Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Wakuu, nina tatizo la mwili kuwasha baada ya kumaliza kuoga tu. Hili tatizo lilijitokeza kama miaka mitatu iliyopita likatoweka lenyewe, sasa naona limerudi tena.
  1. Je, nini chanzo cha hii hali, ni maji ninayoogea?
  2. Ni sabauni ninazo tumia? Sina sabuni specific
  3. Ni maradhi ya ndani ya mwili
  4. Nini tiba yake?
---
Habar ndugu zang. Ninaomba ushauri kwa wenye kujua suluhisho la kuwashwa mwili baada ya kuoga. Najarbu kutumia sabun za aina mbalimbal lakini tatzo bado liko vilevile.

Please wana JF naitaji msaada wenu kwa wenye kujua.
---
---
---
===
UFAFANUZI WA JUMLA JUU YA TATIZO HILI
“Wataalamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi ni mambo mengine yanayochangia kutokea kwa mzio pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi.

Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.”

Katika hali ya kawaida kitendo cha kuoga kinapaswa kuchukuliwa kama jambo la kufurahisha kutokana na ukweli kwamba huufanya mwili uburudike na kuwa safi. Lakini kwa baadhi ya watu mambo ni tofauti. Kuoga huwa sawa na karaha.

Moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanayosumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha mara baada ya kuoga. Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu.

Hali hii inaweza kuwa inajitokeza kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu, hili linaweza kuwa tatizo sugu. Ingawa tatizo hili la kiafya ni kama mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi, hulihusisha na imani potofu.

Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa kama vile kuhatarisha kwa maisha.

Pamoja na ukweli wa kisayansi kwamba asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji, kwa upande mwingine yanaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya hasa pale yanapokuwa na vitu vinavyosisimua mwili au kuchochea hali ya kutokea kwa mzio. Siyo jambo la kushangaza kuona kuwa maji ambayo ni safi na salama kwa kunywa yanaweza kuwa siyo salama kwa kuoga.

SABABU ZA MUWASHO MWILINI
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.

Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa ni dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezi shingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu nyingine ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu, vumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.

Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho pindi mwili unapopata msisimuko, hali ambayo hujulikana kama mzio.

Mzio huanza pale mfumo wa kingamwili unapobainisha kemikali hizi kama mvamizi wa mwili na kuamuru askari wake wajulikanao kama seli za T-lymphocites na B-lymphocytes kujibu mapigo ya wavamizi kwa kuzalisha kemikali maalumu zijulikanazo kama immunoglobulin E na prostaglandins ambazo husababisha kuzalishwa kwa kemikali nyingine kama vile histamine, tryptase na chymase, kwa lengo la kuvunja nguvu za kemikali vamizi.

NI KWA NAMNA GANI?
Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa kutokana na hitilafu za vinasaba vya kijenetiki kunakuwa na ongezeko la kemikali aina ya Cyclic Adenosine Monophosphate Phosphodiesterase ambayo inaharibu mfumo wa udhibiti wa seli za kinga mwili aina ya basophils na seli za mast na kusababisha zisisimuke kupita kiasi na kuzalisha histamine nyingi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa mzio.

Watu wengi wana mzio wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za tiba, kemikali zinazotumika kutengenezea sabuni, vipodozi, aina fulani za vyakula, kemikali kadhaa zinazotumika katika usindikaji wa vyakula, kemikali zinazowekwa katika maji kama vile chlorine (watergurd), maji ya kuoga yenye chumvi nyingi na kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa nguo, ikiwa ni pamoja na mataulo ya kuogea.

Mapambano kati ya kinga mwili na kile ambacho mwili hukibainisha kwa makosa kama wavamizi, yanaweza kusababisha magonjwa ya pumu, muwasho wa ngozi, muwasho wa macho, mafua ya mara kwa mara na maumivu ya tumbo.

SABABU NYINGINE
Mapambano haya pia yanaweza kusababisha hali ya mzio dhidi ya vyakula kama vile mayai, maziwa, samaki, nyama, karanga, vyakula vitokanavyo na unga wa ngano, kahawa, pombe na baadhi ya vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa au kusindikwa viwandani kwa kutumia kemikali. Hali hii pia inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vyenye mchanganyiko wa vikolezo kama pilau na viungo vingi.

