Baada ya ziara za katibu mkuu wa ccm kumalizika kwa awamu hii ya kwanza, sasa tufanye tathmini kwa kifupi.
Kwanza nilishangaa kuona kinana kuanza ziara mara tu alipoteuliwa bila kufanya upembuzi wa kutosha juu ya mapungufu ya ziara za akina Nape na Mukama.
Inawezekanaje akawa anajua kila kitu mara alipoteuliwa na kwenda mikoani kuagiza, kukemea, kuonya na kutoa mikakati. Mbona mzee mangula katulia akijifunza na baadaye aje na mikakati ya maana.
Ndiyo maana sikushangaa niliposikia kuwa ziara za kinana zilikuwa zinafuata taratibu zile zile za kifisadi,kama vile kuchangisha kwa wafanyabiashara wa mtwara kwa ajili ya kugharamia ziara yake kule. Pia kutoa ahadi na maagizo yaleyale kwa serikali.
Kwa mfano, agizo la kutatua kero ya maji mjini sumbawanga lililotolewa na akina mukama na nape mwaka mmoja uliopita lilitolewa tena na kinana. Hatua hii ilisababisha watu wazomee.
Utaratibu wa kusombelea watu ili wajaze mikutano ulikuwepo pia katika ziara hizi za kinana. Pia kuwalipa baadhi ya watu ili washiriki katika misafara ya magari na mapikipiki uliendelea.
Kinana kushindwa kujibu kashfa dhidi yake binafsi ni doa jingine pia. Kashfa hiyo ambayo imeanza kuenea kwa kasi ya kimbunga ikipewa msukumo na ukimya wa kinana itakigharimu CCM. Katika siasa huwezi kujitakasa dhidi ya kashfa kwa kukaa kimya.
Waliokuwa wana matumaini na kinana imekula kwao.ni afadhali mukama ambaye alishindwa kazi kwa uzembe wake, lakini hakuwa na kashfa za ufisadi.
Kitu kingine ambacho kitamfanya kinana aiharibie ccm badala ya kuijenga ni nasaba yake ya kisomali. Kuna mahali nasikia watu walimuita tx, wakimaanisha mtu asiye mtanzania.hii itakazia hoja kwamba hana uchungu na nchi hii.
Nashauri Kinana afanye tathmini ya kina na aamue; ikiwezekana aachie ngazi kwa mapema.