Tatizo la ajira nchini, huwezi amini kuna watu wameajiriwa zaidi ya sekta moja Serikalini

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,700
22,740
Habari wana Jamii Forums,.

Huku wananchi tukilalamika kuhusu suala la ajira nchini kwetu tambua kuna watu wenye ajira zaidi ya moja ndani ya serikali.

Siongei bila facts kwani kuna jamaa wangu wa karibu sana ana ajira mbili tofauti ndani ya serikali hii inayotuambia ajira zimekuwa chache serikalini na hawawezi kuajiri watu.

Binafsi nilishangaa sana maana hajawahi kunieleza kuhusu hilo jambo mpaka nilipombananisha wakati akilalamika mshahara wake kuchelewa kuingia katika akaunti zake mbili tofauti miezi michache iliyopita.

Najiuliza hakuna namna ya kufanya monitoring kuhakikisha mtu hapewi ajira zaidi ya moja katika mashirika ya umma huku wananchi wengine wakikosa hata hiyo moja?

My Take: Kwa hali hii ya mtu kuweza kuwa na ajira zaidi ya moja serikalini basi tatizo la upatikanaji wa ajira katika mashirika ya umma halitakwisha kamwe.
 
Hairuhusiwi kisheria, na kama ni kweli, basi hiyo mishahara yake haitoki Hazina, ni lazima watambamba!
 
Haiwezekani kwa kuwa system inayotumika ni moja na haiwezi ika accept majina matatu yanayofana labda kama antumia majina tofauti kwenye hizo ajira zake.
 
Hii ni hatari?
huyo jamaa ni mhujumu wa uchumi... tafadhali chukua hatua... mwivi kabisa huyo!!!
 
hata mimi nimeshasikia hiki kitu,wanaitwa waajiriwa hewa,hutumia majina tofauti
 
Sure,hili ni tatizo kubwa sana na mishahara mingi hewa hulipwa watu hao hao wa serikalini,yaani wizi mkubwa kabis na wa namna hii unafanyika na serikali haijui au inajua alafu haichukui hatua,xaxa wewe lmeta uzi,kwa kuonesha uzalendo na kusaidia kupambana na matatizo ya ufisadi inabidi uifuate vyombo husika na wamchunguze huyu mtu.
 
Kwanza hupaswi kushangaa.Rais wako mwenyewe anaongoza kuajiri watu ambao atayri wana ajira zao.Mbunge ile ni ajira.Mkuu wa mkoa ile ni ajira.Mkuu wa Wilaya ile ni ajira. Sasa tazama kama wapo wenye vyeo hivyo wakati huo huo ni wabunge. Katibu mkuu wa chama cha siasa ile ni ajira pia kwani analipwa.Sasa niambie hakuna katibu wa chama cha siasa wakati huo huo ni mbunge,na ni waziri? Huko kote anapata mishahara yake. Cheo kama cha Mwigulu kile kisingewezekana kupewa mtu mwingine? Christian Ishengoma na Stella Manyanya sio ajira zile? Ungepewa wewe ukuu wa mkoa ungeshindwa kumudu? Wazira aliwahi kupewa cheo na Baba wa Taifa akiwa chini ya umri wa miaka 32.Acha tu wapate.Lakini mchawi wako ni CCM yako na wahazini wao.
 
Sure,hili ni tatizo kubwa sana na mishahara mingi hewa hulipwa watu hao hao wa serikalini,yaani wizi mkubwa kabis na wa namna hii unafanyika na serikali haijui au inajua alafu haichukui hatua,xaxa wewe lmeta uzi,kwa kuonesha uzalendo na kusaidia kupambana na matatizo ya ufisadi inabidi uifuate vyombo husika na wamchunguze huyu mtu.

una point nzuri tatizo ni hapo xaxa badala sasa sijui ndo kukua kwa lugha? Mh! Janga hili
 
Back
Top Bottom