Tanzia: Imamu auawa akiongoza Ibada Msikitikini Nchini DRC

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,692
Kiongozi mkubwa wa Kiislamu mashariki mwa DRC ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akisali kwenye msikiti mkuu mjini Beni.

Mtu mwenye silaha alimfyatulia risasi Sheikh Ali Amini wakati wa suala ya Magharibi siku ya Jumamosi kisha akakimbia, mwanaharakati wa haki za binadamu ameeleza.

Kiongozi huyo alikuwa akikemea vitendo vya wanamgambo wa kiislamu kwenye eneo hilo, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

Mashariki mwa Congo imekumbwa na hali mbaya ya usalama, ikiwemo mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu (IS)
 
Hakika sisi sote ni wa mwenyezimungu na kwake tutarejea. Hali ya Beni imekuwa ni zaidi ya kutisha mauaji kila uchao.
Ifike hatua watu wa Kongo wajitathimini wenyewe. Maana hata umoja wa Afrika na umoja wa mataifa ni kama washachoshwa na mauji haya.
Vikosi vya kulinda amani vinapelekwa Kongo miaka inakwenda bado hakuna mabadiliko.
 
Wale Magaidi wa ADL wana msimamo mkali na huenda ndio wako nyuma ya haya mauaji.
 
Kumbe kauawa na wenzake! Ni aibu na huzuni kuendeleza vitendo vya kigaidi chini ya kisingizio cha dini. RIP Iman Amini.
 
Kiongozi mkubwa wa Kiislamu mashariki mwa DRC ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akisali kwenye msikiti mkuu mjini Beni.

Mtu mwenye silaha alimfyatulia risasi Sheikh Ali Amini wakati wa swala ya Magharibi siku ya Jumamosi kisha akakimbia, mwanaharakati wa haki za binadamu ameeleza.

Kiongozi huyo alikuwa akikemea vitendo vya wanamgambo wa kiislamu kwenye eneo hilo, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

Mashariki mwa Congo imekumbwa na hali mbaya ya usalama, ikiwemo mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu (IS)
Ni mufti wa Beni
 
Kumbe kauawa na wenzake! Ni aibu na huzuni kuendeleza vitendo vya kigaidi chini ya kisingizio cha dini. RIP Iman Amini.
Screenshot_20210503-043730.jpg

Kwani huyu haiwezekani kuwa aliuwawa na wenzake?
 
Waabudu mizimu na makaburi wamefanya kosa gani hadi wastahili kuuwawa?
hiyo ni comparison nimeitoa kuonesha ubaya wa hao vijana wanaofanya hivyo vitendo kwa mwamvuli wa uislamu, wanawadhuru waislamu wenyewe kama wangekuwa na malengo ya kuunyanyua uislamu vipi wawaue watu wake?!.....wanafanya mass bombing wanaua wanawake, watoto, wanachoma miti na kuharibu makazi ya watu....uislamu gani unafundisha hivyo...
 
Back
Top Bottom