TARURA wilaya ya Ubungo fanyeni utafiti

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,126
7,710
Jana tarehe 14/8/2022 Mhe. Rais amewaonya watendaji wa TARURA kutokutoa zabuni kwa wakandarasi wababaishaji.

Wananchi wa Wialaya ya Ubungo kata ya Kibamba eneo la Kikuvya gogoni/kituo cha polisi, tunaomba viongozi wa TARUARA wachunguze ujenzi wa barabara inayo anzia Kikuvya GOGONI kituo cha Polisi kuelekea maeneo ya kiluvya kwa komba, kimsingi Barabara hiyo ilipaswa ielekee maeneo ya Shule za sekondari hondogo lkn cha kushangaza barabara hiyo haikupita huko.

kuna umuhimu wa barabara hiyo kuelekea katika maeneo ya shule ili kurahisisha usafiri kwa wanafunzi wetu wanao taabika kutozwa nauli kubwa, lkn pia kuna shughuli nyingi za kiuchumi katika maeneo hayo, ulimaji wa mbogamboga n.k.

Tunaomba TARURA Ichunguze, tunaomba barabara hii ijengwe kulingana na mahitaji ya wananchi kuelekea kwenye maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom