Tanzia: Aliyekuwa Askofu Jimbo kuu Katoliki la Dodoma Mathias Isuja aaga dunia

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,371
2,377
Askofu mkongwe mstaafu wa jimbo kuu katoliki la Dodoma Mathias Isuja, ameaga dunia usiku huu.
Mungu aipumzishe roho yakekwa amani peponi.

askofu.jpg


Updates: Mwili wa marehumu Isuja umewasili na tumemuombea tayari na mwili sasa umepelekwa Mochwari,

Ratiba ya maziko na taratibu ziko hivi

Jumanne ya wiki ijayo kutakuwa na misa ya mkesha saa Kumi jioni

Na jumatano ndo itakuwa misa ya mazishi itakayo fanyika kanisa kuu la Paulo wa msalaba jimbo kuu Dodoma
 
R.I.P Babu........ Nimekumbuka mbali sana na dodoma.... na misa zako na pia misa nilizotumikia ukiwa na Fr Peter ambaye nae na Bishop sasa......

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA..
NA MWANGA WA MILELE UMUANGIZIE
 
Nilishiriki misa nyingi alizoendesha enzi tukiwa wuzengo complex Dodoma,
Raha ya milele umpe ee Bwana....
Na Mwanga wa milele umwangazie.....
Apumzike kwa Amani.... Amina
 
isuja.jpg


Aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Dodoma mhashamu baba Askofu Mathias Isuja Joseph amefariki alfajiri hii mjini Dodoma

Alisimikwa kuwa askofu wa jimbo katoliki la Dodoma tangu mwaka 1972 na baadae kustaafu kwa mjibu wa sheria mwaka 2005.
Amefariki leo alfajiri na alikuwa anapigana na salatani ya damu kwa miaka zaidi ya mitano.
Atazikwa ndani ya kanisa kuu la mtakatifu Paulo wa msalaba tarahe itakayotangazwa hapo baadae
Mungu aiweke roho ya askofu Mathias Isuja Joseph mahali pema peponi

AMEN
 
"R.I.P Babu........ Nimekumbuka mbali sana na dodoma.... na misa zako na pia misa nilizotumikia ukiwa na Fr Peter ambaye nae na Bishop sasa......" kwani anakusikia?
 
Back
Top Bottom