Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,630
- 25,586
Kwa kilotokea kabla, wakati na baada ya Uchaguzi mkuu wa raisi na wabnge nchini Tanzania, Tasnia ya habari imezidi kujikuta ikigubikwa na ujinga, ukosefu wa maadili, uhaini na kutokujielewa.
Zikiwa zimebakia wiki chache nchi yetu ishuhudie uhuru kamili wa miaka zaidi ya 60 ilopita, tasnia ya habari nchini nayo isiachwe iendelee kugubikwa na ujinga ilokithiri, iwajibishwe na ianze upya kuwajibika baada ya tarehe 9 Disemba 2025.
Ni majuzi tu kundi la waandishi wa habari nguli, akiwemo kiongozi wao na mwenyekiti wa baraza hewa la wahariri Balile, Absalom Kibanda, Ezekiel Kamwaga na wengine niliwasikiliza wakiongea baada ya kimya cha muda huo wote kabla, wakati na baada ya uchaguzi wakiwa ndani ya SGR wakielekea Dodoma kuendelea kufuata mkiani maigizo yanondelea kuhusu uchaguzi huo ambao kwa viwango vya kimataifa na kwa mujibu wa vyombo vyote vya kimataifa vikiwemo Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za SADC haukuwa wa uhuru na haki.
Nimewasikiliza waandishi hawa manguli wenye uzoefu na wanotegemewa kuondoka katika tasnia hii huko baadae na kushindwa au kuingiwa na uoga wa namna watavyoiacha tasnia hii muhimu katika mihimili ya uongozi wa taifa lolote lile kutokana na majukumu yake khasa kwenye kuhabarisha jamii jinsi wanavyosigina miiko (Ethics) na kuipoteza kabisa tasnia hivyo ya habari katika uso wa nchi kama Tanzania kwa kushindwa kabisa kuja na sababu za msingi za wao kukaa kimya katika kipindi hicho cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa tarehe 29 Octoba 2025.
Kwanza tukumbushane masuala makuu matano ambayo huibeba tasnia ya uandishi wa habari na kuiweka katika kiwango cha juu katika kuheshimiwa duniani kwa kuwa na uwezo wa kujenga hoja, kuhoji, kuelimisha na kuchunguza huku vyombo vingi vya habari vilivyomo ndani ya nchi na vile vilivyopo nje ya nchi.
Mambo hayo ni unyoofu au umakini wa habari yaani "Accuracy" kwamba habari inotolewa iwe na ubora yenye uhakika na iloonyooka.
Pili, ni uhuru yaani "Independence" kwamba habari iwe ni ukweli mtupu (fact) na iwe katika hali ya kutoingiliwa uhuru wake.
Tatu, kutoegemea upande wowote yaani "Impartiality" kwamba habari hiyo iwe haiegemei masuala ya upande mmoja tu yaani serikali ambayo haifuati misingi ya sheria na haki za binadamu na ikaacha upande wa pili ambao wadhulumiwa na kuwa hauna sauti inoweza kusikika.
Nne, uwajibikaji yaani "accountability" kwamba chombo cha habari au mwandishi awe katika hali na uwezo wa kujitambua kuwa awajibika au apaswa kuwajibia kutokana na uwezo wake wa kuwa mwandishi kuingiliwa kwa namna yoyote ile kwa minajili ya kumnyamazisha.
Na jambo la Tano, ubinadamu yaani "Humanity" kwamba uwezo wa kuwa na maamuzi ya kibinadamu au kwa kiingereza yasemwa " The quality if being humane rather than benevolence. Mwandishi au chombo cha habari kinakuwa chajiondoa (Disposition of benevolence) katika wajibu wa kupasha habari, kuelimisha jamii ambalo ni jambo la kibinadamu (Humane).
Sasa katika mambo haya matano makubwa kabisa katika kuweka ubora wa waandishi wa habari wa Tanzania wakiongozwa au kukulazimishwa kuongozwa na jukwaa la hovyo kabisa la wahariri wa habari na vyombo vyote ambavyo viekubali hali hiyo kumeondoa kabisa ubora wa thamani ya uandishi ambao ungetoa habari ambazo twaweza kuita ni "outstanding" yaani za hali ya juu.
Ni msingi mkuu wa mwandishi wa habari yoyote yule kutayarisha, na kutoa habari ambayo ina lengo la kutolalia upande wowote ule, jambo ambalo waandishi wa habari wa Tanzania ambao siku zote nimewalaumu kwa kufuata maneno wa waziri mkuu wa zamani mzee John Malecela kwamba ni waandishi ambao huandika uandishi wa kufuata hongo ya bahasha yaani "chequebook joournalism", maneno ambayo leo hii kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa terehe 29 Octoba 2025 tumeyashuhudia yakitokea.
Ukiondoa vyombo vichache sana khasa jukwaa letu tukufu la JF ambalo sasa limekuwa ni chanzo cha habari nyingi tu na vingine ambavyo wapo waandishi wake wengine wamekamatwa na polisi kwa kujaribu kuandika ukweli, vyombo vingine vyote vilobakia vimekuwa bubu mno.
