Tarehe ipi huangaliwa unapotuma maombi ya kazi?

Mlalahoi Mlalahai

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
399
146
Nataka kujua wadau hivi mtu unapotuma maombi ya kazi mfano deadline ni tarehe 30 April, wewe ukatuma maombi yako tarehe 28 au 30 hiyo hiyo je kitakachoangaliwa ni tarehe ambayo ulituma barua pale Posta au tarehe ambayo kampuni italipokea hilo ombi mfano ulituma tarehe 30 ambayo ndio deadline lakini barua ikaifikia kampuni tarehe 6 May je watakuchukulia kama ombi limechelewa au wataangalia kwamba uliomba kabla muda haujaisha? Msaada tafadhali
 
Posta ambayo wao wataenda kuchukua
Okay, sawa ila nakumbuka wakati nafanya maombi ya mkopo nilituma siku ya mwisho kabisa ya kutuma maombi, na mimi nilituma nikiwa mkoani ambako ni mbali, sasa katika hali ya kawaida Bodi isingeweza kuyapokea yale maombi siku ile ile, inamaana waliyapokea siku mbili au tatu mbele, hii imekaaje ikiwa nilifanikiwa yaani nikimaanisha barua iliwafikia Jamaa?
 
Wafanyakazi wa Posta na wa bodi nao ni binadamu tena inaonekana wenye uweledi na uelewa wa kazi yao ndo mana wakaelewa na kupokea barua yako...ni jambo la kushukuru maana ila usiwe unasubiri karibu sana na deadline....na inawezekana ulitumia EMS ambayo ni fast zaidi ndo mana ilifika on time
 
Back
Top Bottom