Tathmini yangu baada ya uchaguzi mdogo Chalinze

Tathmini yangu baada ya uchaguzi mdogo Chalinze

Peter Dafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
394
Reaction score
272
Nimekaa na kutafakari sana kuhusu hizi chaguzi tulizofanya katika majimbo ya Kalenga na Chalinze ambapo Ccm imeibuka kidedea kwa kishindo kikubwa.

Nilichogundua ni hatua na maamuzi ya wananchi kuonesha kuwa bado wana imani na Ccm.Lakini tathmini yangu itaangalia mambo makubwa mawili.

Moja ni nguvu ya viongozi ndani ya Ccm ambao walipewa jukumu la kuwanadi wagombea.Katika hili nitaangazia na kampeni ya Arumeru Mashariki.

Ridhiwani Jk ni mtoto wa rais ila pia ni Kada mzoefu wa Ccm ambaye habebwi kisiasa bali anapambana mwenyewe.

Sioi Sumari ni mtoto wa aliyekuwa Kada na Mbunge wa Ccm kabla ya kifo chake.Ila pia Sioi Sumari ni mkwe wa Mh. Lowassa ambaye anaamini ana nguvu katika jamii.Katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki huyu Sioi Sumari alishindwa vibaya sana.

Pamoja na kunadiwa vyema na kwa mbwembwe na baba mkwe wake ila bado aliangukia pua.Hapa ndipo jamii ilipojua kuwa Mh. Lowassa hana lolote kisiasa bali propaganda tu.Ila angalia namna Mama Salma alivyodhihirisha kuwa yeye ni mwamba wa siasa za ushindani katika uchaguzi wa Chalinze.

Hakuhonga,hakukejeli wala hakutukana bali alimwombea kura mwanaye na hatimaye wanachalinze wakakubali wakiwemo hadi jamii ya kifugaji iliyopo Chalinze.

Kwa mantiki hii jamii imegundua kuwa siasa ya Mh.Lowassa kwa Mama Salma ni dhaifu sana.Mh.Lowassa anapaswa ajipime sasa.Ndiye Waziri Mkuu pekee Tanzania aliyepewa jukumu la kumnadi mgombea wa CCM na akashindwa.

Angalieni namna Mzee Malecela alivyokuwa mwamba katika kampeni za zamani.Ni aibu kwa Mh.Lowassa.

Hongera sana kwa Mama Salma kwani hajapoteza jimbo.Kaongea akasikika na wananchi wakaheshimu maneno yake.

Kisiasa yupo juu sasa kuliko Mh.Lowassa.Ila pia nikija kwa upande wa Chadema ni kwamba wanachama wao wenye hasira na hatua ya uongozi wao kwa kumsimamisha nafasi zake Mh.Kabwe ndio zinawamaliza katika chaguzi hizi.

Wameona bora waipe kura Ccm.2015 tutaona mengi sana.People's power imekuwa devil's power sasa.Ni tathmini tu.
 
Wewe ni nani? Jitambue ndugu usifuate upepo!. Improve your idea, think big please! We sema tufanye nini sasa? Sio unathamini tu, what is your standing on this issue?
 
Asante kwa tathimini yako iliyojitathimini kuwa unachuki/wivu binafsi kwa Mh. Lowasa
 
hujui maana ya tathmini,hapa hujatathmini ila umesisimka
 
Inaonekana nguvu ya Mh. EL inakunyima usingizi mleta uzi huu.... jipange upya kwa tathmini nyingine kipenga kitakapopulizwa rasmi!
 
hujui maana ya tathmini,hapa hujatathmini ila umesisimka
 
chadema kila jambo wanaiga ccm .umeona wapi photocopy ikawa bora kuliko orijino'hawawezi kushinda hadi wajikane.
 
yaleyale ya kina LEMUTZ leo hii wabeba box wanajua vyema mambo ya uraiani wakati huku wamekimbia miaka zaidi ya 30,
pole sana ndugu LOWASA wakati wa kampeni za ARUMERU alikuwa ujerumani kwa matibabu ya macho
alifanya mkutano mmoja tu tena akuongea zaidi ya dakika 20
jitambue mkuu
 
Back
Top Bottom