Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 4,037
- 2,839
Aliyewahi kuwa Mbunge, Waziri wa maji madini na nishati, waziri wa mambo ya nchi za nje na nyadhifa nyingine kadhaa serikalini Mh Isael Elinawinga alifariki dunia 9/2/2016 katika hospitali ya Rufaa KCMC Moshi.
Atazikwa kesho tarehe 13/2/2016 huko kwao Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Maisha yake yote ya ustaafu alikuwa anaishi kijijini kwake akipata pensheni kidogo sana.
Nasikitika vyombo vya habari maarufu hapa nchini havijatangaza taarifa za kifo cha huyo mzee japo alitumikia taifa kwa bidii tena akiwa waziri na mbunge.
Naona harufu ya watanzania kusahau historia ya waasisi wa taifa hili. Kizazi cha sasa kinapaswa kujua historia ya nchi na walioitumikia kwa moyo wa uzalendo hata kama wamestaafu.
Au kwa vile huyu mheshimiwa hakuishi Dar ndiyo sababu ya kusahaulika?