TARURA kujenga barabara mpya maeneo korofi Dar es Salaam

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo kutoa agizo kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Dar es Salaam kutengeneza mashimo na viraka vyote kwenye barabara ndani ya jiji hilo.

Meneja wa TARURA mkoa wa Dar, Mhandisi Chacha Magori amesema hivi karibuni wataanza ukarabati wa barabara hizo sambamba na ujenzi wa barabara mpya kwenye mitaa mbalimbali wilaya ya Ilala.

Amesema mpango huo utazihusu barabara chakavu katika maeneo ya Kariakoo, Upanga Magharibi, Mchikichini na Ilala.
 
Waachane kabisa na habari za upanga wako vizuri wahamishie nguvu tabata kwa ujumla wake sie ndo wapiga kura bana, wale wahindi wa upanga hawapigi kura mjue
 
Back
Top Bottom