Tatizo la kuuma kwa moyo

Oct 21, 2020
19
4
Wanajamii hivi tatizo la kuuma kwa moyo na kwenda mbio huwa lina sababishwa na nini na dawa yake nini?

Maana huwa linanijia kwa mda na hupotea yani moyo unakwenda mbio mpaka naisi kama nakufa

Nikila vidonge vya presha tatizo ndo linazidi na dawa za hospital nikila ndo linazidi

Anaejua kitu kuhusu hili tatizo tuambizane jamani
 
Ulipewa Dawa ganiii??? Inawezekana hukupewa COMBINATION sahihi ya dawaa na dose so moyoo lazima uendee mbioo sababu ya Effect ya hiyo dawaa ulizokunywaaa.
 
Mim nilikuwa na tatizo kama hilo, lilinitesa kwa Miaka mingi, Hivi sasa nimepona. Usitumie dawa za Presha, zinafanya tatizo kuwa kubwa zaidi.

1. Zingatia aina fulani ya chakula, punguza kula vyakula vya Mafuta sana kama Chipsi
2. Kunywa sana Maji
3. Tumia sana Vitunguu Swaumu
4. Tengeneza Juice ya Limao, kunywa Mara kwa Mara. Ila usizidishe.
5. Acha kutumia Soda
6. Pendelea sana kula Almonds, Walnuts na Pecans. Zinapatikana Kariakoo au kwenye Supermarket kubwa kubwa.
7. Pendelea kufanya mazoezi ya Kukimbia na Pushups walau 50 kwa siku.

Ukipata muda ingia YouTube, Andika Health Benefits of Almonds au Walnuts au Pecans utaweza kuelewa zaidi ni vitu gani na vina kazi gani mwilini.
 
Mim nilikuwa na tatizo kama hilo, lilinitesa kwa Miaka mingi, Hivi sasa nimepona. Usitumie dawa za Presha, zinafanya tatizo kuwa kubwa zaidi.

1. Zingatia aina fulani ya chakula, punguza kula vyakula vya Mafuta sana kama Chipsi...
Tatizo litakua apo kweny vyakula nais kuna. Chakula kinanifanya niwe ivi ila ndo sijakijua
 
Kwanza anza kwenda hospitali ukachunguzwe mkuu,nilikuwa na tatizo kama la kwako ,nilienda mhumbili,pia nilifika kitengo cha magonjwa ya moyo cha jk hapo muhimbili lakini hawakuona tatizo,hapo muhimbili nilifika Mara mbili,baadae nikaja Bugando kama Mara nne nikafanyiwa vipimo vya kila namna lakini wapi.

Mwisho wa siku nikaona nionanae na daktari wa mfumo wa chakula ,hapo hapo Bugando anaitwa Dr majinge ,nishukuru mungu hapo ndo ulikuwa mwisho wangu wa kwenda hospitali, hadi sasa Nina miaka miwili bila kwenda tena hospital, maana ilionekana Nina madonda ya tumbo hivyo nilipewa masharti ya namna ya kuishi na madonda ya tumbo na vyakula amabavyo sipaswi kutumia.

Nishukuru mungu kwa sasa hata madonda ya tumbo sioni tena dalili,lakini pia nikili kuwa watu wengi hufa kwa kukosa matibabu na huduma mzuri za afya kwanini kwa namna hali yangu ilivyokuwa imefikia nilikuwa nimekata tamaa sana lakini kwa sasa Niko buheri wa afya.

Ushauri wangu ni kuwa hebu nenda hospitali ukafanyiwe vipimo vyote vya moyo ili kubaini tatizo baada ya hapo Pima vipimo vya mfumo wako wa chakula.

Mwisho nakupa pole sana,lakini pia kama huna bima ya afya na kiuchumi hauko vizuri naongeza kukupa pole.
 
Kwanza anza kwenda hospitali ukachunguzwe mkuu,nilikuwa na tatizo kama la kwako ,nilienda mhumbili,pia nilifika kitengo cha magonjwa ya moyo cha jk hapo muhimbili lakini hawakuona tatizo,hapo muhimbili nilifika Mara mbili,baadae nikaja Bugando kama Mara nne nikafanyiwa vipimo vya kila namna lakini wapi...
Asante ila bima ndo mtiani na uchumi mdogo kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom