TARIME: Mchungaji wa kanisa afariki dunia akimwombea marehemu

TARIME: Mchungaji wa kanisa afariki dunia akimwombea marehemu

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
26,597
Reaction score
29,531
Mchungaji wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) la Sirari, tarafa ya Inchugu wilayani Tarime mkoani Mara, Nestory Papaa amefariki dunia wakati akimwombea marehemu katika mji wa Kehancha nchini Kenya.

Taarifa za kuaminika zimesema mchungaji huyo alikwenda katika mji huo na rafiki zake ili kuhani msiba wa shemeji wa rafiki yake.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa maziko ya mchungaji huyo, Diwani wa Kata ya Sirari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpakani, Nyangoko Paulo, amesema mchungaji huyo alifikwa na umauti baada ya kuanguka ghafla wakati akimuombea marehemu huyo.

Ndugu wa Mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina Charles Papaa alisema kaka yake aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la EAGT lililopo katika mji wa Sirari na pia mfanyabiashara wa duka la kuuza vipodozi alikufa katikati ya maombezi aliyokuwa akiyafanya.

Mnamo Jumatano iliyopita, kaka na marafiki zake akiwemo Nyangoko Roman walikwenda kuhani msiba wa shemeji yake na Nyangoko huko Kehancha, Kenya.

Wakati akitoa neno ghafla aliishiwa nguvu na kuanguka chini ambapo watu waliokuwa msibani hapo na marafiki zake walijitahidi kumkimbiza katika hospitali ya jirani ya Migori ili kumpatia matibabu, lakini alipoteza maisha kabla ya kupatiwa matibabu,” amesema Charles.

Alisema wakati wa uhai wake Mchungaji Papaa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na taarifa ya madaktari katika hospitali alikokimbizwa baada ya kuanguka zinaeleza kuwa kifo chake kimesababishwa na mshituko wa moyo.

Alisema Mchungaji huyo alizikwa Jumamosi katika Kitongoji cha Buriba kata hiyo ya Sirari.

Katika tukio lingine, mkazi wa Kitongoji cha Nyamorege kata hiyo ya Sirari ambaye ni mwendesha bodaboda, Sinda Gichengwe maarufu kwa jina la Mtandao amekufa baada ya kuchomwa kisu mgongoni.

Sinda anadaiwa kuchomwa kisu na mtu aliyefahamika kwa jina moja la Samweli mwenyeji wa Mugumu, Serenngeti usiku wa kuamkia Oktoba 7, mwaka huu. Tukio hilo lilitokea katika Baa ya Migombani wakati wawili hao wakigombea mwanamke.

Imedaiwa kuwa baada ya kufanya kitendo hicho mtuhumiwa alitoroka. Kamanda wa Poliisi Kanda Maalumu ya Tarime /Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi linamsaka mtuhumiwa huyo ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Screenshot_2018-10-09-15-35-09.jpeg
 
Maelezo ya Kichwa cha habari hayafanani na kilichoandikwa ndani ya habari yenyewe. Wasoma vichwa vya mabandiko wataishia kuchagia wakidhani mchungaji alikuwa anafanya maombi ya kumfufua marehemu!
 
Kiimani tunamuombea angalau huko anakokwenda akawe salama.

Hata wewe siku ukifa Ndugu zako wataita Kiongozi wa dini akuombee.
na bila kuwa na hela ya kutosha marehemu haombewi...
duuh hizi trick zinawanyonya watu sana
 
marehemu anaombewa ili iweje!
watakiwa kupewa faraja ni ndugu na majamaa tu ...
Ama kweli Kweli itawaweka huru
Nipe mstari unaokataza kuombea marehemu. Unajua toharani wewe? Kwa taarifa yako ukifa huku ukiwa na dhambi ndogo ndogo bila kupata fursa ya kutubu hutaenda mbinguni moja kwa moja bali utapitia toharani kwaajili ya "kusafishwa" ni kama kwa moto ili ustahili kwenda peponi. refer andiko hili "15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto."
1 Wakorintho 3 :15

Ukitaka kujua kama kuna fursa ya msamaha baada ya kifo soma neno hili la Yesu juu ya msamaha katika ulimwengu ujao, "32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao."
Mathayo 12 :32

Ukiijua kweli raha sana. Laiti mngejua pengine yupo ndugu yako anateseka toharani na maombi/toba yako ingemtoa mngewaombea. Marehemu walio toharani wapo kwenye malipizi ya dhambi zao ndogo ndogo ambazo hawakupata fursa ya kutubu na haziwezi kumfanya aende motoni. Mbinguni wanaingia watakatifu tu wasio na doa.

Someni hayo maandiko kabla hamjaanza ubishi ubishi wa kukariri mistari.
 
huo ni upotoshaji mtupu hakuna kitu kama hicho...
unadanganywa na wewe unadanganya
 
Marehemu toka lini akaombewa?

Ndio yaleyale ya TUMSWALIE mtume
Kinachoombewa ni Roho ya marehemu na sio mwili uliokufa....

Mhubiri 12:7
Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
 
Back
Top Bottom