gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,307
- 3,335
Lile tatizo lakimfumo lililohubiriwa kwa muda mrefu na wapinzani sasa halizungumzwi tena na wala halisikiki.
Tuliambiwa kwa serikali ya CCM hata angeshuka malaika bado angeshindwa kuongoza Tanzania kwani mfumo mzima umeoza.
Tuliaminishwa muarubani pekee wa tatizo hili lakimfumo ni katiba mpya ya Warioba katiba ambayo haikupatikana.
Kwasasa tunasikia tatizo jipya kabisa kutoka kwa wapinzani kwenye serikali hii ya awamu ya tano nalo ni demokrasia.
"Kwakweli nimeanza kum miss Kikwete".Hii ni kauli ya G Lema alipokua akilalamikia ukosefu wa demokrasia na kuanza kumkumbuka JK ambaye kipindi cha utawala wake walimpinga na kuonekana hakuna alilolifanya.
Yapo maswali ya msingi yakujiuliza je Mh Magufuli amefanikiwa kuubadilisha mfumo bila yakuleta katiba ya warioba?
Pale mwanzo kwenye uongozi uliopita tuliambiwa na kimsingi wakati fulani ndivyo ilivyokua kwamba serikali ilikua ikicheza beat ya wapinzani.
Ila kwa sasa wapinzani wanaonja joto ya jiwe kwani sasa wanalazimika kucheza beat ya serikali na kwa bahati mbaya beat wanazo chaguliwa wacheze hawazipendi na wanalazimika kucheza kwa nguvu.
Kimsingi hali kwa wapinzani imekua mbaya kila kukicha wamekua wakihaha pasipo mafanikio.
Kimsingi wapinzani wanakazi yakuisoma serikali ya Magufuli na kutambua ni style gani mahususi ya siasa itakayoweza kwenda sambamba na uongozi wa raisi Magufuli.