini ya 10 toka ninapoishi! Silitaji jipu hili kwa sababu maalumu!!
Narudia, pole sana manake nafahamu mtihani ulionao. Ikiwa siku hizi naweza kulala hata jamaa wafungulie maspika hadi mwisho basi lazima masikio yangu yatakuwa yameshatengeneza antigen! Trust me, vurumisheni maspika yenu mtakavyo mkidani mtanikomoa, lakini mbonji pale pale!! Ajabu ni kwamba mtu akikohoa tu anaweza kuniamsha kuliko akifurumisha muziki kwenye maspika!!!

Nahitaji medical check up manake hii si kawaida!
 
Back
Top Bottom