Taraka Mahakamani

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Apr 18, 2009
1,195
232
  1. Kwa wajuzi wa sheria. Je mtu kama alifunga ndoa kanisani na ikatokea wakakorofishana na mwana ndoa mwenzie (mfano mwanaume anampiga mke wake na kutishia kuuza mali zote na kutoweka) na wameishi kwa zaidi ya miaka 20. Je Mwanamke anaweza kwenda mahakamani kudai taraka ili wagawane vilivyopo au mpaka church tu?
  2. Na je sheria zetu zinasemaje juu ya tendo la wanandoa. Ikitokea mwanaume kamlazimisha mke tendo la ndoa na mwanamke akawa hata, hivyo ikapelekea mwanaume kumpiga mkewe au kumbaka, je mwanamke anaweza kwenda mahakamani kumshitaki mume kwa ubakaji?

Naomba muongozo!
 
Mkuu omba MoDs wakubadilidhie heading yako ni Talaka na siyo Taraka.

Mengine mimi siyo mjuzi sana watakuja kukusaidia.
 
.1 Mahakama peke yake ndiyo yenye uwezo wa kutoa talaka na kugawa mali siyo kanisa 2. Kwenye masuala ya kujamiana suala la makubaliano ni muhimu sana kama hakuna makubaliaö ni kubaka hata awe mkeo makubaliano ni suala muhimu.
 
Kuna Ndoa za aina tatu zinazotambulika na serikali
1) Ya Kidini
2) Ya kimila
3) ya Kiserikali

Maana ya serikali kuzitambua hizi ndoa ni kukubaliana na taratibu na imani ya hizo ndoa, Kila imani inaelekeza namna ya kugawa ama sababu zinazokubalika katika kuvunja ndoa

pamoJa na serikali kuzitambua hizo aina za ndoa lakini, bado serikali/Mahakama inaonekana ina nguvu zaidi ya hizo jamii zilizokubaliwa kufungisha ndoa halali, maana ya kusema hivyo ni kuwa mara nyingi tumeona mahakama zinaingilia maamuzi ya Dini husika kuhusiana na mambo ya Talaka na pia mirathi


kwa kesi yako ni ngumu kidogo kuieleza kwa maana umeeleza mambo mengi, na inaonekana umejitahidi kutafuta talaka na imeshindikana sasa unajaribu kutafuta visa ambavyo havina nguvu wala ushahidi kisheria, Kesi ya kusema umebakwa ni ngumu sana kwa mume na mKe japo sheria hipo, lakini ushahidi huwa ni wa shida sana kuthibitika \

Jaribu kuwaona watu wa sheria wakusaidie kufungua madai ya talaka bila kuweka hizo sababu za kubakwa ama nini
 
Ndoa zote huvunjwa Mahakamani.Kwa mujibu wa sheria za nchi hii na za kanisa,mume hambaki mkewe...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom