Hauwezi kutabiriwa soda kiasi gani kwa wiki inaweza kusababisha sukari...Soda/Sukari nyingi sio nzuri kwa afya yako kwa ujumla kwahio ni vizuri ukiiepuka kutumia ...Ninachoweza kukushauri ni kula vyakula healthy na natural sio artifical readymade foods/junk foods!
Insulin ni homoni inayozalishwa kwenye pancreas.Kwa muonekano unaweza kutazama picha chini hapo
Kwa lugha rahisi insulin ni UFUNGUO ambao unachukua sukari kutoka kwenye DAMU kupeleka kwenye Body CELLS.Body CELLS zinahitaji glucose au sukari ili kutengeneza energy.Kama umesomea baiolojia utajua Body cells ni nini,mwili wa mwanaadamu umejengwa na thousands of body cells which are also called animal cells.
Mfano kama mtu ana ugonjwa wa kisukari na hatibiwi inamaana kutakuwa na muongezeko wa sukari kwenye damu na hali hio itasababisha UBONGO kukosa glucose(energy) hatimae kupelekea kifo.
Ugonjwa wa kisukari unampata mtu anapokuwa na mapungufu ya homoni ya insulin au kutozalishwa kabisa na homoni ya insulin.
Ugonjwa wa kisukari umegawanyika katika makundi matatu:
Watu wanaopatwa na Diabetes type I wanakuwa hawana uwezo wa kuzalishwa kwa homoni ya insulin kabisa mwilini,ni lazima wachome sindano za homoni ya insulin.Hali hii inasababishwa na kurithi na mtu anazaliwa na ugonjwa huu.Waathirika wa ugonjwa huu hawawezi kupona.
Hali hii huwapata haswa watu walokula chumvi kuanzia 40+ na inatokana na kutokujali afya kwa kupenda kula vyakula ambavyo si vizuri kiafya fatty foods,vyenye sukari nyingi ambayo hupelekea Pancreas kuwajibika (overproduce) insulin kwa wingi kuliko ipasavyo hatimae kudhoofika kabla ya wakati wake au kupungua kwa uwezo wake wa kufanya kazi.Watu wanaopatwa na Diabetes type II wanauwezo wa kupona wakifata matibabu ipsavayo na kula healthy pamoja na mazoezi.Waathirika wa ugonjwa huu hutibiwa kwa vidonge kwasababu wengi wao wanao uwezo wa kuproduce homoni ya insulin ijapokuwa inakuwa sio ya kutosheleza.Kuna uwezekano pia waathirika wa ugonjwa huu wakapoteza kabisa uwezo wa kutengeneza inslin na hatimae kuhitaji sindano kama wa Type I.
- Kuna kisukari cha mimba vilevile ambacho huwapata wajauzito.
Kuna uzi tofauti ambazo zimeanzishwa kuhusu mjadala wa ugonjwa huu..Nakushauri ujaribu kuperuzi utajifunza kitu!!