Tarime: Wananchi waendelea kuvamia Mgodi wa dhahabu usiku na mchana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili ya kuchunguza mchanga wa dhahabu wa Kampuni ya Madini ya Acacia, wananchi wa Tarime wamevamia mgodi wa North Mara kwa siku mbili mfululizo.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni mwendelezo wa kupinga uonevu unaofanywa na wawekezaji hao kupitia Kampuni ya Acacia.

Taarifa kutoka wilayani Tarime zinadai kuwa wananchi hao walivamia mgodi huo juzi saa 2.00 usiku na jana asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi hao walikwenda hadi kwenye mtambo wa kufua dhahabu na kufanya uharibifu huo kabla ya kudhibitiwa na jeshi la polisi.

Hata hivyo shuhuda huyo ambaye hakutaka kutaja jina , alisema vurugu hizo zimetokana na uongozi wa Kampuni ya Acacia kushindwa kuwalipa fidia wananchi waliokuwa na maeneo yao tangu awali.

Alisema wakati madini yalipogundulika, wananchi walioondolewa walitathiminiwa mali zao yakiwamo mashamba, nyumba na kuahidiwa kulipwa fidia akini hadi sasa hawajalipwa stahiki zao.

Alisema kwa siku mbili mfululizo wanachi wenye madai yao walifika katika ofisi za kampuni na kuona baadhi ya majina ya wanaotakiwa kulipwa fidia yakiwa yamebandikwa katika ubao wa matangazo lakini majina ya wengine yakiwa hayajabandikwa.
 
Wale ni wavamizi kwa mujibu wa ripoti iliyosomwa na kubarikiwa na mkuu, kuwa ni majizi acha wapimane ubavu na wananchi kila atakae pata apate polisi asisogee hapo kuwatawanya kabisaaaa maana wanachukua vyao vilivyoporwa.
 
Oooooh Baby nimekuweka moyoni usije niacha nikaumia moyoni
.."Nikaenda Daresalama nikawakuta wazungu,wanaongea kizungu nami nikaimba kizungu, Baby Give it to me "...
SAIDA KAROLI ON HER VERY BEST..

BACK TO THE TOPIC
Serikali izuie uhuni huu kwa gharama zote, Dawa ya mwizi sio kumuua bali ni kumshtaki..

Mkuu wa mkoa wa huko anashindwaje kuweka ulinzi mpaka pale utaratibu utakapofuatwa.?
 
.."Nikaenda Daresalama nikawakuta wazungu,wanaongea kizungu nami nikaimba kizungu, Baby Give it to me "...
SAIDA KAROLI ON HER VERY BEST..

BACK TO THE TOPIC
Serikali izuie uhuni huu kwa gharama zote, Dawa ya mwizi sio kumuua bali ni kumshtaki..

Mkuu wa mkoa wa huko anashindwaje kuweka ulinzi mpaka pale utaratibu utakapofuatwa.?
Acha wachukue ni Mali yao, wameibiwa sana, hata mwenyekiti wa ccm amethibitisha hili,

Tumeibiwa sana
Tumenyonywa sana
Tumedhaoilishwa sana

Acha wachukue ni Mali yao
 
Back
Top Bottom