Tatizo la maji Mbezi mtaa wa Muhimbili, Dawasa mko wapi?

biznes_dealz

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
346
124
Wakuu poleni kwa majukumu. Mimi ni mmoja wa wananchi ninayepata adha hii kubwa, najua wahusika wapo humu ndani, natumai nitapata majibu ya kueleweka kujua nini kinaendelea Mbezi Luis, mtaa wa Muhimbili.

Kumefungwa mabomba yapata mwaka sasa, bili zimekuwa zikija kila mwezi kutaka wananchi walipie maji, kipindi chote hicho maji hayajawahi kutoka, je ina maana wahusika hawajui kuwa maji hayajawahi kutoka? Bili zinazotoka ni za kulipia kitu gani?

Na yale mabomba yamekaa kama urembo, nahitaji ufafanuzi na ufumbuzi wa kina MBEZI LUIS, MTAA WA MUHIMBILI.
 
yaan mnalipa bill wakat mwaji hyatoki so hyo bill unalipaga tsh ngap wakat unit ni 0 kwny mita
 
Nadhani mbezi yote, malalamiko ni hayo hata mitaa ya msakuzi, kama ni Kura tumesha ipa chama chetu waheshimiwa tupate ma water basi!
 
Nadhani mbezi yote, malalamiko ni hayo hata mitaa ya msakuzi, kama ni Kura tumesha ipa chama chetu waheshimiwa tupate ma water basi!

Huu ni mtihani kwa kweli, kero imekuwa kubwa sana, bili inatumwa kila mwezi na wakati maji hayatoki.
 
yaan mnalipa bill wakat mwaji hyatoki so hyo bill unalipaga tsh ngap wakat unit ni 0 kwny mita

Wanatuma kila mwezi bili na wakati maji hayatoki, ushahidi upo kwa wakazi wa Mbezi Luis, mitaa ya Uzunguni, Muhimbili pamoja na Tanzanite.
 
Back
Top Bottom