Kuna Ndoa za aina tatu zinazotambulika na serikali
1) Ya Kidini
2) Ya kimila
3) ya Kiserikali
Maana ya serikali kuzitambua hizi ndoa ni kukubaliana na taratibu na imani ya hizo ndoa, Kila imani inaelekeza namna ya kugawa ama sababu zinazokubalika katika kuvunja ndoa
pamoJa na serikali kuzitambua hizo aina za ndoa lakini, bado serikali/Mahakama inaonekana ina nguvu zaidi ya hizo jamii zilizokubaliwa kufungisha ndoa halali, maana ya kusema hivyo ni kuwa mara nyingi tumeona mahakama zinaingilia maamuzi ya Dini husika kuhusiana na mambo ya Talaka na pia mirathi
kwa kesi yako ni ngumu kidogo kuieleza kwa maana umeeleza mambo mengi, na inaonekana umejitahidi kutafuta talaka na imeshindikana sasa unajaribu kutafuta visa ambavyo havina nguvu wala ushahidi kisheria, Kesi ya kusema umebakwa ni ngumu sana kwa mume na mKe japo sheria hipo, lakini ushahidi huwa ni wa shida sana kuthibitika \
Jaribu kuwaona watu wa sheria wakusaidie kufungua madai ya talaka bila kuweka hizo sababu za kubakwa ama nini