Tatizo la kupata usingizi wa mang'amung'amu

Tatizo la kupata usingizi wa mang'amung'amu

emavalery

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
628
Reaction score
1,252
Hodi hodi huku ndani wakuu,

Nina msaada wa kiafya au wa saikolojia, ila natanaguliza shukrani kwa Muumba maana sio mgonjwa ila pia binadamu bila afyaa njema anakua na wakati mgumu sana, ningeshauri pia jukwaa la JF Doctor liwe pale juu kabisa ili kila mmoja aingie na kujua masuala na ushauri mbali mbali wa kiafya.

Nije kwenye mada, kiukweli imenichukua muda kujua hili tatizo la kukosa usingizi ifikapo muda wa kulala, nalala kwa bahati sana na asubuhi naamka bado na usingizi unaishia huko kwenye jua la Dar.

Ila kuna vitu nikifanya kabla ya kulala, nalala fresh tu, moja ni ikiwa nimepiga bia mbili mpaka nne, nalala safi kaabisa.
Na pili, au nifanye mapenzi hata kidg tu mwili unarelax na usingizi naupata bila tabu.

Swali au msaada?, Hii shida inaletwa na nini na njia zipi nitumie ili niweze pata usingizi katika hali zote??

Asanteni sana wakuu, najua ntapata msaada wa kutosha,
 
Solve ishu zako mzee, ziwe za mapenzi kazi biashara au ajira. Mimi huwa nachelewa kulala afu nawahi kuamka ila matatizo yangu nayafahamu nafikiria sana michongo yangu kiasi nakosa usingizi, mwisho wa siku ni utu uzima tu ain't a kid no more.
 
Solve ishu zako mzee, ziwe za mapenzi kazi biashara au ajira. Mimi huwa nachelewa kulala afu nawahi kuamka ila matatizo yangu nayafahamu nafikiria sana michongo yangu kiasi nakosa usingizi, mwisho wa siku ni utu uzima tu ain't a kid no more.
Asante mkuu,
 
Lipa madeni ya watu mzee😀😀😀😀
 
Ni tabia tu ambayo umeijenga kichwan mwako bila kitu Fran hupat usingiz hata hiyo tabia ninayo tuseme ni stress tu zinatutesa hata mm bila pombe Kali sijapata usingiz lakn nashukuru mwez wa Ramadhan huu Nina siku NNE sijatumia japo sifungi lakn nalala saa tisa usiku tena kwa kubahatisha lakn naamka Nina nguvu tena mapema tofauti na nikinywa
 
Back
Top Bottom