kamanyani
Member
- Jan 2, 2015
- 65
- 110
Aliandika ujumbe nanukuu"habariza huko ndugu pole na majukumu. Uongozi wa shule tunapenda kukujulisha amepata na tatizo la homa ya ghafla hapa shuleni na sasa tupo nae hospitali anapatiwa huruma ya matibabu, tunakuomba ufike mapema, Mimi mwalimu.
Lengo: hapa lengo ni kujipatia fedha Kwa utapeli.
Ukitazama huu ujumbe ni wakipuuzi na utapeli wa kijinga, kwasababu hajajitambulisha yeye ni mwalimu Nani, wa shule hipi na mwanangu anaitwa Nani na anasoma wapi. Ila Kwa mzazi yeyote akipokea taarifa kama hii lazima atapaniki na kushindwa kutafakari Kwa kina kuhusu taarifa husika.
Nilichokifanya nilimpigia simu nikamuhoji, wewe ni mwalimu Nani, na wa shule gani? Na mwanangu unayemsema anaitwa Nani na anasoma darasa gani na shule gani? Alishindwa kujibu hayo maswali na kuishia kujifanya anisikii vizuri.
Angalizo: wazazi/walezi mkipokea ujumbe wa staili hizi tuliza akili, na muhoji muhusika Kwa ufasaha. Natambua taarifa hii inastua kama Una mtoto na pengine kweli yupo shule anasoma. Na tujitahidi kuwa na namba za simu za uongozi wa shule ili kuthibitisha taarifa zozote tunazopokea Kwa njia ya simu zinazohusu watoto wetu pindi wapo mashuleni.