figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.
Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.
Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.
Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Bi Asha Bakari amewai kuwa Mwakilishi wa bunge maalum la katiba na Waziri wa wanawake na watoto Zanzibar na Makamu wa Jumuiya ya wanawake wa CCM.
Mwaka 2014 wakati wa mikutano ya kamati za Bunge la katiba (Dodoma) Bi. Asha Bakari alianguka ghafla na kutokwa Damu puani na masikioni ambapo aliwahishwa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya Threads kuhusu Bi. Asha Bakari
Asha Bakari aanguka ghafla Dodoma
Huwezi kuamini Asha Bakari alichokisema kwenye semina baada ya kuufyatua bungeni
VIDEO: Asha Bakari Makame, CUF Hata Mshinde Vipi Hatutoi madamu tumepindua
Asha Bakari hakuwa na haki ya kumtukana Jussa
Bi. Asha Bakari shujaa