Unaweza kutueleza huyo wandosya kafanya nini hapa Tz,toka aanze utumishi wake kafanya nini au kasimamia jambo gani likapata ufanisi mkubwa? Acheni porojo bwana!
Mkuu, una mtazamo uliopotoka sana kuhusu uraisi. Uraisi sio tuzo au medani wanayopewa watu waliotufanyia mambo mazuri hapa nchini.
Hata hivyo labda turudi nyuma kwa kutumia kigezo chako "katufanyia nini". Pale Mwinyi alipoteuliwa kuwa mgombea uraisi alikuwa amewafanyia nini Watanzania? Au hata Mkapa, na Kikwete, walikuwa wamewafanyia nini Watanzania kilichofanya wastahili kupewa nafasi ya kugombea Uraisi? Labda wewe unajua, mie sijui, na wala sikuona wwote hawa walichowafanyia Watanzania hadi kiwafanye wastahili uraisi. Lakini naelewa kwamba huenda walionwa kuwa na sifa za kuwa maraisi wetu, na sifa hizo hazikutia ndani kile walichokuwa wamewafanyia Watanzania.
Huenda kati ya Mkapa na Mrema, kwa kutumia kigezo chako Mrema alistahili kuwa raisi kuliko Mkapa - lakini swali la msingi ni kama Mrema alikuwa na sifa za uraisi zaidi ya Mkapa.
Hivyo basi, Magufuli anaweza akawa amesaidia sana kusimamia ujenzi wa barabara nchini na akastahili pongezi na wote tukasema Magufuli ametoa mchango mkubwa kwa Watanzania - sasa je tutamchagua Magufuli kuwa raisi kwa sababu alisimamia vizuri ujenzi wa barabara zetu? Toka lini kusimamia barabara inakuwa sifa ya kuwa raisi mzuri?
Katika mfano wa Tanzania kuwa kama wasafiri wa ndege niliotaja hapo juu; ukiuliza Mwandosya katufanyia nini ni sawa na mtu kusema mhudumu wa ndege aliyetudumia vizuri sana ndie anastahili kuchukua jukumu la kuwa pilot katika safari yetu.
Tutakuwa tumepotoka sana ikiwa tutadhani sifa ya kuwa raisi wa Tanzania ni kutokana na yale uliyowafanyia Watanzania. Wapo wengi waliowafanyia Watanzania mambo makubwa, tunawapongeza na huenda wanastahili medani. Lakini haina maana wana sifa ya kuwa maraisi wa Tanzania. Sifa za mtu kuwa raisi wa Tanzania ni kutia nani kuwa decisive, patriotic, assertive, visionary, wisdom, intelligence, exposure, diligence, leadership capability, kuheshimika na watu wa ndani na nje, kuheshimiwa na baraza la mawaziri na taasisi za serikali, nk. Nitakuwekea post juu ya hili ili ufanye tathmini.