Ulaji wa vyakula vyenye upungufu wa viinilishe nao unatajwa kuwa unachangia kutokea kwa tatizo la mwili kuwasha wakati wa kuoga.
Watu wengi hawatumii kiasi cha kutosha cha matunda, mboga na mafuta salama yanayotokana na mimea au samaki, jambo ambalo huathiri vibaya afya ya ngozi.

Tatizo jingine linalochangia mwili kuwasha wakati wa kuoga ni kutokutumia kiasi cha kutosha cha maji ya kunywa kila siku. Hali hiyo inafanya mwili kuwa na upungufu wa maji na kuathiri vibaya afya ya ngozi na uwezo wake wa kuondosha sumu mwilini.

Ngozi isiyokuwa na afya njema inashindwa kutunza kiasi cha kutosha cha unyevu na kusababisha ukavu. Ngozi inapokuwa kavu husisimka kupita kiasi wakati wa kuoga na kusababisha muwasho. Sababu ya mwili kuwasha baada ya kuoga ni kuishi katika hali ya msongo wa mawazo inayosababishwa na hofu, wasiwasi na sonona.

Tatizo jingine linalosisimua mwili na kusababisha muwasho wakati wa kuoga ni kujisugua kupita kiasi au kujisugua wakati wa kujifuta kwa taulo baada ya kuoga. Kwa kawaida seli za ngozi zilizokufa, jasho na vumbi ndivyo vinasababisha mwili kuchafuka.

Lakini uchafu huo huondoka mwilini tunapooga na nguvu nyingi hazihitajiki ili kuondosha uchafu na taka mwili juu ya ngozi. Matumizi ya nguvu nyingi na kusugua ngozi sana, husababisha madhara kwenye ngozi na kusababisha muwasho au ukavu wa ngozi kwa kuondosha mafuta yanayolinda usalama wa ngozi.

Watu wenye tatizo hili wanaweza kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuoga ili kupasha mwili joto au kupaka lotion ili kuifanya ngozi kuwa na unyevu na kupunguza hali ya ukavu wa ngozi

===
USHAURI NA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
---
---
---
---
---
---
---
---
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII
- Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara linasababishwa na nini? - JamiiForums
 
Siku mbili hizi nimefanya ka research kadogo kuhusu miwasho, nadhani hiyo yako inaweza kuwa inasababishwa na ngozi kuwa dry so ukitoka kuoga jipake mafuta fasta na pia ukijifuta na taulo usijisugue fanya kama una ji sponge kwa kugusia gusia kwenye mwili.
 
Bwana we hata mi hili tatizo ninalo na linanikera sana na linanitokea nikioga maji baridi yani nawashwa naskia kero vby sana, lakini nikikoga maji moto siwashwi, nilichoamua kufanya ni kuweka maji yangu detol ya maji na kuyaogea sasa tatizo limepungua.
 
Muwasho baada ya kuoga yaweza kuwa ina sababishwa na maji unayotumia kuogea yana aina ya chumvi chumvi ambayo haipatani na ngozi yako. Hii ni kama unaogea maji ya kisima. Au inasababishwa na aina ya sabuni unayo ogea.

Ngozi yako iko sensitive kwa hiyo ina react na ngozi yako na baada ya muda inpozwa na mafuta ya mwili. Pia inweza kuwa unatumia taulo damp ambayo haikauki vizuri toka uitumie mara ya mwisho.

Vyote hivi vinahitaji uchunguze mwenyewe na take actions acordingly.
 
Hebu fuatilia ushauri wa Doctorz natumaini utakusaidia.lakin pia kunawatu wanatumia vitu vigumu kujisugua mwilini kama unafanya hivyo hebu acha na tumia kitambaa/taulo ndogo laini
 
Mimi nikioga na maji moto nawashwa kwa dk kama 15 alafu inaacha . Sijui hata nini ?
 
