Tatizo la ajira....

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Hello JF,

Nilishawahi kuleta thread,kuwe na scholarships programs(sijui kama zipo)..zinazolenga ku stimulate minds za walioko vyuoni kuja na mawazo ya kutoa ajira kwa wengine....hii sio tu itabadilisha mtazamo wa wasomi wengi sasa hivi ambao wana mawazo ya kuajiriwa,kuanza kufikiria kujiajiri na kuajiri wengine…..

second,ni ku revamp education system yetu,sababu kelele humu nyingi ni kuwalaumu 'wasomi' wetu waliohitimu kuwa wajiajiri,bila kufikiria kwa undani kuwa huko chuo hakujawaandaa au elimu waliyopata huko sio yenye kuwaandaa wajiajiri...so,contents za courses nyingi zinabidi zibadilishwe kutoka ma theories ya kucramm mpaka elimu ambayo iko practical.....na mazingira halisi,kwa sasa the whole education system inawa fail wasomi wetu,wengine kufikiria kwamba walipoteza muda kusoma….

Pia,kama climate imechange kutoka soko la kuajiriwa mpaka kujiajiri then,na sisi tubadilike badala ya kuwasomesha watu courses ambazo baadae watashindwa kuzitumia baadae….,tubadilishe masomo 3/4 iwe ni masomo ambayo watu wanaweza kujiajiri baadae…kusomesha mtu akakariri akapata cheti..hii ni wastage of resources/time...I believe tukianza kubadilisha mind set za vijana walioko chou wajiandae kujiajiri na kutoa fursa kwa wengine,tutamove forward...masomo mengi tu yapo practical....biashara,teknolojia,kilimo,electronics...etc
 

mkuu lipia tangazo,jukwaa la matangazo hulijui AU ??πŸ˜•πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘
 
Mi nadhani wanaongea tu hivi ni nchi gani ina program za kujiajiri kwenye elimu yake.
Kujiajiri kuna hitaji moyo sana, sisemi haiwezekani lakini ni ngumu na hii sio kila mtu anaweza.
Vilevile inategemea umesomea nini, hata kozi zinazoweza kujiajiri bado watu wameajiriwa. Wapo Madaktari wamefungua vijiofisi vyao na wanapata wagonjwa lakini wa cash, wagonjwa wa bima hawawapati. Jiulize Nurse anajiajiri vipi?! Au Mwalimu anajiajiri vipi? Hii naongelea ndani ya taaluma zao.
Ajira muhimu, lakini first lady wangu Rebeca 83 hizo scholarship zikiwepo unawapeleka wapi kwenye mitaala ya kujiajiri?! Labda tukiingia madarakani tuseme ni lazima kila graduate aende kusoma miaka miwili VETA au SIDO kozi aipendayo ili wakikosa ajira ya degree zao wafanye hizo walizojifunza huko vocational school na SIDO. Isiwe mandatory kwenda JKT kujifunza uzalendo badala yake waende VETA, labda hii itasaidia ingawa nitaitwa TOPE, kinyume cha J IWE.
Maana dunia nzima ukizunguka utakuta wapo walioajiriwa na wapo waliojiajiri. Ajira sio lazima zitengenezwe na serikali, ukianzisha mgahawa ukaajiri wapishi na wahudumu wengine, unakua umetoa ajira.
Lakini scholarship mbona zipo, tatizo hata wanaozipata wakirudi wanataka kuajiriwa.
 
my dear nilikua natafuta practical solution ya tatizo la ajira nchini,

ukiponda,maanake uje na alternative solution....

huku mnawabeza wahitimu 'wajiajiri' wakati system tayari inawa Fail big time...wengi wamejaza ma theories kichwani...

hakuna mantiki uitwe engineer wakati kipato chako hakimjazidi mkulima...kitu ulichomzidi ni theories kichwani, sidhani kama kuna ubaya wote tukiwa wakulima...kuliko kung'ang'ania ma course ambayo hayatusaidii...

Si kweli kuwa dunia nzima hamna somo la kujiajiri,nimeona one of the modules somewhere ni ' employability skills' ambapo students wanafundishwa how to sell themselves kwenye soko la ajira/kuajiriwa..hii inaweza kubadilishwa kulingana na mazingira yetu,tukaweka unit ya kujiajiri.mtu ajiandae kukabiliana na hali halisi ya mtaani…..pia kuna course work/research nimeona tena mahali mwanafunzi anapewa topic aandike course work barua kupeleka kwa prime minister jinsi tatizo Fulani linavyoisumbua jamii na kuandika recommendation,huoni kama tunaweza employ hii kitu katika mitala yetu ili i stimulate minds za wanafunzi kuja na mambo yatakayosaidia jamii including unemployment...………………...

Yes,serikali lazima iingilie kati,course zenye kutoa watu watakaoweza kujiajiri serikali inaweza kupunguza fees...labda 20% off....kuwachagiza watu wazisome kwa wingi….watu wakitoka na kujiajiri/kuajiri wengine itapunguza mzigo kwa serikali...na ishu sio kuwa haijawahi kufanyika katika nchi nyingine,inabidi sisi kwa sisi tuangalie tunahitaji nini halafu ndio tujue tufanyaje kuitatua hii changamoto...I guess ndio maana hata madaraja yetu yanavunjika watu wamesoma mambo general ya madaraja wakati tunachohitaji ni somo SPECIFIC na mazingira yetu..tusijenge daraja mvua ikinyesha tu msala...
 
Mimi naomba nitofautiane na wewe Rebecca kwenye hili. Mawazo yangu ni hivi: Huu uzalendo tunaouimba siupingi lakini, binafsi dunia hii yetu sote mungu aliumba tuishi. Tungetafuta mitaala hata kwa kuiba au ku-copy ya wenzetu walioendelea pia tuajiri walimu toka nje waje kutufundisha. Kisha tukimaliza tusambaze watanzania huko duniani kila fani. Mwisho wa siku tutakuwa tumepunguza tatizo la ajira nchini hii iwe ni long term. Short term tuwasaidie vijana waende huko nje wakatafute maisha, wapo watakao soma wapo watakao fanya kazi za viwandani. Cha muhimu kila kijana awe na ajira. Kuliko hii kuzungushana humu, mara JKT mara sijui unawapa mchinga vitambulisho, kesho wengine wanamwagika kutoka primary hadi vyuo vikuu hawana ajira, unagawa vitambulisho mwisho nchi nzima tutavivaa maana hakuna ajira.
Hizo course za kujiajiri hazisaidii, hata waliosoma entrepreneurship wanatafuta ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…