TATIZO LA ELIMU YETU

Remark

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
479
931
Leo wakati naangalia kipindi skonga cha EATV nimeshangaa kuona wanafunz wa secondary wakishindwa kujibu maswali ya kawaida tu na mengine hadi ni ya shule ya msingi kwa mfano mtoto wa kidato cha pili hajui Nigeria inapatikana upande gan mwa bara la Africa wakati hilo swali hata mtoto wa darasa la tano anaweza kujibu. Ni aibu sana kwa level ya mtoto wa kidato cha pili kutokujua kitu kama icho,sasa sijui tatizo ni elimu ndo shida au ni ujinga tu wa uyo dogo lakini hii inatutia aibu sana hasa ukiangalia ni television inayotazamw Africa ya mashariki
 
Laweza kuwa ni tatizo la mwanafunzi binafsi la kama swali hili wanafunzi wa kidato cha pili nchini wote hawalijui au angalau 50% hawajui,hapo tungelaumu mfumo
 
Kwa hiyo unataka kusema huyu mtoto hakupita darasa la tano! Au huko napo hakufunzwa jambo hilo!
 
Sasa wewe unashangaa dogo kushindwa kujibu swali! Hujashangaa mtoto kufaulu na hajui kuandika jina lake mwenyewe? Kupuuzwa kwa Elimu Tz ndiyo sababu kuu ya umaskini.Kuna wengine humu husema 'ualimu ni kazi ya laana'.mwl anajitoa kwa moyo kufungua ubongo wa mtoto lakini hathaminiki,anaishi kifukara na akiwa na bodaboda ya mkopo anarushwa kwenye TV ata hafanyi kazi.Acha tuaibike tu maana hakuna namna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom