Tathmini ya 2013: JE, MBUNGE WAKO AMEWAJIBIKA IPASAVYO JIMBONI AU ALIKUWA NI MZIGO TU

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,463
0
Nini maoni yako kuhusiana na uwajibikaji wa mbunge wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo jimboni?
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,360
2,000
Wa kijijini kwangu (Jimbo nililozaliwa) ni mzigo mzito kuubeba, ni sawa na gunia la mawe!!! Wa jimboni kwangu mjini amejitutumua tutumua kidogo lakini jinsi miaka inavyoenda anaonekana kuwa Mzigo!
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
36,226
2,000
Mb wangu nliyemtaka kura hazikutosha ila waliomchagua wao mda mwingi yupo nje ya nchi kazi yake ni ku-update status tu facebook.
 

bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,772
2,000
Mb wangu, hata jina lake nishalisahau, hata sijui kama yupo, nasikia huwa anawaambia anaokutana nao kuwa miaka 5 ni mingi sana! Anatamani kutua mzigo, ila siamini maneno hayo
 

lulambo

Member
Aug 31, 2013
26
0
Mi wng ni Emanuel nchimbi, sifuri kbs, na hukumu yake ya kwanza imepita kapigwa chini uwaziri, ya pili 2015
 

Pyepye shola

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
296
0
Mi wangu kbona hachangii chochote bungeni... akirud ileje anapita kwenye virabu vya pombe na kuwanunulia pombe kibao... huu nao ni mzigo...
 

Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,857
2,000
Wangu kinondoni Yuko poa! ila rafiki yangu anakaa jimbo la ubungo anasema wakazi wa jimbo la Mnyika hawana hamu nae tena bla bla nyingi na haonekani tena maji hakuna kama jangwani, wamepanga kumpiga chini 2015.
 

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,023
2,000
Mtutura na Ramo Makani bora ubebeshwe gunia la viroboto sio hawa. Barabara mbovu,elimu duni,maji duni,vitu bei juu. CHADEMA nisaidieni TUNDURU 2015 nimng'oe mmoja wapo kati ya hawa. Kama CHADEMA tuko pamoja mni pm.
 

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,082
1,195
Nini maoni yako kuhusiana na uwajibikaji wa mbunge wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo jimboni?


Mbunge wangu huku vunjo naona kachoka mbaya. Ni mzigo usiobebeka. Tulimtuma kazi moja tu kuisimamia bei ya kahawa. La kushangaza kwa kipindi cha miaka miwili tu kahawa imeporomoka toka TShs5000/= mpaka TShs 1000/= kwa kilo.
 

Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,428
1,500
Njombe kaskazini Deo Sanga jah people yan sio mzigo ni zigo halijawajibika ila katiba mpya italiondoa mana lina elimu ya darasa la pili lilikimbia shule kwa hiyo halijui hata wajibu wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom