jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,227
- 25,039
Wanajamvi,
Humu ndani, nimegunduwa jambo moja. Pale inapokuja kwenye ugombea urais, majina mengine yanayotajwa tofauti na lile la mgombea wa CCM, kwa kiasi kikubwa, hawapewi nafasi haya kidogo! Sababu kubwa inayotumika, ni kwamba NEC itatangaza mgombea wake iwe iweje!
Lissu aliulizwa swali kama watashiriki uchaguzi mkuu chini ya mazingira yaliyopo. Akasema hawawezi kuacha kushiriki uchaguzi. Pamoja na wasiwasi ambao wananchi wengi walionao kuhusu uhuru wa tume ya uchaguzi na malalamiko ya “goli la mkono”
Hili likanifanya nijiulize kama walishawahi kulifanyia tathmini “goli la mkono”. Goli ambalo Nape alivunjika mkono akiwa kwenye kampeni na jitihada za kupiga goli hilo “la mkono”, na kuna tetesi kuwa hatoshiriki tena kwenye mchezo huo! Lakini hilo haliondoi ukweli kuwa bado kuna ambao ndani ya ccm watakaoucheza mchezo huo!
Je upinzani mmejipanga vipi? Nina amini kabisa kama siyo Lowassa, kungekuwa na vurugu kubwa za wananchi waliiona kuwa wamedhulumiwa!
Ni ukweli kuwa uchaguzi huu ujao utatupiwa jicho sana! Je ukitokea mchezo mchafu, nini kitafanyika kukabiliana na hali hiyo? Inashangaza sana kuona kuwa kuna watanzania wanaongea kwa kujiamnini kabisa hadi unajiuliza maswali kama uchaguzi ni jambo la muhimu chini ya mazingira kama hayo! Pamoja na kwamba watanzania ni waoga, bado ninatoa ushauri kuwa ccm msithubutu tena kupiga goli la mkono, maana mtajuuta na kupata taabu sana!
cc Nape Nnauye britanicca