Tatizo la kupata AVN number

Ndosh

Member
Joined
Oct 14, 2020
Posts
31
Reaction score
13
Habari za leo wakuu, kuna shida moja katika upatikanaji wa AVN kwa wahitimu katika ngazi ya stashahada, hasa katika baadhi ya kozi zinazotolewa na baadhi ya taasisi za elimu.

Mimi ni mhitimu wa kozi ya UALIMU ELIMU YA UFUNDI SECONDARY ngazi ya stashahada, niliomba AVN nikapewa lakini kila nikiomba chuo naletewa details za matokeo yangu zinazoonesha GPA ya 0.0 tena nilipewa mara mbili lakini tatizo liko palapale, hili Ni tatizo kwa mamlaka husika.

Tafadhali kama kuna wahusika wa hiyo mamlaka WEKENI MFUMO WENU VIZURI. Kumbukeni kuwa muda wa kuomba vyuo umebaki kidogo sana.

Kwa ushauri wangu, bora huo mfumo utupiliwe mbali maana umetukera sana.

Ahsante.
 
NACTE na vyuo vyake bado wana kazi kubwa ya kufanya kuoanishaacademic cycle yao na admission cycle viende pamoja smoothly. Mwaka jana niliongea na kijana mmoja aliekuwa anamaliza diploma, cha kushangaza wakati yuko field dirisha la udahili TCU ndio lilikuwa linaelekea kufungwa. Hivyo hadi anapata matokeo yake yote TCU walikuwa wamemaliza kazi, na ilibidi asubiri mwaka mzima ili aweze kuomba udahili TCU.

Lingine ni la kupeleka matokeo NACTE kwa wakati kama alivyoleta mleta uzi, yakichelewa tu inakula kwa anaetaka kudahili chuo kikuu chini ya TCU.

Naamini tuna vichwa vyenye uwezo wa kutatua hili ama sivyo NACTE na TCU waunganishwe tuwe na mfumo mmoja.
 
Hakika ndugu, Lakini sijajua shida Ni Nini,, sababu nikiangalia kwenye mfumo wao (Student information verification) taarifa zangu ziko nacte.
 
Hakika ndugu, Lakini sijajua shida Ni Nini,, sababu nikiangalia kwenye mfumo wao (Student information verification) taarifa zangu ziko nacte.
Kama taarifa zako zote unaziona basi system yao itakuwa na bugs.Nafikiri kama unajua GPA inapigwaje au unajua GPA yako-omba halafu hayo mengine uyafuatilie (nenda NACTE au piga simu au peleka malalamishi kwa e-mail).
 
Reactions: p2k
Kama taarifa zako zote unaziona basi system yao itakuwa na bugs.Nafikiri kama unajua GPA inapigwaje au unajua GPA yako-omba halafu hayo mengine uyafuatilie (nenda NACTE au piga simu au peleka malalamishi kwa e-mail).
Nishapeleka hadi barua but wako kimya, hadi inafika mahali nalaumu walioweka huu mfumo unaokwamisha ndoto za vijana wengi,,, na wahusika nimeshaonana nao wanalinga utafikiri waliwekwa kurudisha maendeleo ya wanyonge nyuma!!😱😱😱, Serikali iangalie hili, Wanakera hadi nakata tamaa!!
 
Niwape pole. Mfumo huu ni wa kufumua kabisa kwani miaka nenda miaka rudi shida hii haishi.
 
Waliouanzisha hawana uataalam wowote,, Ni kuhangaisha masikini tu,, mtu unamwambia aende ofisi za nacte wakati aliko Ni mbali hawangalii hata hali za watu masikini 😱
 
Da ili tatzo n kubwa sio Poa na sijui wizara ya elimu inafanya kazi gani Ila usikate tamaa mm mwenyew niliangaika knoma japo nilifanikiwa kupata
 
Isitoshe nimegharamika hadi kuomba mkopo,, MFUMO WETU WA ELIMU NI wa kizezeta sana ,, tena wanazidi kunirusha, mara niende NECTA Dare es salaam,, gharama za nauli nazitoa wapi?????? Ujinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…