Tarehe 29 ilikukuta wapi na ulikuwa wapi?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,127
Reaction score
24,429
Leo tupeane ushuhuda wa Tarehe 29 ilikukuta wapi, ilikuaje ulivyoshtuka watu wapo barabarani?Na jee kuna story gani za watu waliouliwa uliziskia ukashtuka au zilizokuhuzunisha?Kipi kilikushangaza?Leo tupeane habari kuhusu tarehe 29

Nianze na mimi binafsi kabla ya tarehe 29 na marafiki zangu wanne tulipanga tutatoka kuandamana....Nakumbuka tulifanya kikao jumamosi ya tarehe 25 tukiwa watano tukijadili mambo ya nchi na jinsi tulivyojiandaa kuandamana

Tupo watu watano ambao tunaaminiana sana na tunashirikishana katika mambo nyeti kama haya.Kwa hali ilivyokua social media zilivyokua za moto tulijua kabisa tarehe 29 uhakika wa kutoka ni mkubwa.

Twende mbele kufupisha mambo,tarehe 28 tulikutana tena tukipiga story kuhusu tumejiandaa vipi nakumbuka jamaa yangu mmoja.alisema what if watu hawatotoka?Nikajisemea liwalo na liwe.

Usiku wa kuamkia tarehe 29 nakumbuka tulikua macho mtandaoni mpaka saa 7 usiku, nikaenda kulala nikiwa na shauku kubwa sana.

TAREHE 29 ASUBUHI...
Tuliamshana tutoke mapema saa 11 ila rafiki yangu akanambia tutoke saa 12 muda wa maandamano kuanza.Niliswali nikamuomba Mungu sana na wife alikua siku zote hataki nikaandamane akihofia nitauwawa japo haipendi serikali ya Samia wala ccm lakini alikua ananisihi nisiamandane, lakini nilimweleza ukweli wote kuwa ishu ya kuandamana inaanza na kila mmoja nikisema sitoki na yule akisema hatoki jee ni nani atatoka?

Kusubiriana tulijikuta tukikutana Goba tulikua jumla wanne tu pamoja na mimi yule mmoja tuliona anatuchelewesha

SAFARI IKAANZA
Tulitoka Goba kiukweli palikua hamna hata dalili ya maandamano, tukaenda hadi mbezi mwisho napo hakukua na dalili za maandamano, yule jamaa yetu ambaye alichelewa kutoka alitufata hadi mbezi mwisho kwa boda boda.Tulikaa mpaka saa tatu na robo hamna dalili ya maandamano kabisa kiasi kwamba tukaanza kukata tamaa na kilichoudhi ni kufungua mitandaoni na kuona barabara zote ni nyeupe na hakuna dalili za maandamano yoyote yale.

Tulikaa mahali hapo mbezi tukaanza kuulizana sasa itakuaje?Kiukweli nilijikatia tamaa na nilikua na hasira balaa nikasema why watanzania tumekua waoga kiasi hichi, tulikaa mbezi mpaka tukawaza turudi tu majumbani mwetu hapo nilikua na hasira balaa nikasema nikifika home siongei na mtu yoyote zaidi nitalala tu.

Nilikua nishakata tamaa kabisa, tukaona tuingie mgahawani tunywe tu chai maana tangu tulipotoka tulikua hatujala chochote.

MAANDAMANO YAKAANZA RASMI
Tumemaliza kunywa chai tunaanza kurudi zetu Goba ile tunavuka njia panda ya Goba ndo naona mtandaoni watu wameanza kujikusanya ubungo Kibo, Aisee hatukua na jinsi kwa haraka tulichukua pikipiki kila mmoja hadi Kibo, nilishuhudia watu kwa mamia wakielekea Kibo wakisogelea eneo ya Kibo nyomi za mbezi kimara zote zilielelekea Kibo!!
ITAENDELEA
 
Ilinikuta geita hakukua na dalili yoyote ya maandamano rkn ilipofika saa8 tulipata taarifa huko kwa majirani zetu katoro yakua kimenuka sisi mda huo tunafanya biashara kama kawa amani ya kutosha

ilipofika saa kumi kama na nusu tukasikia et mitaa ya nyakumbu geita kimenuka mimi hata sikushituka kwasababu nilijua amani ipo baada ya nusu saa niliona kwa kasi watu wanakimbia wengne wanafunga maduka chapu, naami nikaanza kurusharusha bidhaa zilizokua nnje kwa kasi ile namaliza tu mabomu ya machozi

sija kaa sawa ile njia ya kwenda home kila nnapokimbilia polisi wapo nikajikuta nipo kati kati lile eneo nililokuepo na tulikua wengi ili ukatishe barabara ni kujitoa mhanga mda huo tumejibana kwenye mjumba ya watu vichochoroni na maafsa nao wengine wanashuka kwenye gari kutoka kwenye njia kuu lami kuja vichochoroni ALOOOOOH nilijua nakufa kilichosaidia kalikuja kamvua ka kasi kidogo ndipo nikakatisha barabara na kundi jingne lilinifata pale kati ya barabara tunakimbia alikuepo jamaa kapigwa risasi ya kifuani anatuita tumusaidie

yaani dah jamaa ameshakatalia machoni pangu jamaa bonge hivi sijui alipona Amani ni nzuri tusiombee maandamano isingekua mvua mimi ningekua nmekufa

EXALIOTH

JF--GEITA
 
Maswali ya ki-spy
 
Aiseee
 
Niliamka safi na kwenda kwenye mishe zangu, kufika saa 6 nilikua njiani nageuza mahome, nilishangaa tu barabarani vituo vya kupigia kura vikiwa havina mtu sikujipa mawazo nilijua wameenda kupata chakula au kuzimua kabia si unajua tena kazi na dawa

Nimefika home nikauchapa kwanza usingizi ili baadae mida ya kama 9 au 10 nitoke nikaandamane, natoka nakutana na jirani ananiambia mbona kimeumana muda tu ndo nikaanza kupata picha kumbe ule weupe wa vituo vya kupigia kura ulikuwa na sababu

Nilipitwa na mambo mengi kizembe sana nikashindwa kumtwanga vitasa hata polisi mmoja tu na mimi niambulie vurugu angalau
 
maandamano sio fujo bali serikali na vyombo vya ulinzi wanavunja katiba kwa kufanya fujo ili watu wasiandamane
 
Pole sana ulivyosema kazi ya Dhulma nimeelewa ila huwezi amini asilimia kubwa ya waliotoka kuandamana ni makarani na wasimamizi wa huo huo uchaguzi baada ya kukimbia vituoni walibadili nguo na kuingia barabarani kukomboa nchi
 
Hahaha au ulikua ushapiga vyombo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…