TANZIA: Diwani wa CHADEMA Kata ya Namwawala mkoani Morogoro auawa kwa kukatwakatwa mapanga

Idadi wa watu waliofariki baada ya kupita chaguzi yetu ya mwaka 2015 mpaka sasa hivi Nadhani Upinzani viongozi wake WANAONGOZA KWA KUPATA VIFO VYA UTATA UTATA,,, Okay ngoja tuone
 
Kiuhalisia hii hama hama ya madiwani sometimes haipo kwa ajir ya pesa tyu bali na vitisho ukigoma kuhama chama ndo viwanda vya CCM ni kuua, daah tumefika kwenye wakat mgumu maana Magu ameandaa mauaji badala ya maendeleo hii nchi haikaliki tena. R. I. P diwani damu yako itamgusa kila mtu aliehusika hata kwa kutoa ushauri
 
Kiuhalisia hii hama hama ya madiwani sometimes haipo kwa ajir ya pesa tyu bali na vitisho ukigoma kuhama chama ndo viwanda vya CCM ni kuua, daah tumefika kwenye wakat mgumu maana Magu ameandaa mauaji badala ya maendeleo hii nchi haikaliki tena. R. I. P diwani damu yako itamgusa kila mtu aliehusika hata kwa kutoa ushauri
Dah jamani inatisha namna huyu diwani alivyokatwakatwa kuiangalia hiyo picha yahitaji moyo kidogo,dah Mungu atunusuru maana hali sio hali tena.
 
Nasikia alikuwa na kesi nyingi lakini alifanikiwa " kushinda hizo kesi" mambo ya sheria mmmh!!!!
 
Naona sasa uhai wa wawatu kukatishwa imekuwa jambo la kawaida tu
 
View attachment 700064
Sikitiko. Habari za sasa hivi,

Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Lwema (CHADEMA) ameuawa muda huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Polisi ndo wanaelekea huko.

Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akalutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho.

Namwawala Kilombero- Morogoro

========

Kamanda wa Polisi Morogoro na Mbunge wa Kilombero wazungumzia mauaji hayo

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kuuawa kwa diwani wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la Mlimba.

Diwani huyo Godfrey Lwena ameuawa usiku wa Alhamisi nyumbani kwake.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Matei amesema kwa sasa hawezi kufahamu mauaji hayo yanatokana na nini.

Akizungumza kwa simu Kamanda Matei pia amesema kwa sasa ni mapema mno kuwajua watu waliohusika na mauaji hayo na hivyo amewataka wananchi kuwa wavumivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wa mauaji hayo.

"Mauaji yametokea usiku huu na polisi wameshafika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, sasa hivi tuko kwenye uchunguzi na tunaomba wananchi watusaidie kutoa taarifa za watu wanaodhani kuwa wanahusika kwenye tukio hili na tutahakikisha tunawapata," amesema Kamanda Matei.

Awali mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali alithibitisha mauaji hayo na kudai kuwa yatakuwa yamepangwa.

Amesema kuwa mauaji hayo yametokea saa moja na nusu usiku wakati diwani huyo akiwa nyumbani kwake.

"Akiwa nyumbani kwake ghafla umeme ulikatika, Lwena alitoka nje na kuzunguka nyuma ya nyumba yake kuangalia kama kulikuwa na hitilafu na ndio ghafla lilitokea kundi la watu na kuanza kumshambulia kwa mapanga, " amesema Lijualikali.

Lijualikali amesema kuwa pamoja na watu hao kumshambulia diwani huyo kwa mapanga hadi kufariki lakini pia familia ya diwani huyo imepigwa mawe wakati wakijaribu kupambana na kundi hilo la watu.

Chanzo: Mwananchi
Haki ya Mungu hawa ni polisi!! wanalipwa wanatumiwa!! Hata huyu aliyempiga risasi mtu pale isamilo mwanza ni polisi alivaa mavazi ya ccm, nimesema mara nyingi kuwa huu unyama siyo ccm wala TISS ila ni polisi ndiyo wenye akili makalio!!. Operesheni piga polisi ianze mara moja!!
 
Inawezekana kabisa wapo wanaofurahia haya mateso wanayoyapata hawa Chadema na Ukawa kwa ujumla.Watambuwe tu kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kuwaacha wateseke wakati wote.

KAMA TAIFA, TUMEKWAMA.Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom