Tanzanite One yakwepa kodi kwa miaka mitano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzanite One yakwepa kodi kwa miaka mitano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  [h=2][/h]JUMAPILI, JULAI 15, 2012 07:54 NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

  WAKATI Kampuni ya Tanzanite One ya Afrika Kusini ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha Dola milioni mbili za Marekani, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe, ameibuka na kudai makosa ya kiufundi kati ya kampuni yao na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) ndiyo yaliyosababisha fedha hizo zisilipwe kwa wakati.

  Kodi inayodaiwa kukwepwa kulipwa na Kampuni ya Tanzanite One inayochimba madini ya Tanzanite katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ni ya kuanzia mwaka 2004 na 2008.

  Hata hivyo, alisema tayari Kampuni yao imekwisha anza utaratibu wa kulilipa taratibu deni hilo.

  Kuibuka kwa madai hayo kulijitokeza juzi, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele, alipotembelea maeneo ya migodi katika eneo la Mererani, wilayani Simanjiro juzi.

  Pamoja na mambo mengine, alielezwa malalamiko ya wachimbaji wadogo jinsi wanavyonyanyaswa na Kampuni hiyo kwa kumwagiwa maji chini ya ardhi pindi wanapochimba madini.

  Katika majibu yake kwa Naibu Waziri Masele, Balozi Mpungwe, aliweka wazi kuwa hakuna jambo kama hilo, bali kinachofanyika kwa wakati huo wa kuchimba madini huwa ni kukutana na maji chini ya ardhi.

  “Unapochimba chini ya mwamba lazima ukutane na maji na lazima uyatoe kwa kutumia mabomba yaliyofungwa chini ya ardhi ambayo hutoa maji migodini na kumwaga nje,” alisema Balozi Mpungwe na kuongeza:

  “Tatizo linalosababisha wachimbaji wadogo kulalamika kuwa wanamwagiwa maji linasababishwa na uchimbaji usiozingatia sheria na taratibu. Hivyo tunaiomba Serikali kutukutanisha na wachimbaji hawa ili tumalize tofauti na kuangalia upya taratibu za kuvuta maji nje,” alisema.

  Kwa upande wake, Masele, akizungumza baada ya kusikiliza apande zote mbili, kuhusu suala la kuongezewa mkataba au la alidai kwamba kwa sasa Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo.

  Akifafanua kuhusu tatizo la kuwapo kwa maji, Masele, aliitaka Kampuni hiyo kuhakikisha inaondoa maji hayo chini ya migodi mara moja.

  “Ni vyema mkiandaa utaratibu wa kuwa na vikao baina ya vijiji vinavyozunguka mgodi huu kwa kuwa kutarahisisha kuainisha mambo mnayotaka na kuafikiana kwa pamoja ili kuondoa kero kwa wananchi.

  Naye, mchimbaji mdogo, Hawa Karanga, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema sheria ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite inamtaka mchimbaji kuchimba madini hayo kwa kwenda chini ya eneo lake na si kuingiliana mipaka chini ya ardhi.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Amy Mpungwe... Blessings

  Kila Kiongozi wa Kitanzania anaiibia nchi yake; hakuna upenzi wa nchi hakuna anayejali...

  Na nchini ni visa na masihara kati ya wananchi ili kujenga chuki na kusahau wezi...
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wamieba Tanzanite, wametesa WaTz wenzetu na kodi yetu wanatutapeli, waondoke hao.
   
 4. J

  JIS Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Hawa TanzaniteOne wasichezee watanzania, TMAA wamebaini wizi wao waziwazi na wamewabana kisawasawa halafu wanasema eti kasoro za kiufundi. Ama kweli, mwizi hakubali kirahisi. Hawa ni wezi wakubwa, wanainyonya nchi hii kwa kivuli cha watanzania wenzetu akina Mpungwe. Naomba Mungu usiku na mchana Serikali isiwape leseni tena ili rasilimali ya nchi isiendelee kuporwa na hao wezi. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Balozi wa Bongo South Africa then Amy Mpungwe ndio aliyeileta... wengine wanasema PRINCE ana share;

  Nachanganyikiwa; sasa hawalipi kodi, madini ni yetu...
   
Loading...