Tatafakari juu ya Tamko la Prof. Mwandosya

Tatafakari juu ya Tamko la Prof. Mwandosya

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,107
Reaction score
28,608
Wiki iliyopita nilitoa post mbili ambazo kwa namna fulani zina mkaribio mkubwa na habari iliyotoka hivi karibuni kwamba Prof. Mwandosya ameonyesha nia ya kugombea uraisi. Nilisisitiza sana kwamba mimi sina ushabiki na Chama chochote cha siasa nchini, hasa pale wengi walipodhani nilikuwa nikimfanyia kampeni Makamba.

Post hizo zilisema;

1.
Ushauri wa Bure kwa Kikwete Kuhusu Makamba Kutaka Kuwa Rais
2. Je unadhani Salim Ahmed Salim au Mwandosya wangefanya vizuri zaidi ya Kikwete?

Katika post yangu namba 1 wengi walidhani niko kambi ya Makamba, hasa pale niliposema Tanzania imenajisiwa sana kiuongozi na kupoteza heshima ya Ofisi ya Raisi, Bunge na Baraza la Mawaziri. Nikasema kwamba "ikiwa Makamba ana uwezo wa kurekebisha hili kwa hivi sasa, wale tulio na uchungu wa nchi yetu tutasema hewala, acha Makamba aje, ili mradi umri wake unaruhusiwa kikatiba. Kwetu sisi si busara kusema acha nchi iendelee kuharibika hadi Makamba afikishe umri aliokuwa nao JK alipopitishwa kuwa mgombea wa uraisi. Huo utakuwa ni wendawazimu. Kuendelea kungoja katika hali tuliyo nayo ni ku-compound uozo wa tatizo la kiuongozi linalotukabili kwa sasa. Suala la msingi ni kama Makamba ndiye desparate remedial solution tunayohitaji, na kama watu wenye akili hatutajadili umri wake katika hili ".

Katika post No2 kuhusu kama Mwandosya angekuwa Raisi badala ya JK nilisema kwamba "Kwa mtu kama Mwandosya nadhani tungeshuhudia mawaziri wengi wakifungwa au kufukuzwa kazi, na Takukuru na ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu kupewa uhuru na meno zaidi. Pia ninaweza kusema kwa uhakika kwamba chini ya JK tumekuwa na urafiki na mataifa mengi ya nje, lakini ni urafiki ambao haujapelekea sisi kuheshimiwa kama taifa bali urafiki wa kimaslahi kwa hao wanaojifanya rafiki zetu. Chini ya Mwandosya naona kama heshima yetu kama taifa ingepanda sana, na urafiki ungeimarishwa katika misingi ya kuheshimiana na sio kutumiwa. Kwa hiyo binafsi naona Mwandosya angekuwa makini na mkali zaidi ya JK. Mawaziri wangemheshimu sana na kumwogopa".

Basi nikiwa Mtazania mwenye mapenzi na uendelevu wa nchi yangu, ninachowasihi Watanzania wote walio CCM, Chadema NCCR, TLP na kwingineko, kuacha ushabiki wa kisiasa na kutafakari sana juu ya muelekeo wa nchi yetu katika kipindi hiki. Tutafakari tamko la Mwandosya kwa makini, hasa kuhusiana na niliyoandika hapa juu na katika post nilizotaja. Tanzania ni kubwa sana zaidi ya vyama vya siasa, na inapita katika kipindi muhimu sana kuelekea uchumi ambao unaweza ukaifanya kinara wa maendeleo katika Afrika, na hilo litawezekana tu tukiwa na mtu makini kama Raisi ajaye, anayeweza kuheshimiwa sana na wananchi, mawaziri wake, na watendaji wa serikali, na vile vile viongozi wa mataifa ya nje.

Mbele yetu tuna nafasi ya kipindi cha miaka kumi cha kutembea kifua mbele kama Watanzania, au kujutia uamuzi tuliofanya kwa misingi ya ushabiki wa kisiasa, uliofanya tuamue mambo kutokana na misingi ya uchama, makundi, ukabila, udini, uzee au ujana kama watu wasio na akili timamu.

Mtu yeyote anayezungumzia mambo ya rais kutokea CCM hana akili timamu.
 
...huu uraisi umekuwa raisi sana kiasi kwamba unaweza kumchomo mgonjwa dripu za dawa na kumtoa wodini na kumpeleka ikulu aongoze nchi...wagojwa wanataka uraisi,wahuni wanataka uraisi,wazinzi wanataka uraisi,walarushwa wanataka uraisi na mafisadi ndio kabisa hawataki kuukosa hasilani....sasa nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazim,kila mtu anaona anaweza kunyoa...
 
