Tatizo la kuzimia,kutapika na kuweweseka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kuzimia,kutapika na kuweweseka

Discussion in 'JF Doctor' started by Aluta, Dec 29, 2008.

 1. A

  Aluta Member

  #1
  Dec 29, 2008
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nina mtoto wa uncle wangu mwenye umri wa miaka takribani 18. Alikuwa na afya njema kabisa na alikuwa anafanya vyema kwenye masomo, yupo form three. Lakini sasa hali yake si shwari kabisa kwani kapatwa na ugonjwa wa kuzimia kwa ghafla muda wa miezi miwili, tatu sasa, hasa mida kuanzia saa sita usiku akiwa kalala, na huwa inatokea kwa nguvu hasa.Kisha anatapika; na mara chache amekuwa anaweweseka na kupiga makelele usiku kiasi cha hata kuamsha majirani. Sasa wakuu kwa info nilizonazo, walimpleleka hospitali kwa doctor wa Moyo, akafanyiwa x-ray wakamwambia hawaoni tatizo lolote. Wakahangaika kwa tiba za jadi, waganga bado tatizo likawa palepale. Kinachohuzunisha ni kuwa huyu kijana amekata tamaa mpaka akafikia hatua ya kutaka kujiua na kusema kuwa anapoteza hela za wazazi tu, bora afe kama haponi. Watu wamejaribu kumsihi na kumshauri na yeye mwenyewe akaamua kumpokea Yesu, kwani ndio anaona suluhisho la mwisho. Lakini jana hali ile ya kuzimia imetokea tena baada ya kutulia siku chache baada ya kumpokea Yesu. Sasa ninachouliza, Je kuna mtu mwenye idea haya ni majonjwa ya aina gani kama ni ya kibinadamu? au ndio mambo ya kiswahili? Na kama kuna mtu anayefahamu Mchungaji anayeweza kumuombea kijana wetu aweze kufurahia maisha kama watu wengine tunaomba ushauri. Inauma kuona kijana mtiifu, hard working, maisha yake yanakwenda mrama namna hii. Asanteni kwa michango yenu.
   
 2. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2008
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu, nimejaribu kuilinganisha na ishu yangu iliyonipata mwaka (2007) mwanzoni ilinichukua kama two months kupata nafuu. Kwa kweli yangu haikufikia kuzimia ila nikutapika, kutojielewa, kuishiwa nguvu mpaka kufikia kutaka kujiua. Kwa kweli naamini YESU kristo ndo aliyeniponya. Mimi nilipelekwa Mikocheni B kwa Mch. Lwakatare. Itategemea ni wapi wewe unapendelea kwenda ila ni Yesu tuu ndo mponyaji wangu. Nakutakia kila la heri na pole sana kwa matatizo.
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aonane na daktari wa mifumo ya fahamu, sio daktari wa moyo. Chaweza kuwa kifafa...
   
 4. A

  Aluta Member

  #4
  Dec 30, 2008
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante sana, tutafuatilia maana hata familia yenyewe sasa imeamua kuegemea kwenye imani zaidi.
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa mwaka huu alikumbwa sana na tatizo kama hilo la kupoteza fahamu, kwanza huanza kujisikia kama viungo vinakakamaa, baada ya kukakamaa viungo hupiga kelele sana za kuomba msaada, na baadae kuishiwa nguvu. Katika matibabu, wakaangalia kila kitu, wakakuta hana ugonjwa wowote. Baadae wakagundua ana "stress" na "depression" (Sonona), sasa akahitajika apumzike sana, kumbuka alikuwa ni mfanyakazi, na ofisi yao wanafanya kazi si mchezo. Baada ya kuwa anapata mapumziko, ikawa hiyo hali bado inamtokea, lakini si sana kama alipokuwa hana mapumziko marefu. Daktari aliyekuwa anamtibu akasema kuwa hiyo hali hutoka taratibu sana, na inachangiwa tena na wasiwasi alionao wa huenda atapona ama la, na vile vile wasiwasi wa kazi yake na mengineyo. Kaishi kwa mapumziko na ushauri nasaha kutoka kwa madaktari, kwa sasa kapona kabisa.

  Hivyo nakushauri mumpe moyo kuwa atapona, pia mumuondolee hofu na kwenda hospitali kuonana na wataalamu ambao watamsaidia. Huyo jamaa alikuwa natibiwa Agakhan hospitali
   
  Last edited: Jan 5, 2009
 6. A

  Aluta Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante Mfumwa, lakini huyu dogo tatizo ni kuwa hana kazi za aina yoyote zaidi ya shule na kujisomea, achilia mbali vikazi vidogo vidogo vya nyumbani ambavyo hatuwezi ku-count kama anaweza kuwa busy kiasi hicho. Alafu yeye huwa inatokea kwa nguvu, kiasi kwamba anaweza akadondoka kitandani;tutafuatilia huko Agha Khan kama twaweza pata msaada wowote.
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Aluta:

  Matatizo mengine yanatokana na chemical imbalance katika brain. Ni brain inayo-trigger viungo vya mwili. Shemeji zangu watatu wanayo inayoitwa brain seizures. Mmoja ambaye nafahamiana naye anatumia vidonge na vilevile kuna aina ya vyakula amekatazwa kula.

  Vilevile brain tumor nayo inaweza kusababisha hayo matatizo

  Hivyo ikiwezekana wamtembelee neurologists and ifanyike brain scan.

  Na vilevile wagonjwa wanakuwa kwenye depression. Hiyo ya kutaka kujiua ni sign ya depression.
   
Loading...