Tathmini ya uongozi wa awamu tano za Tanzania, Wakristo waliwekeza zaidi kwenye maendeleo ya vitu na Waislam kwenye maendeleo ya watu.

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
UTAWALA WA NYERERE (1961 - 1985)

Kazi kubwa kipindi hiki ilikuwa ni kujenga umoja wa nchi. Hata hivyo kiuchumi serikali ilisimamia kitu, uzalishaji, biashara, kupanga bei n.k. Kukawa na kauli za Chama kimoja kushika hatamu, Siasa ni kilimo, Siasa ni Uchumi, kutaifisha mali za watu binafsi ziwe za umma, kuanzisha vijiji vya ujamaa, ujamaa na kujitegemea, kilimo cha kufa na kupona, kukaza mikanda, n.k.

Hali za watu kiuchumi kwa ujumla zilikuwa duni kwa kuwa serilkali ilikuwa ni kila kitu, ndio inayotoa dira ya maisha na maendeleo.

Mwalimu yakamshinda, akaona atoke kwa staili ya kung'atuka (Kwa maksudi hakutumia kustaafu ama kujiuzulu).

UTAWALA WA MWINYI (1985 - 1995)

Huyu akaja na sera zilizo mpa uhuru mtu binafsi kuonesha talent yake katika kujiletea maendeleo (ruksaa), Tukaanza kuona sekta binafsi, soko huria, Vyama vingi, Ajira zikaongezeka, Watumishi wakaruhusiwa kufanya kazi zaidi ya moja, Biashara zikaongezeka hadi kwenye dhahabu, Wazanzibar wakaanza kudhubutu kudai nchi yao au la basi waruhusiwe kujiunga na umoja wa mataifa ya kiisalam (OIC) n.k

UTAWALA WA BENJAMIN MKAPA (1995 - 2005).

Huyu akaona sera za Mtangulizi wake za sekta binafsi ziliwapa watu nguvu za kiuchumi, ila hawakulipa kodi ipaswavyo na serikali ikawa maskini.

Akaja na Ukweli na Uwazi. Akabana vice, pesa irudi serikalini. Kodi ikakusanywa kweli kweli, pesa iliyopatikana, ikaenda Paris Club kulipa madeni ya nchi, mashirika na mabenki yakabinafishwa, Majengo ya serikali yakapigwa bei, Neno ujenzi wa miundo mbinu likachipuka. Watanzania wajasilia mali wakapungua sana kutokana na ukata au ukapa.

UTAWALA WA JAKAYA (2005 - 2015).

Huyu akaja na Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya na baadae Ari Zaidi, Kasi zaidi na Nguvu zaidi. Akajitahidi kujenga barabara zaidi, akatafuta wawekezaji na wafadhili zaidi, akajitahidi kuajiri zaidi na kuongeza mishahara, Mikopo ya mabilioni ya JK, akajitahidi kuongeza provision ya huduma za jamii kama shule nyingi, vituo vya afya, Madawa hospitalini na ukimwi n.k. Matumizi ya serikali kwa rasimali watu yakaongezeka.

Aliingia ikulu akiwa na degree moja akatoka akiwa profesa JK.

UTAWALA WA MAGUFULI (2015 - 2020)

Huyu kaja na hapa ni kazi tu. Asiye fanya kazi asile na afwee.

Matumizi ya serikali kwa rasilimali watu yamepunguzwa kiwango kikubwa sana, ajira mpya zipo kidogo sana, hakuna kupandishwa mishahara ila kwa sekta nyeti, Uhuru wa kisiasa watu umebanwa sana (narrowed)

Makusanyo ya kodi yamepanda haswa kwa kuziba mianya iliyokuwako kipindi cha JK toka bilioni 900 hadi trilioni moja na bilioni 300.

Matumizi makubwa ya serikali ni kujenga miundo mbinu, kulipa madeni, kununua ndege 7 ili kuimarisha sekta ya anga na utalii.

Ukiangalia kila awamu utaona ama ilikuwa na mrengo wa kuwekeza kwa vitu au kuwekeza kwa watu
 
Je unaweza kusema ni kwa sababu gani?
nadhani wakristo wanazingatia ile kanuni ya
mle nini mvae nini, tizameni ndege wa angani hawalimi ila wanakula kama kawaida. kwahiyo ni kuwekeza tu kwenye miradi swala la kula mtajua wenyewe mtafanyaje
 
Kwa maelezo yako unatuaminisha utawala wa 2005 -2015 mpaka sasa ndo bora kuliko wote nadhan hii thread yako itadumu 2025 ndo nitatoa comment nyingine. ...tuombe uzima
 
Huh uzi ni wa kibaguzi!
 
Kwa maelezo yako unatuaminisha utawala wa 2005 -2015 mpaka sasa ndo bora kuliko wote nadhan hii thread yako itadumu 2025 ndo nitatoa comment nyingine. ...tuombe uzima
kwa maoni yangu bado JPM hajamfikia kikwete kwa uchumi kiujumla ila awamu hii inajitahidi sana kufanya branding kuliko awamu ya nne nadhani ni kwa sababu ya uwezo wa kiuongozi awamu ya nne ikiamini katika kutimiza wajibu na kuleta ahueni kwa watu waliokuwa wamesinyaa ya sasa inaamini katika self branding,postive legacy japo ukizidisha zana kuamini katika legacy ya pekee yako na kusahau mnyororo wa maendeleo unaweza hususani nchi hizi za africa ukashia njia na kufeli au kuacha nchi katika madeni makubwa kwa kuwa utataka kufanya vitu nje ya uwezo halisia ili uonekane ulikiwa tofauti lakn muhimu katika uongozi ni kusukuma maendeleo has ya watu yanayochagizwa na vitu
 
Back
Top Bottom