Tasaf imewaibia madereva wake haki zao za mwaka huu wote:

Kimboko

Member
Nov 16, 2010
56
6
Nawasalimuni wanajamii wote mnisaidie hili jambo, maana mimi nimeshindwa kuelewa hawa madereva walioachishwa kazi kwenye kitengo cha IKULU kana kwamba ni kiofisi cha muhindi!

Kuna ndugu yangu mmoja alikuwa ameajiriwa na TASAF katika moja ya Mkoa hapa Tanzania; alikuwa amesainishwa mkataba wa miaka miwili yaani Jan, 2011 - Dec 2012. Cha ajabu hawa mabwana sijui kama kulikuwa na mabibi katika fani yao, wamesitishiwa mkataba huo mwezi Dec 2011 bila kulipwa haki zao kwa mujibu wa sheria ya ajira za mwaka 2004 na nyinginezo mnazozijua.

Sababu ya kusimamishwa ni kwamba eti magari yamechakaa yanatakiwa kuuzwa na yatakaponunuliwa mengine watafikiriwa kurudishwa kazini. Mliwahi kuona kauli kama hiyo tena ya mdomo siyo maandishi. Naweza kusema hawa jamaa walilogwa mchana!!

Taarifa walizonazo sasa na wanaanza kujipanga lolote liwezekanalo hiyo tasaf ife ili wote wakose ni kwamba wanahitajika Madereva 15 tu kwenye awamu ya III inayoandaliwa, yaani kwa sasa wamebaki 8 na kama wataongeza magari watachukuliwa 7 kukamilisha 15.

Wanaosubiri kurudishwa kazini ni zaidi ya 30 sasa je waungwana hii ni haki kweli kuua familia za watu wengi kama hawa ikiwa bado Mkurugenzi anakalia kiti cha ofisi kwa ubabe wa namna hii!!

Management ya tasaf yote naona imeoza maana sidhani kama walishirikishwa kuamua hili swala. Na huyo meneja rasilimali watu anaongoza akina nani kwa sasa maana rasilimali zake ni watu wakiwemo hao 30 waliopigwa teke bila kujali wamejiandaa namna gani ili hali walikuwa wana uhakika na mwaka wa kazi na hakukuwa na mtu yoyote aliyekuwa na wazo la kutafuta kazi.

Naomba kama kuna mtu yoyote wa World Bank anayesoma hii safu ya uongozi mbovu kwenye miradi yake, wachukue hatua kukataa uteuzi wa kipuuzi wa Mh Rais kuelekezwa na watu wa chini yake na inajulikana kabisa aliyemweka huyo mkurugenzi Ladisilausi Mwamanga hapo ni ndugu yake aliyeboronga kwenye issue ya Jairo mzee Luhanjo.

Ninaomba wanasheria na wanaharakati pamoja na wabunge wote watakaopata hii taarifa wachukue hatua maana vijana hawa wanahangaika huku na huko kutafuta pa kujishikiza lakini inashindikana ikizingatiwa Tume ya Ajira nayo iko hoi bin taabani, inatangaza kazi January mnakuja kuitwa usaili mwezi wa nane aibu kweli!!!

Nitawashukuru kwa watakaochukua hatua hasa wale wanaojua sheria za kazi kusaidi hawa vipofu wa akili zao kwa kuacha haki zao za msingi kwa mwaka mzima.

Asante.
 
Back
Top Bottom