...huu uraisi umekuwa raisi sana kiasi kwamba unaweza kumchomo mgonjwa dripu za dawa na kumtoa wodini na kumpeleka ikulu aongoze nchi...wagojwa wanataka uraisi,wahuni wanataka uraisi,wazinzi wanataka uraisi,walarushwa wanataka uraisi na mafisadi ndio kabisa hataki kuokosa....sasa nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazim,kila mtu anaona anaweza kunyoa...
Watu wanaongozwa na mihemuko ya bangi tu wanadhani urais ni kutanua vidole badala ya kutanua akili.
 
Unamfagilia Mwandosya kijanja.Huyu ni mccm na ccm hawatoweza kufagia
uchafu wao walioulundika kwa miaka zaidi ya hamsini. Upepo uvumao sasa hivi
ni upepo wa kuweka chama kingine madarakani. Tuwaache akina Makamba, Membe
Sita, Lowassa waendelee kulilia pipi!
 
Mtu yeyote anayezungumzia mambo ya rais kutokea CCM hana akili timamu.

Mkuu waonaje basi, ni akili timamu kwa mtu kusema mtu yeyote yule hapa nchini ana sifa za kuwa raisi wa Tanzania ili mradi tu hatoki CCM?
 
Unamfagilia Mwandosya kijanja.Huyu ni mccm na ccm hawatoweza kufagia uchafu wao walioulundika kwa miaka zaidi ya hamsini. Upepo uvumao sasa hivi ni upepo wa kuweka chama kingine madarakani. Tuwaache akina Makamba, Membe Sita, Lowassa waendelee kulilia pipi!

Mkuu hapo ndipo tunapotofautiana kimawazo. Mie ninaamini kwa dhati tazizo la CCM sio CCM kama taasisi ya kisiasa bali baadhi ya watu ndani ya CCM. Na hili sio kwa CCM tu, hata Chadema, TLP, CUF nk kuna uozo ambao wasipokuwa makini utawaharibia mambo yao. Hili dudu la CCM kama taasisi ya kisiasa lina sera nzuri tu, zinazokubalika. CCM ni nyumba nzuri tu kwa nje.

Ikiwa ndani ya nyumba ya CCM, au Chadema, au CUF, au NCCR nk kuna uozo, suluhisho sio kubomoa nyumba hizo bali ni kutafuta mtu jasiri ndani hizo nyumba na kumwambia fagia uozo ndani ya nyumba yenu na kuutupa jalalani na kuuchoma moto.

Nimesema huko nyuma, kwamba kuna watu ndani ya CCM, Chadema, CUF, NCCR nk naweheshimu sana, na pia kuna watu ndani ya vyama hivi ninawadharau sana. Lakini sasa hawa watu ninaowadharau ndani ya hivi vyama hawatanifanya nihukumu vyama vyao kwamba havifai kutoa kiongozi wa Tanzania.

Je, waona ni sahini tumkuhumu mtu kama Mwandosya, ambaye wala sio hata Mwenyekiti au kiongozi wa juu wa CCM, kwa uozo ulio ndani ya CCM? Au je, ni sahihi kumhukumu Nassari, mbunge tu wa kawaida wa Chadema, kwa uozo wowote utakaonuka ndani ya Chadema?

Tanzania ni kama tuko ndani ya safari ya ndege. Sasa ni akili kuona rubani wa ndege anahatarisha maisha ya abiria wake halafu tukaishia kuwalaumu wahudumu wa ndani ya ndege kwamba na wao wamechangia sana kufanya safari yetu iwe hatarini?
 
Mimi nipo Timu ya Kigwangalaa,watanzania tupeni nafasi tena tuwape utumishi uliotukuka kupitia Kigwa,rais kijana mwenye maono mapya !
Tanzania ya neem,a chini ya Kigwa inawezekana!
 
...huu uraisi umekuwa raisi sana kiasi kwamba unaweza kumchomo mgonjwa dripu za dawa na kumtoa wodini na kumpeleka ikulu aongoze nchi...wagojwa wanataka uraisi,wahuni wanataka uraisi,wazinzi wanataka uraisi,walarushwa wanataka uraisi na mafisadi ndio kabisa hataki kuukosa hasilani....sasa nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazim,kila mtu anaona anaweza kunyoa...

Mkuu, unajua unaona pua ni vema kuwa nayo kwa kuwa kila mtu asiye mlemavu ana pua. Ikiwa leo hii dunia nzima itaamua kwamba ni sawa kutembea uchi, na peke yako ukaona ni vibaya kutembea uchi na ukavaa nguo, wewe ndio mwendawazimu.

Sasa ikiwa watu wote walioonyesha nia ya kugombea uraisi wewe unawaona ni wendawazimu, basi inawezekana kabisa wao hawana tatizo, bali mwenda wazimu ni yule anayewaona wao kuwa wendawazimu.
 
