Tatizo la Kutokulala kwa watoto wachanga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Watoto wengi wadogo huwa wanapata shida sana kutulia na kulala wakati wa usiku. Kwa watu wengine hili sio tatizo kwao na kama haikusumbui mtoto wako kwenda kulala muda ambao wewe unaenda kulala, basi sio shida. Lakini, kama wewe, ama mtoto wako anasumbuka na tatizo la kushindwa kulala usiku unaweza kujaribu kufanya yafuatayo:

Kila mtoto ni tofauti na fanya tuu kile unachoona kinafaa kwa mwanao.

Kama Mtoto wako hataki kwenda kitandani:

  • Amua saa ngapi ama mda gani unataka mtoto awe anaenda kitandani.
  • Kwa kuanza, mda wa mtoto kwenda kulala ukikaribia (ule mda anaolalaga kila siku) anza kumpeleka kulala dakika 20 kabla kwa siku ya kwanza, alafu siku ya pili mpeleke dakika 30 kabla, ya tatu iwe dakika 40 kabla na kuendelea kuongeza dakika 10 kila siku mpaka ifikie mda ule unaotaka wewe.
  • Jipangie kikomo cha kukaaa na mwanao kitandani wakati wa kulala, mfano msomee hadithi moja tuu, alafu sema usiku mwema, muage na kumwacha alale.
  • Mpatie mtoto wako toy yake anayoipenda alale nayo, mfano kama huwa anatumia dummy ya mdomoni, ama kitaulo (kuna watoto hunyonya kitaulo) ama chochote kitakachombembeleza kulala.
  • Kama mtoto wako analia, umwache kitandani na uondoke chumbani na mpatie dakika 5 mpaka 10 ya kujituliza mwenyewe kabla ya kumyamazisha tena.
  • Usimnyanyue ama kumbeba mtoto, ama kumtoa kitandani na kama mtoto atainuka na kutoka kitandani basi mchukue na kumrudisha kitandani tena.
  • Washa taa yenye mwanga mdogo (kama unayo) ama acha mwanga wa mbalamwezi uingie kama kutakuwa na ulazima huo.
  • Hakikisha amelala kabla ya kwenda kumwangalia mtoto ili usimwamshe tena.
  • Fanya hivi kila siku na usikate tamaa baada ya siku moja tuu, jipatie siku 5 ili mtoto awe na mazoea.
Kama mtoto anaamka mara kwa mara usiku.
Ni kawaida kwa watoto wa zaidi ya miezi 6 kulala usiku mzima bila kuamka, Hata hivy, kuna watoto wengi chini ya miaka mitano huwa hawalali usiku mzima bila kuamka. Kuna ambao watarudi kulala tena wao wenyewe na wengine ambao watalia kwa kutaka uwepo wa mtu.

Kama hii hali itatokea, jaribu kutatua tatizo linalimfanya mwanao aamke usiku.
Je ni njaa? kama mwanao ni mkubwa zaidi ya mwaka moja, maziwa na uji huwa yanaweza mfanya alale usiku mzima kama hivyo ndio alikunywa mda tuu kabla ya kulala.

Je ni uoga/hofu ya giza? unaweza kutumia taa za usiku ama unaweza acha taa ya corrido iwake usiku.

Je ni ndoto mbaya? kama ni hivyo jaribu kutafuta kama kuna kitu kinachowasumbua ambacho ndio husababisha kuota usiku.

Je ni joto/ baridi kali? kama ni hivyo punguza ama uongeze nguo za kujifunika ama punguza/ongeza joto ama baridi kwenye chumba kwa kufungua milango ama kupunguza AC.

Kama hakuna sababu maalumu inayomfanya mwanao aamke, alie ama kutaka ukae nae usiku basi jaribu yafuatayo:

  • Mda wa kuamka - kama mwanao huamka wakati huo huo kila usiku basi jaribu kumwamsha kati ya dakika 15 mpaka 60 kabla alafu mbembeleze tena kurudi kulala.
  • Mruhusu mtoto alale chumba kimoja na kaka yake ama dada yake kama tatizo ni kuogopa kuwa peke yake. Hii itawasaidia wote walale usiku mzima.
  • Mfundishe mwanao kujirudisha kulala yeye mwenyewe usiku, kwanza kama kila kitu kiko sawa, mmbembeleze mwanao kulala bila ya kuongea nae sana akiwa kitandani. Kama anataka kinywaji mpe maji ila angalisho usimpatie chakula wakati akiwa ameshtushwa na usingizi. Ili njia hii ifanye kazi ni lazima umwache mtoto kitandani na usimnyanyue na kwenda nae sebuleni, ama chumbani kwako. Mwache alie kwa kati ya dakika 5 hadi 10 ndipo ukamwangalie tena. Mwambie arudi kulala na mwakikishie kwamba hakuna kitu cha kuogopesha na usiongee nae kitu kingine, kama ni mtoto mchanga mbembeleze kwa kumpapasa mgongoni akiendelea kulia mbebe kwa dakika 2 tuu alafu mrudishe kitandani. mwache kama analia ikifika dakika 10 nenda tena, fanya kama hapo juu na umwache ena ajirudishe kulala. Endelea hivyo kwa siku kadhaa na mtoto atazoea na kuanza kusinzia mwenyewe ukimweka kitandani.
  • Msaidiane na mumeo, mnaweza mkafanya zamu ya kumwangalia mtoto anapolia, hii pia husaidi mtoto kuwajua na kuwazoea wazazi wote wawili, pia itamfanya mama asichoke sana.
Ndoto za kutisha

