Tatizo la ac kwenye gari yangu

MTINGIJOLI

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
1,383
1,358
Habari Zenu Wakuu, Poleni Na Hongereni kwa Majukumu.

Nina Toyota Alphard ambayo haijamaliza Miezi miwili tangu nimeichukua, Sasa ghafla AC ikawa Hapozi Nikapeleka kwa Wale Jamaa Wanaojaza gesi, Wakaicheki, Wakaniambia gesi imeisha, nikawaambia Wajaze, Wakabadilisha na Fuse sijui Iliungua , Kweli baada ya Pale Ac ikawa Inafanya Kazi Vizuri tu, Leo ghafla Nawasha gari, Tatizo limejirudia, Na Hili Joto la Dar, nimeanza Hata kulichukia Gari lenyewe.

Naomba kwa anaefahamu tatizo hili linasababishwa na nini? Au wapi naweza kupata fundi mzuri Maana natupa hela bila Mafanikio.

Natanguliza Shukrani
 
Leakage...kuna leakage mahali...mwambie fundi akague vizuri azine sehemu inyovuja maisha yatakuwa mazuri
 
Hapo bila shaka gari yako itakua kuna pipe inavujisha au kuna kitu kama chujio la ndani lilalohifadhi gas ya Ac limekwisha so lazima livuje na ni mafundi wachache wanaoweza kugundua hiyo
 
Nashukuru Sana Mkuu, So Wale Wakujaza Gesi Wanaweza Kufahamu au Kuna Mafundi Maalum Wa AC
Sometimes yes...sometimes no.....
Kuna wengine wanajua kujaza gesi tu..
Ila kuna wengine wanaweza kufanya marekebisho yote yanayohusiana na AC
 
Kuna jamaa nasikia yupo Kariakoo anaitwa Fundi Makofia. Nina tatizo same kama wewe. Natafuta tu muda wa kwenda. Jamaa ndio mkali wa AC mjini. Nikipata namba zake nitakucheki.
Huyo fundi anapatikana sehemu gani ya Kariakoo maana Kariakoo kubwa sana
 
Back
Top Bottom