Mfumo wa kutahini watoto ubadilike

Mfumo wa kutahini watoto ubadilike

kachwankizi

Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
99
Reaction score
158
Napendekeza mfumo wa kutahini watoto ubadilike. Ni kumuonea mtoto wa sekondari Kwa kumuuliza mambo aliyo jifunza miaka minne Kwa muda wa masaa matatu. Au mtoto wa darasa la Saba kumtahini Kwa masaa mawili mambo aliyo jifunza miaka Saba.

Ndani ya miaka minne maeneo aliyojifunza ni makubwa hivyo ni ngumu kujua area of concentration. Hata vyuoni mfumo ulibadilika Kuna mfumo wa semister.Ukifanya mtihani wa semister Kwa kozi Fulani mmetokana.

Watu wazima wenyewe wakienda semina ya SIKU kama tatu mwishoni wakipewa mtihani hawapati wanachemsha. Iweje mtoto akumbuke mambo ya miaka Saba au minne ndani ya masaa alafu useme unampima intelligence!

Napemdekeza Kwa sekondari mtoto akisha tahiniwa kidato Cha pili habari ya mada hizo awe amemalizana nazo. Apige tena miaka miwili atahiniwe Kwa mada za kidato Cha tatu na Cha nne. Baada ya muda tutafikia utahini wa mwaka mmoja mmoja.
 
Kumbuka bado tuna elimu inayounda pyramid. Wengi chini, wachache juu. Hivyo lazima watu wafyekwe.

Hapo labda tubadili malengo ya elimu kwanza.
Isiwe hii ya kutengeneza waajiriwa.
 
Back
Top Bottom