Ahsanteni wakuu, nitajaribu ushauri wenu
 
Doctorz, umesema vema sana, binafsi huwa nina tatizo hili na nitafuatilia ushauri wako
 

Maji hayo unayoyaoga yawezekana kabisa yakawa si masafi na kusababisha ngozi yako kureact.na maji yetu tuogayo si masafi kwa sababu water system zetu ni za zamani sana na kusababisha maji kuchafuka kabla ya kuwafikia watumiaji.
 
doctorz,
Doctorz umesema kweli, hiyo kuwashwa ni reaction ya mwili kwa alergy; yaani kunakuwa na aina ya chumvi kwenye maji ambazo mwili wako haukuzoea. Hivyo kuwasha, hakuna dawa ila jaribu kuchemsha maji ya kuoga kila inapowezekana vinginevyo ya baridi yatakuwasha lakini ukiyatumia muda mrefu taratibu mwili unazoea na hali hiyo inaisha.
 
Kumbe siko peke yangu? Mie nawashwa baada ya kuoga haswa mikono na miguu!!
 
Sometimes pia ngozi ikipata rapid temperature change huwasha, mfano ulikua kwenye sehemu yenye AC na ghafla ukatoka nje kwenye jua kali ngozi huwasha sana, au ukitoka kwenye joto kali sana na ukaenda kuoga na maji baridi pia ngozi huwasha.

Despite tatizo la allergies pia hii nayo ni sababu, ngozi kuwa exposed to rapid temperature changes zile pores zinazohusika na kupitisha hewa zina 'shrink' kwa haraka na kusababisha hali ya muwasho wa ghafla.
 

Pia jaribu kutumia sabuni 'gentle' na zenye mafuta .... kama DOVE (huu ni mfano tu bila shaka kuna aina nyingine. Check with your pharmacist)
 
Tatizo kama hili ninalo kaka yani wakati mwingine huwa nawashwa mpaka najikuna na kisoda ila nikijipaka mafuta vaselin inakwisha
 
Nadhani ni sabuni, hasa hivi za manukato. Mimi baada ya kuanza kutumia sabuni jamaa hakuna tena.
 
Mimi pia nina hili tatizo na limekuwa ni tatizo la muda mrefu sana, na hasa nikioga maji ya baridi nimeenda hospital tofauti tofauti lakini tatizo liko pale jibu nililopata kwa hospital ni allergy. Kuhusu maji sijui kama ni kweli kwa sababu mimi naishi kanda ya ziwa so naoga maji ya ziwa hayana chumvi, kwenye maeneo ya maji chumvi nimefika lakini ni yale yale tu.

Mimi ninachofanya na kidogo tatizo limepungua kwa sehemu ni kwamba naoga maji ya moto, sijifutii taulo natumia khanga kujikausha na nikimaliza kuoga najikausha fasta, sikai na maji zaidi hata ya dk moja na kujikausha kwenyewe ni kama unajisponji sio kujifuta, nikishajikausha napaka mafuta kidogo sehemu ninazaowashwa, so inanisaidia kidogo angalau muwasho unakuwa si mkali sana, halafu mimi siwashwi mwili mzima nawashwa kwenye mikono na kwenye mapaja basi.

 
Hata sabuni sidhani kama ni sababu, mimi nina hili tatizo zaidi ya miaka 10. Hospital nilishauriwa kuacha kitu kimoja baadya ya kingine matokeo yake yalikuwa ziro, ilifikia hatua nachemsha maji ya kuoga yanachemka kama ya ugali then unaacha yanapoa unaenda kuoga lakini wapi.

Sabuni ndo usiseme nilianza na gwanji, ilula, kwanga hadi sabuni ya mbuni inayosemekana haina kemikali ilikuwa ni kazi bure, nowdays naogea sabuni ya dettol na ninafanya kama nilivyosema kwenye post yangu ya mwanzo ndo angalau tatizo limepungua, nawashwa lakini si sana. Mimi hata kama kuna baridi kama mikono iko wazi chamoto nitakiona, nitajikuna balaa


Nadhani ni sabuni, hasa hivi za manukato
Mm baada ya kuanza kutumia sabuni jamaa hakuna tena.
 
Pole sana ni tatizolinalosababishwa na mambo mengi ambalo jibu la jumla ni tabia ya mwili mimi pia nlikua na tatizo hilo nkatumia sabuni fulani ya kichina kutoka kampuni inaitwa TIENS sabuni yenyewe inaitwa Spirulina body wash ilinisaidia sana pia nlikua natumia majani ya chai yao kiukweli imeniondolea tatizo hilo na mengine sasa najsikia fresh itumie na wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…