...huu uraisi umekuwa raisi sana kiasi kwamba unaweza kumchomo mgonjwa dripu za dawa na kumtoa wodini na kumpeleka ikulu aongoze nchi...wagojwa wanataka uraisi,wahuni wanataka uraisi,wazinzi wanataka uraisi,walarushwa wanataka uraisi na mafisadi ndio kabisa hataki kuukosa hasilani....sasa nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazim,kila mtu anaona anaweza kunyoa...
Naungana na wewe kwamba nchi imeongozwa hovyo hovyo mpaka watu kama akina mwandosya nao wanauota urais. Huyu waziri asiye na wizara maalum hana lolote na ana kiburi na nyodo sana. Yeye ndiye aliyeivuruga DAWASCO kwa maslahi yake binafsi. Alimwondoa CEO mchapakazi Bw. Kaaya kwa maslahi yake tu. Nasikia alipokuwa wizara ya maji alikuwa anafunguliwa hata mlango wa gari na msaidizi wake. Je, akiwa rais itakuwaje?? After all, ana nini cha kujivunia katika utumishi wake?! Ningekuwa mimi Kikwete, ningemtupilia mbali hata ukuu wa wilaya asingepata.
 
Unamfagilia Mwandosya kijanja.Huyu ni mccm na ccm hawatoweza kufagia
uchafu wao walioulundika kwa miaka zaidi ya hamsini. Upepo uvumao sasa hivi
ni upepo wa kuweka chama kingine madarakani. Tuwaache akina Makamba, Membe
Sita, Lowassa waendelee kulilia pipi!
Mbali ya kuwa ccm, generally, mwandosya hafai kuwa rais hata mkuu wa wilaya.
 
Naungana na wewe kwamba nchi imeongozwa hovyo hovyo mpaka watu kama akina mwandosya nao wanauota urais. Huyu waziri asiye na wizara maalum hana lolote na ana kiburi na nyodo sana. Yeye ndiye aliyeivuruga DAWASCO kwa maslahi yake binafsi. Alimwondoa CEO mchapakazi Bw. Kaaya kwa maslahi yake tu. Nasikia alipokuwa wizara ya maji alikuwa anafunguliwa hata mlango wa gari na msaidizi wake. Je, akiwa rais itakuwaje?? After all, ana nini cha kujivunia katika utumishi wake?! Ningekuwa mimi Kikwete, ningemtupilia mbali hata ukuu wa wilaya asingepata.

Mkuu, tatizo kubwa sana linalotukabili nchini ni kufanya uamuzi kutokana mambo ya kusikia. Sasa wewe umesikia tu kisha ukaamua Mwandosya sio kiongozi mzuri? Je unataka nikueleze niliyosikia kuhusu Lipumba, Mkapa, Zitto, Membe, James Mbatia nk?

Kuna Mwandishi wa Habari mmoja pale Nairobi aliwahi kumuuliza Nyerere "Nasikia unataka kuitawala Uganda". Nyerere alimuuliza wewe unaamini kila unachosikia? Na je ukisikia mimi ni baba yako, nilitembea na mama yako kukuzaa wewe, utaamini pia?

Sasa Mkuu, achana na mambo ya kusikia kisha ukakurupuka kukata shauri au kuchukua hatua. Utaja acha mke bure, maana nina uhakika kuna mengi unaweza sikia juu ya mkeo.
 
Mbali ya kuwa ccm, generally, mwandosya hafai kuwa rais hata mkuu wa wilaya.

Mwana saikolojia yeyote anaweza kukupa "profiling" nzuri sana ya aina ya mtu atakaechukua jina la Dumelambegu kwenye social forums. Sasa nadhani nikuache ufaidi uhuru wa kuchangia humu JF.
 
Mkuu, tatizo kubwa sana linalotukabili nchini ni kufanya uamuzi kutokana mambo ya kusikia. Sasa wewe umesikia tu kisha ukaamua Mwandosya sio kiongozi mzuri? Je unataka nikueleze niliyosikia kuhusu Lipumba, Mkapa, Zitto, Membe, James Mbatia nk?

Kuna Mwandishi wa Habari mmoja pale Nairobi aliwahi kumuuliza Nyerere "Nasikia unataka kuitawala Uganda". Nyerere alimuuliza wewe unaamini kila unachosikia? Na je ukisikia mimi ni baba yako, nilitembea na mama yako kukuzaa wewe, utaamini pia?

Sasa Mkuu, achana na mambo ya kusikia kisha ukakurupuka kukata shauri au kuchukua hatua. Utaja acha mke bure, maana nina uhakika kuna mengi unaweza sikia juu ya mkeo.

Unaweza kutueleza huyo wandosya kafanya nini hapa Tz,toka aanze utumishi wake kafanya nini au kasimamia jambo gani likapata ufanisi mkubwa? Acheni porojo bwana!
 
Back
Top Bottom