Tathmini ya ziara za Kinana: Ameanza kwa kushindwa!

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Baada ya ziara za katibu mkuu wa ccm kumalizika kwa awamu hii ya kwanza, sasa tufanye tathmini kwa kifupi.

Kwanza nilishangaa kuona kinana kuanza ziara mara tu alipoteuliwa bila kufanya upembuzi wa kutosha juu ya mapungufu ya ziara za akina Nape na Mukama.

Inawezekanaje akawa anajua kila kitu mara alipoteuliwa na kwenda mikoani kuagiza, kukemea, kuonya na kutoa mikakati. Mbona mzee mangula katulia akijifunza na baadaye aje na mikakati ya maana.

Ndiyo maana sikushangaa niliposikia kuwa ziara za kinana zilikuwa zinafuata taratibu zile zile za kifisadi,kama vile kuchangisha kwa wafanyabiashara wa mtwara kwa ajili ya kugharamia ziara yake kule. Pia kutoa ahadi na maagizo yaleyale kwa serikali.

Kwa mfano, agizo la kutatua kero ya maji mjini sumbawanga lililotolewa na akina mukama na nape mwaka mmoja uliopita lilitolewa tena na kinana. Hatua hii ilisababisha watu wazomee.

Utaratibu wa kusombelea watu ili wajaze mikutano ulikuwepo pia katika ziara hizi za kinana. Pia kuwalipa baadhi ya watu ili washiriki katika misafara ya magari na mapikipiki uliendelea.

Kinana kushindwa kujibu kashfa dhidi yake binafsi ni doa jingine pia. Kashfa hiyo ambayo imeanza kuenea kwa kasi ya kimbunga ikipewa msukumo na ukimya wa kinana itakigharimu CCM. Katika siasa huwezi kujitakasa dhidi ya kashfa kwa kukaa kimya.

Waliokuwa wana matumaini na kinana imekula kwao.ni afadhali mukama ambaye alishindwa kazi kwa uzembe wake, lakini hakuwa na kashfa za ufisadi.

Kitu kingine ambacho kitamfanya kinana aiharibie ccm badala ya kuijenga ni nasaba yake ya kisomali. Kuna mahali nasikia watu walimuita tx, wakimaanisha mtu asiye mtanzania.hii itakazia hoja kwamba hana uchungu na nchi hii.

Nashauri Kinana afanye tathmini ya kina na aamue; ikiwezekana aachie ngazi kwa mapema.
 
Mkuu umenena huyu bwn ni boya kabisa,hasafishiki, ni mzigo kwa chama na mbaya zaidi sio mbunifu hana mvuto,tutamkumbuka mkama.
 
Vyama vya mageuzi inabidi wafurahie udhaifu wa chama kilichopo madarakani hakuna haja ya kuihurumia ccm zaidi ya kuipiga pini za moto inapokuwa imeingia mkenge.

Mi naona sawa tu kuingia kwa watu kama kinana ktk cc ya ccm ili kuharakisha kifo chake
 
bashe ,kinana,adeni rage ni watanzania wenye asili ya kisomali wanaong'ara ccm .hongera watanzania kwa kutokuwa na ubaguzi .sidhani kama sisi tukienda huko somalia tutapewa hata umonrta wa darasa
 
huna lolote la maana, mkabila we. wasomali wamekukosea nini, shida yako ni mtu mmoja anaekusumbua akili, sasa kipi kinacho kutuma kwenye umma mzima ambao haujakiletea shida yoyote.
 
Kitu kingine ambacho kitamfanya kinana aiharibie ccm badala ya kuijenga ni nasaba yake ya kisomali. Kuna mahali nasikia watu walimuita tx, wakimaanisha mtu asiye mtanzania.hii itakazia hoja kwamba hana uchungu na nchi hii.

Hili nalo neno la kutafakari.
 

Heri ufungwe kifungo ndani ya sufuria maana jua utaliona kuliko kifungo ndani ya mtungi maana kila siku giza!! Ukikubali kuongozwa na jangili basi na wewe ni jangili!!!
:horn::horn::horn::horn::horn:
 
Ina maana Kikwete amewahadaa wana ccm wenzake kwa kumtuma Kinana eti muuaji wa tembo ili akiue ccm pia kwa kuwa ana mbinu za hali yajuu katika kutekeleza mauaji.
 
Nashangaa ndani ya CCM huyu ndiye aliyeonekana anaweza "kukifufua" chama. Wenzake ndani ya chama wana imani naye, maana ni juzijuzi tu alitangaza kuachana na siasa lakini nini kimembadilisha mawazo?
 
si lile ganda la mua la jana alitoa sharti kwa Rais kama anataka awe makamu basi kinana ateuliwe?
 
Kinana hajawahi kuwa msafi. Uteuzi wake kwa ufupi unatiririka hivi " ndege wa aina moja huruka pamoja". Pia "ukinikuna mgongo wangu nami nitakuna wako", "nipe nikupe" nk

Kikwete ni fisadi papa, kama alivyo Kinana na wengine wengi CCM. Je sio dhambi kutegemea JK ateue mtu msafi? Alichofanya ndio sahihi kiroho na kimazingira
 
CCM kwa upofu wao wanadhani nguvu ya fedha itawaokoa. Kinana ataua tena tembo wetu kwa mamia kutunisha mfuko wa rushwa na ufisadi chamani
 
wakati wa uteuzi wake alimwagiwa sifa kumzidi hata JK. nadhadi kichwa kilivimba karibia mount kilimanjaro. sifa hizo zimeanza kumyumbisha hadi kutoa maagizo kibao. siku moja ataagiza rais asisafiri out hadi atakporuhusu yeye knn. pengine hilo litasaidia na pengine lisisaidie.
 
Umejawa na Hofu,woga Pamoja na chuki Mtoa mada. Kuwa na imani utamshinda adui yako.Kiri ushindi sio kinyume
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom