Baada ya uchaguzi kulikuwa na vigelegele vingi sana. Tulisikia watu wakisema Nyerere amerudi, wengine wakasema huyu ni zaidi ya Nyerere! Kila gazeti lazima litafute headline yake ili liuze. Wengine wakasema kwa kasi yake ataua upinzani. Wakosoaji tukasubiri mwangwi wa vigelegele utulie tuwarudishe watu kwenye mstari.
Hivi karibuni tukasikia sauti za ukosoaji zikianza kusikika, kuanzia Lugumi, utumbuaji majipu, bunge kufunikwa na blanketi la serikali, sukari nk. Watanzania wakarudi kwenye asili yao, kulalamika, kukosoa kama siyo yote hayo basi kunung'unika.
Hatuwezi kupuuza kelele za 'dikteta' hata kama zitakuwa chache, zimeanza. Magazeti yameanza kumpa kisogo mpaka wanaanza kulalamika Chadema inanunua wahariri! Siyo kweli, watanzania wanarudisha matumaini kwa chama TUMAINI lao.