Tarehe 29 ilikukuta wapi na ulikuwa wapi?

Mimi usiku wa kuamkia tarehe 29, nililala gest moja iko karibu na hospital ya Msewe.Asubuhi yake ya tarehe 29, mida ya saa tatu hivi nikaenda kunywa supu na mchepuko wangu pale Kona.Aisee nikaona watu wanapita wengi mno ikabidi namimi nielekee barabarani.Kucheki pale stand ya mwendokasi kibo kuna gari ya mwendokasi imepaki na kuna gari la maji ya kuwasha la polisi upande wa pili kimepaki.Ghafla watu walitokea upande wa pili wa stand wakalimwagia mafuta gari wakatia moto.Lile gari la maji ya kuwasha likaanza kuwamwagia watu maji lakini wapi.Watu wakaanza kupanga mawe na yale maplastick ya nayopangwa pembezoni mwa barabara sahzi wakari barabara inajengwa.Pamoja na kumwagiwa maji yakuwasha watu waliendelea kupanga na kurusha mawe kwenye stand ya mwendokasi.Punde si punde ndipo yakatokea magari matatu ya polisi kutokea kimara huko, yalikuja huku yanamimina risasi na mabomu ya machozi kutawanya watu. Hapo ndo mshikemshike ulipoanzi.
 
Mi nilikuwa Ubungo Maziwa saa nne kasoro nikavuka fresh kale kadaraja ka watembea kwa miguu kuingia EALC ,Ile nafika yard ya mwendokasi chuma zinalia nyuma ilibidi nilaze mshale mpaka Emmaus Center kituo Cha Wakarismatiki Wakatoliki nikajisemea bora waniulie kanisani.
Nimekaa hapo mpaka saa kumi na Moja anga limetulia njia zote zimefungwa .

Ninaamini watu wengi wemeuwawa wakati wakitafuta namna ya kurudi nyumbani kutoka mafichoni.
 
😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴
 

Ni kweli mkuu, Kwenye kundi la watu ulikua unakua safe, Ila ukiwa peke ako ndo kinaumana
 
Yaani ndo hivo mkuu kuna watu walitoka hata kupiga Kura yaani
 
Kwa jicho la mwewe naona maadhimisho/sherehe za 9december zikiota mbawa.
Huwezi arika jumuia za kimataifa sebleni kwako afu vi junior visimame kwa mlango wa chumbani vi funue Pazia muda wote.Atakae aibika zaidi ni mwenye nyumbani.
Haidhuru tutasherehekea mwaka wa mbele.
 
Nilikuwa home family,hakuna aliyeenda kupiga kura na tulishakula kiapo hakuna m TU u kupiga kura,

Tarehe 29 iliisha poa huku kwetu,,,kiliumana tarehe 30,ta

Tarehe 30,kumekucha vizuri amani tele,raia wanasema hakuna baya mishe zikaendelea,,,,mida ya saa 10 nipo zangu nimelala nasikia nje mageti yanabamizwa watu wanafungwa maduka,,, nikitoka nje kumbe Gen z washawasha moto wa matahiri barabarani hakuna mtu kupita,, nikatoka nje kushangaa hiiiii,watu wamejaa barabarani kibao na kushangaa kinachoendelea mjini milio ya risasi na makelele.
 
Ni kweli mkuu, Kwenye kundi la watu ulikua unakua safe, Ila ukiwa peke ako ndo kinaumana
Ni kweli aisee mi niko nahojiwa na wajeshi likapita gari la Polisi lile pick up wamefura balaa nikasema hapa ningekutwa mwenyewe ningebebwa.
Hapo Sina habari kama wanapiga risasi kavu kavu muda huo mitandao washazima.
 
Sikua Kwenye maandamano ila kuna mtoto mmoja hivi aliniita baba nisaidie, kabla sijafanikisha lengo la kumuokoa wakaniwahi wao😢😢😢 Imagine a child between 13-17yrs unamfumua kichwa bila huruma.

Hii kitu sitokuja kuisahau kwa kweli.
 
Tarehe 29, me nliamua kubaki ndani kama taadhari incase maandamo yatatokea, mpaka saa saba mchana huku mtaani kwetu palikua shwari kabisa hapakua na dalili za maandamano, nkaamua nimuite demu mmoja aje kunipa kampani home, alikuja fresh... ilivofika mida ya saa tisa tukaanza kuskia milio ya risasi huko nje, kumbe tayar palishaanza kuchangamka, plan ilikua mtoto wa watu arudi kwao by saa 12 jioni lakini kwa hali ilivyokua hatari ikabidi alale tuu home,
Kesho yake tarehe 30 ndo alirudi kwao, nashukuru Mungu alifika salama
 
Ulifanikiwa vipi kurudi nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…