Tarime waamka

Tarime waamka

Diwani Unga Ltd

Senior Member
Joined
Oct 12, 2013
Posts
149
Reaction score
70
Baada ya siku 4 tangu CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti mstaafu wa BAVICHA taifa ndg John Heche akiongozana na katibu wa kanda maalum ya Kinondoni HENRY KILEO kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya Jumamosi tarehe 18 Oct 2014 katika mji mdogo wa Sirari ulioko mpakani mwa Kenya kuwaelimisha wananchi kuhusu namna ya kushiriki katika ujenzi wa maabara wakitahadharisha Kiwango kikubwa cha michango kinachotozwa na serikali ya kata kati ya tsh 100000-67000 kwa kaya kuwa sio sahihi kwani mgodi wa North Mara ulitoa tsh 1.9 b kwa ajili ya kusimamia mapungufu ya maabara hizo.

Kwa mapokeo hayo yaliyoichanganya CCM Yamesababisha diwani wa kata ya Sirari AMOS SAGARA kutaka kujibu mapigo kwa kuilinda serikali isinangwe naye akaitisha mkutano akijaribu kupinga hoja hizo
Yaliyotokea ni kuambulia zomeazomea ya hali ya juu.
 
sasa huko ndiyo kuamka,upuuzi mtupu.
 
safi sana chadema kwa kuelimisha wananchi.

Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.
 
Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.

Wananchi wa sasa si wale wa Kidumu tena Wameshajitambua, tukutane kwenye Serekali za Mita ndio utajua nguvu ya umma imekata Kidumu
 
huyu diwani wa kata hiyo na ulofa wake alijua anaweza kuwajibu CHADEMA? tena viongozi na vijana machachari kama HECHE na KILEO
yaani diwani uwajibu
WABUNGE wawili
mwanga
na Tarime?
aisee akajipange upya
zomea zomea!
tuletee video mura
 
wanatarime sio mbumbu huyu diwani alizana ataweza kuwaxhawishi amuulize mtikila alie fika tarime na kuanza kuonge na kuchonganisha alichoambulia ni mawe kichwani kule watu ni waelewa sana na ccm wajipange mwaka huu mpaka mwakani tunatka kunyakuwa viti vyote
 
Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.

Mkuu unazungumzia Kigoma ipi,ya Zitto,Kafulila,Serukamba,Obama,Machali au Mkosamali?.Mana kigoma mjini tangu uchaguzi umeisha mbunge wetu Serukamba alikuja Mala moja hajaludi tena,tunamsubiri tena bado kidogo
 
Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.

Kama kodi zetu zinatafunwa, wananchi wakichangia hela zao ndizo hazitatafunwa? Hebu jiulize tangu nikiwa mtoto nasikia wanafunzi wananchia madawati kila mwaka na mpaka muda huu baadhi ya shule bado wanafunzi wanakaa chini hata baada ya kuchangia hayo madawati, je haya ndiyo maendeleo unayoyasema? Tunataka serikali iwe na watumishi/watendaji waadilifu, wenye uwazi na wanaowajibika kwa wananchi. Na siyo kuendeleza utamaduni wa kuwafisadi wananchi kwa kisingizio cha maendeleo. Serikali haikusanyi kodi na badala yake inawafisadi wananchi. Angalia huduma za usafiri: gari limeandikwa (mfano) abiria 65, linajaza hadi abiria 110 na zaidi, lakini kodi inayolipwa ni ya abiria 65 tu au pungufu yake na hii yote ni kuwafanya wafanyabiashara waendelee kukipigia kura chama tawala kwa kuwabeba. Kuna maeneo mengi pia ambayo serikali ingeweza kukusanya kodi ya kutosha na badala yake inawabebesha wananchi mzigo mkubwa wa michango isiyo isha wakati huduma za jamii zinaendeleza kudolola - elimu, afya, usafiri nk.
 
Chadema Tarime hawafiki hata watu 20. Tangu wamfukuze Mwenyekiti wa Chadema mkoa na diwani wa Nyamongo hali yao imekuwa mbaya sana, pamoja na hayo Mzimu wa Chacha Wangwe umeshawapiga kofi la shavu.
 
Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.

mgodi wa north mara mine umetoa bil 1.9 kwa kazi hiyo wananchi hawa hawana uwezo ndio maana serikali ilianzisha mradi wa TASAF 3 kwa ajili ya kuwakomboa kiuchumi8000 kwa mwezi
 
Akili za kutazamia hizo ungeona wenzako kigoma wanavyohamasishana kuchangia maendeleo eti nyie mnakwamisha kileo mwenye gaidi kazi yake kumwagia watu sumu atajua maana ya maendeleo.

Kama kila kitu kuchangia,kazi ya kodi ni nini? Haiwezekani kodi zetu ziendelee kunufaisha mafisadi na makuwadi wao huku watz maskini wanakamuliwa michango ya kila aina! Ccm lazima tuisulubu kwenye hizi chaguzi
 
baada ya siku 4 tangu chadema kupitia kwa mwenyekiti mstaafu wa bavicha taifa ndg john heche akiongozana na katibu wa kanda maalum ya kinondoni henry kileo kufanya mkutano mkubwa wa hadhara siku ya jumamosi tarehe 18 oct 2014 katika mji mdogo wa sirari ulioko mpakani mwa kenya kuwaelimisha wananchi kuhusu namna ya kushiriki katika ujenzi wa maabara wakitahadharisha kiwango kikubwa cha michango kinachotozwa na serikali ya kata kati ya tsh 100000-67000 kwa kaya kuwa sio sahihi kwani mgodi wa north mara ulitoa tsh 1.9 b kwa ajili ya kusimamia mapungufu ya maabara hizo.

Kwa mapokeo hayo yaliyoichanganya ccm yamesababisha diwani wa kata ya sirari amos sagara kutaka kujibu mapigo kwa kuilinda serikali isinangwe naye akaitisha mkutano akijaribu kupinga hoja hizo
yaliyotokea ni kuambulia zomeazomea ya hali ya juu.

fungua video zipo mbili

shuhudia zomeazomea ya mwkt wa hal ya wilaya tarime
 
tayari kuna file limeandikwa Video.zip
zipo crpi mbili aise
 
huyu diwani wa kata hiyo na ulofa wake alijua anaweza kuwajibu CHADEMA? tena viongozi na vijana machachari kama HECHE na KILEO
yaani diwani uwajibu
WABUNGE wawili
mwanga
na Tarime?
aisee akajipange upya
zomea zomea!
tuletee video mura

Hivi kumbe kileo ni naye ni mbunge?
 
Back
Top Bottom