Tanzia

R.i.p m4c on the way

Amani na upendo tuliokuwa nao unaanza kumong'onyoka taraatiiibu manake siku hizi ukisikia msiba wa kiongozi awaye yote basi hata kabla hajazikwa unasikia siasa zinaingia.

Wana jamvi vipi wale madiwani wa LIndi tulioambiwa kwamba wameitwa mbele za haki baada ya kuwa wamegawa sanda misikitini wakati M4C ikiwa Lindi? Sijasikia tena habari zao.
 
Poleni wafiwa wote na watanzania kwa ujumla poleni sana
 
Diwani wa kata ya Manchira (CCM) na ambaye pia likuwa makamu mweyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti amefariki dunia,
Mungu awafariji wafiwa na wanaManchira kwa ujumla!
Rest in Peace brother Mechama

R.I.P. diwani Mungu amekupenda zaidi yetu
 
Hii habari kweli ilistahili kuwa katika ukurasa huu?
 
Ni kweli, kwa upande mmoja tunasema pole maana hakuna anayependa kufa. Hata hao mafisadi tusingependa waondoke kwa kufa bali tuwaondoe madarakani wakiwa hai. Mwombee adui yako aishi siku nyingi ili unapobarikiwa ajionee mwenyewe.

Ni kweli tunaomboleza msiba, lakini kwa uoande wa pili tunategemea m4c itie timu muda si mrefu.
 
rip diwani. heading to 2015. bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. mia
 
Diwani wa kata ya Manchira (CCM) na ambaye pia likuwa makamu mweyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti amefariki dunia,
Mungu awafariji wafiwa na wanaManchira kwa ujumla!
Rest in Peace brother Mechama
Majonzi!
Msiba nautangazi,
Tumetokwa na kipenzi,
Mechama wetu mgenzi,
Ghafla imemwisha pumzi,
Tena pasi maandalizi,
Katutoka!
Machozi! Simanzi!
Ooi Ooi kama chizi, Tumetokwa na mlinzi,
Diwani wetu kipenzi, Mahiri kwa utetezi,
Kajiendea kwa Mnyezi, Tunatiririkwa machozi,
Kusiko na uonezi, Jamani hili pengo wazi,
Ufisadi wala wizi, Niwaulize wapenzi,
Akhera! Tulizibeje?
Mkurugenzi!
Uyaanze maandalizi,
Uwaite wafanyikazi,
Madiwani na viongozi,
Raia wote wapenzi,
Mechama 'wamhifazi'
Maana imemuisha Pumzi,
Na tumuombe Mwenyezi,
Amrehemu!
Aaaaaamen!!!
 
Diwani wa kata ya Manchira (CCM) na ambaye pia likuwa makamu mweyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti amefariki dunia,
Mungu awafariji wafiwa na wanaManchira kwa ujumla!
Rest in Peace brother Mechama

Majonzi!
Msiba nautangazi,
Tumetokwa na kipenzi,
Mechama wetu mgenzi,
Ghafla imemwisha pumzi,
Tena pasi maandalizi,
Katutoka!

Machozi!
Ooi Ooi kama chizi,
Tunatiririkwa machozi,
Mechama imemwisha pumzi,
Kajiendea kwa Mnyezi,
Kusiko na uonezi,
Ufisadi wala wizi,
Akhera!

Simanzi!
Tumetokwa na mlinzi,
Diwani wetu kipenzi,
Mahiri kwa utetezi,
Niwaulize wapenzi,
Hivi hili pengo wazi,
Tulizibeje?

Mkurugenzi!
Hebu anza maandalizi,
Uwaite wafanyikazi,
Madiwani na viongozi,
Raia wote wapenzi,
Mechama 'wamhifazi'
Maana imemuisha Pumzi,
Na tumuombe Mwenyezi,
Amrehemu!
Aaaaaamen!!!
Aaaaaamen!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…