mcndomba maprosoo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 225
- 94
TANZIA!
Ndugu zangu tumepatwa na janga lingine la kufiwa na mwanakijiji wa mwaka wa 3 (2012/2013) hapa Stemco marehemu SAMWEL SHILA MBOYA (25). Akitoa taarifa za kifo hicho Rais wa serikali ya wanachuo wa chuo kikuu kishiriki STELLA MARIS cha Mt. Agustino Mtwara Bw. Kamili John Chamafwa alisema kuwa, marehemu Samweli alianza kuugua Julai, 2012 akiwa anasumbuliwa na uvimbe sehemu za kwapani, shingoni na maeneo mengine, lakini hakuwa na maumivu.
Hata hivyo alitibiwa katika zahanati nyingi bila mafanikio, kabla ya kupelekwa hospitali ya wamisionari, Nyangao ambapo aliendelea kupata matibabu hadi uvimbe ulipofifia na kumfanya aendelee na masomo yake vizuri.
Januari 2013, uvimbe ulijitokeza tena, ambapo alitakiwa kwenda tena Nyangao ili 10/4/2013 sehemu ya sehemu ya uvimbe ikatwe ili kupelekwa Ujerumani kwa uchunguzi zaidi. Alipofikishwa hospitali mgonjwa alionekana kuwa na malaria kali ambapo alipewa drip za quinine kabla ya kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo mei 6, 2013.
Samwel aliendelea kuwa dhaifu na mwenye kukosa nguvu na hamu ya kula kabla ya kumhamishia hospitali ya mkoa, Ligula ambako alionekana kuwa na upungufu wa damu. Pamoja na kuongezwa chupa mbili za damu, hakukukuwa na nafuu ya haraka kwani damu ilizidi kupungua kwa kasi ndipo alipohamishiwa Muhimbili, ambako alikaa huko kwa juma moja hadi 30/4/2013 saa 2.30 usiku mauti ilipo mfika.
Hali hii imewafika katika kipindi kigumu ambapo wanachuo na jumuiya ya chuo wakiwa na shamra shamra za sherehe ya kumpongeza Rev Titus Mdoe, aliyekuwa Mkurugenzi wa utawala na fedha wa chuo hicho ambaye amepakwa mafuta kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mei 1, 2013.
Safari ya kwenda kuzika kijijini kwao Masoko, kata ya Ilembo, tarafa ya Isangati, Mbeya (V) imekwisha anza. Ndugu na jamaa wote wa vyuo vya SAUT walioko mbeya wanaobwa kushiriki mazishi ya kumuaga mpendwa wao yanayotarajiwa kufanyika 3/5/2013. Walioko mbeya wafike Mjini Mbalizi wapande gari zinazoenda Ilembo ama Iwiji ili kuweza kufika masoko km 50 toka mbalizi.
Marehemu alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Masoko kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Ilembo day alipohitimu kidato cha 4, baadaye aliendelea na masomo ya kidato cha 5&6, St. Elizabeth Education Centre Mkoani Morogoro kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kishiriki cha STELLA MARIS MTWARA mwaka 2010 akiwa anasomea Shahada ya Sanaa katika Elimu kwa masomo ya Historia na Kiswahili ambapo alikuwa anatarajiwa kuhitimu Juni, 2013.
Tuendelee kuwaombea na kufarijiana na ndugu, jamaa na marafiki waliopatwa na shida hii katika kipindi hiki kigumu. Hakika Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
Ameeen!