Waandishi wa habari wa Tanzania wakiongozwa na jukwaa la wahariri TEF mwaka 2021 waliitwa kuzungumza na raisi Samia Suluhu Hassan alipokuwa akitimiza miaka 100 ya kukaa madarakani tangia aapishwe baada ya kifo cha mtangulizi wake John Magufuli. Katika mkutano huo TEF waliwasilisha tu madai yao ya muda mrefu kama ruzuku, ada ya usajili na kupata fursa ya kuwa na matangazo katika vyombo vyao.
Lakini hili ni la siku ingine nitapolishauri baraza hili la TEF kujindoa na utegemezi wa serikali katika kuendesha shughuli zake kwa kutegemea hizi bahasha ambazo leo hii bahasha hizi zimelifanya baraza hili la TEF kuwa bubu katika uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Octoba 2025.
Sasa kwanini ujinga umeigubika tasnia ya uandishi wa habari nchini Tanzania?
1. Baraza hili bado laitegemea serikali katika kujiendesha hivyo kusababisha kushindwa kuwajibika katika sehemu ya uwajibikaji kama nilivoeleza hapo juu yaani "accountability". Kila mtanzania ni shahidi wa kilichotokea tarehe 29 Octoba kwamba vyombo vy ahabari viliketi kimya na kushindwa kufuatilia na kuandika chochote au kuhabarisha kilokuwa kikitokea siku ile na aiku zilofuata yaani tarehe 30 Octoba hadi tarehe 4 Novemba.
2. Vyombo vyote vya habari nchini Tanzania kutoongelea chochote kuhusiana na uchaguzi wa tarehe 29 Octoba na pia kutotoa maoni yoyote kuhusiana na kukatwa kwa internet nchi nzima jambo lilowezesha polisi na vyombo vingine vyote vikiwemo vya mamluki kufanya mauaji ya halaiki nchini tangu nchi ipate uhuru. Kwa jambo hili vyombo vya habari vikiwemo TBC vimekiuka kanuni hii ya kutoegemea yaani "impartiality" kwa kurudi moja kwamoja kuendelea na matangazo baada ya internet kurudishwa na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo na kushindwa kutangaza mauaji yalokuwa yakiendelea katika sehemu mbalimbali nchini.
3. Kukosa ubinadamu yaani "Humanity" kwa maana kwamba kitendo cha waandishi wa habar wa Tanzania wakiongozwa na baraza lao la wahariri TEF kukaa kimya kabisa kwa siku zaidi ya 4 na kutoutaarifu umma wa watanzania wenzao na dunia juu ya kilokuwa kikiendeelea kwaonyesha watu hawa kukosa ubinadamu na kuwa ni watu wenye roho mbaya, ngumu, ukatili na kukosa ubinadamu kwamba uwamgaji mkubwa wa damu za watanzania wenzao haviwahusu.
Niwaambie waandishi wa habari wa Tanzania kwamba, mmewakosea sana watanzania na mmejiweka katika sehemu mbaya katika macho yao na macho na uso wa Dunia kwa kujiweka kuwa sehemu ya utawala dhalimu ambao hauzingatii utawala wa sheria na haki za binadamu, kwani mmekwenda kuhudhuria kuapishwa raisi ambae ameamuru vikosi vya usalama vifanye mauaji ya watanzania wenzenu kwa niaba yake. Pia moa Dodoma kwa kulipiwa marupurupu na malazi hivyo mmewasaliti watanzania wenzenu kwa kujiweka upande wa huo kwa kuendelea kuwa Dodoma kushuhudia kuapishwa kwa wabunge ambao ni wa chama kimoja kilojiweka madarakani kwa nguvu.
Mapendekezo- Nini cha kufanya baada ya ushuhuda huu wa ujinga huu mloufanya?.
1. Ombeni radhi wa watanzania kwa kutoa tamko rasmi kwamba mmekosea. Tumieni TBC, YouTube na vyombo vyote kufanya hivyo. Hilo litawaweka katika nafasi nzuri ya kuanza kupata dawa ya kiwatibu ujinga mlojivika kwa makusudi kwani mwatambua madhara ya uandishi wa kutumia bahasha.
2. Ufanyike uchunguzi au itolewe taarifa ya tahmini ya majukumu yenu ili kuondoa migongano kati yenu na waandishi au vyombo vingine khasa binafsi. Tathmini hii itatoa mwanga wa namna ya kutengeneza kanun mpya na miongoz ukiwemo mwongozo wa kujitafakari au kujiwajibusha pale inapotokea kuna kutokuwajika.
3. Mageuzi ya Usimamizi wa Jukwaa la wahariri.
Jukwaa hili livunjwe na kuundwa jukwaa shirikishi lenye sura mpya na sio akina Balile wala Kibanda and Co. Wapishwe waandishi wengine wapya kabisa na wenye weledi ambao wataibadilisha tasnia ya habari kuwa na heshima yake na sio kuonekana na tasnia ya waganga njaa.
Hii itatusaidia sana kuwa na waandishi wa habari chipukizi waso na madoa ya uchawa wala kupenda bahasha za uandishi wa habari.