Tatizo la kufa ganzi mguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kufa ganzi mguu

Discussion in 'JF Doctor' started by Mshume Kiyate, Oct 20, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF.
  Mimi natatizo la kufa ganzi mguu wa kushoto nikikaa chini muda mrefu..

  Kama kuna mtu anajua ni nini kinachosabisha tatizo hilo au tiba yoyote naomba anijuze
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Maradhi ya Ganzi ni moja katika sababu zinazoweza kuhatarisha kiungo cha mwili ni mfumo wa kufanya ganzi katika kiungo kwa muda mrefu, ganzi hutokana na kuvilia au kusalilia damu katika sehemu moja kwa ufupi damu kutozunguka katika sehemu ile kwa muda mrefu. Kwa mfano ukikaa sana, au pia ukisamama sana na hii sio sababu ya kukaa na kusimama tu, mwili wa mwanaadamu haustahamili kitu kupita kiasi.

  Miili ya wanaadamu imeumbwa na kiasi kila kitu kwa kiasi, kula kunywa kulala n.k kwa hivyo, ikiwa utakaa au utalala kwa muda wa kupindukia bila harakati yoyote basi damu hushindwa kuzunguka katika mwili na hushindwa kupokea hewa safi na kutoa hewa chafu, ndipo mfumo wa GANZI hutokea na ukianza kufanya harakati tu basi ngazi wenyewe huondoka.

  nakushauri kwanza ukutane na Daktari haraka iwezekanavyo, na huku ukiendelea kutumia mafuta ya habati sauda (Nigella seed oil)kwa kujipaka kwenye sehemu inayo kufa ganzi.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,585
  Trophy Points: 280
  asante sana mkuu kwa ushauri.
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nashukuru mkuu MziziMkavu Mungu hakuzidishie
   
Loading...