Ndoto za kutisha ni kawaida kabisa. Wao mara nyingi huanza kati ya umri wa miezi 18 na miaka mitatu. Ndoto hizi ni si kawaida ni ishara ya masumbuko ya hisia. Huwa inaweza kutokea kama mtoto wako ana wasiwasi juu ya kitu au amepata hofu na kipindi ama hadithi aliyoangalia kwenye luninga. Baada ya ndoto, mtoto wako atahitaji faraja na uhakika. Kama mtoto wako anaota ndoto hizi sana na hujui ni kwa nini basi ongea na daktari.

Kuweweseka usiku

Hutokea kabla ya umri wa mwaka moja ingawa pia ni kawaida zaidi kwa watoto kati ya umri wa miaka mitatu hadi nane. mara nyingi mtoto huweweseka na kupiga kelele ama kupigapiga mikono na miguu akiwa bado yupo usingizini. hutokea baada masaa machache ya kulala, wanaweza kukaa na kuongeaongea wakiwa usingizini na kuonekana wenye hofu wakiwa usingizini. Wala usiogope na mtoto wako itafika wakati itapita tuu.

Usimwamshe mwanao wakati akiweweseka ila kama hutokea mda huohuo kila usiku basi jaribu kumwamsha dakika 15 kabla ya muda ule anaoweweseka kila siku. abaki macho kwa dakika chache kabla ya kumrudisha kulala tena.

-MTOTO NA AFYA-
 
Kwa uzoefu watoto wengi husumbuliwa na ndoto mbaya usiku na ndoto hizi hutokana na mambo ya kiroho yanayoendelea wakati wa usiku. Mambo huwa mabaya zaidi kwa nyumba zisizokuwa vizuri kiroho; nyumba zisizosali, nyumba zenye ushirikina au zinazosumbuliwa na ushirikina.Watoto wanaweza kuteseka sana endapo wazazi hawana uelewa wa mambo ya kiroho; watafikiri ni kawaida tu. Unapaswa kumlinda mtoto wako kwa maombi na sala kila siku.

Wakati wa usiku ndipo wachawi wanafanya kazi zao na hupenda sana kucheza na watoto na kuwaibia nyota zao pia. Mtoto atalia sana kwani huwa watoto hawaoti ndoto mbaya tu bali huwaona wachawi live, hasa watoto kati ya mwaka 1 hadi 4.

Wanaowavalisha watoto hirizi ndio huwafanya watembelewe zaidi na wachawi na mapepo, kwani huwakabidhi watoto kwa ulimwengu wa giza bila kujua.
 
Hakuna lolote

Mtoto kutolala usiku sababu tatu kuu za msingi

1. Njaa .....mtoto usiku kama hashibi halali nivurugu tupu, maana mama analala hashughuliki Naye

2. Akiwa mgonjwa hususani tumbo kumuuma nk

3. Mazingira mabovu yaani sio comfortable....joto, kuwasha mwili, vumbi, harufu kali nk

Mtoto akiwa nimeshiba, haumwi na mazingira bora Kulala....hawezi Kulia kamwe

Thanks everyone.
 
Nasikia watoto huwaona wachawi
Ni kweli sababu roho zao zinakuwa Safi hazina dhambi hata moja wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuona uwezo Huo waweza endelea Hadi miaka sita kwa Watoto wa familia nzuri zisizo za walevi au watukanaji waishio mazingira mazuri yenye majirani wazuri
 
Mtoto anaezungumziwa hapa ni wa umri gani??
Kulingana na ulivyoelezea ni dhahiri unazungumzia watoto wakishua/malezi flani hivi wale wa kijijini interior mtoto anaenda lala kwakusindikizwa na bao moja analilia kitandani mpk usingizi umchukue

Cc Kingsmann
 
Ni kweli sababu roho zao zinakuwa Safi hazina dhambi hata moja wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuona uwezo Huo waweza endelea Hadi miaka sita kwa Watoto wa familia nzuri zisizo za walevi au watukanaji waishio mazingira mazuri yenye majirani wazuri
Haswa akitokea familia ya lumumba
 
Watu wazima tuna biological clock. Miili imjiwezesha kuwa usiku ni wakati w kulala. Mtoto mchanga bado mfumo wake bado haujatengeneza huu mfumo. Hivyo hana muda maalum wa kulala. Wewe usiku ukitaka lala mfumo wake bado haujozoea. Analala au halali.
 
Haswa akitokea familia ya lumumba
Hata ya chadema mfano ya familia ya Mbowe wanawe hajawahi washirikisha maandamamo yoyote wanaenda Watoto wengine wa wenye dhambi wa chadema.Ulishawahi ona mtoto wa Mbowe akiandamana?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom