Tapeli huyu akamatwe.


Umenikumbusha tukio lililowaikunitokea mimi pia, ilikuwa jumamosi usiku kama saa 2 pale CRDB Tower branch (PPF TOWER) Nikitoa pesa ATM, wakati natoka nje nikakutana na mzungu mmoja

Akaniuliza "pls can u speek english!" nikamjibu poa... basi akaanza kunielezea kuwa kadi yake imezama kwenye ATM hile ni VISA ya nchi yake, so mpaka j5 ndio atapata huduma kwani (j2, Na j3 na j4 ilikuwa sikukuu ya iddi) so angeteseka sana na anaishi kariakoo hotelin akaniomba nimsaidie pesa ya kuishi siku hizo zote mpaka j5 na akanieleza vitu vingi n.k

Kwa huruma kabisa akaniomba atanirudishia mara mbili yanitakayompatia, basi nikaona siku zote zile nikampatia 100,000 nzima, akanipa namba yake ya simu basi nikaona maisha tayali tena mzungu....

Basi siku ya iddi nikaona nimtafute tushiriki naye, nikawa kigamboni naye vizuri kabisa tena kwa pesa yangu, wee ilivyofika jumatano nikipiga simu inaita weeeeeeeeeeeeeeeeeee mpaka, ijumaa akanipokea nakuniambia yupo mbali anakuja nilipo, yani mpaka leo simu inaita tuuuuuuuuuuuuuuuu, basi nimeamua kuacha tuuu

Kweli ni fundisho kubwa sana, sio kila msaadie anania nzuri na wewe ni bora kumpatia tu kuliko kukuazima.

Sio wabongo tu matapeli, mpaka wazungu ndani ya Tz.
 
Ila wahusika wenyewe ndo wamejitapeli hapo:
unawezaje kutapeliwa kirahisi namna hii!

Ndugu yangu kuna kitu kinaitwa dhamiri iliyomo ndani ya moyo wako, zimetofautiana na ya mtu mwingine siyo kwamba alitapeliwa kirahisi
 
kweli mjini shule. wasipokupiga finga watakupiga kwa maneno matamu.
 
Nilichogundua sisi watanzania ni wakarim saaana aseeee, napata mawzo kuwa kumbe inawezekana taifa likatumia fursa kuwachangisha raia ili kuleta maendeleo, maana mimi cjaona utapeli
Ila n ukarim, aseeeee!
 
we unapajua anapopaongelea au!!!
 

Wazungu nao njaa kali hapa mjini siku hizi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…