Tanzanite One Mining Ltd yaelekea kufilisika

Tanzanite One Mining Ltd yaelekea kufilisika

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,178
Reaction score
37,475
Heshima sana wanajamvi,

Taarifa za ndani na uhakika ni kwamba Tanzanite One Mining Ltd kampuni ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite ipo katika hali mbaya kifeha.

Ikumbukwe Tanzanite One imeuzwa kwa wazawa kutoka kampuni ya wageni (south Africa) tangu ilipochukuliwa na wanaojiita wazawa wakiongozwa na Hussein Gonga mkaazi wa Arusha hali ya kifedha imezidi kuwa mbaya,wafanyakazi wanamaliza mwezi wa pili bila kulipwa mishahara,vifaa vingi kwaajili ya uchimbaji vimeshindwa kununuliwa,wazabuni mbali mbali hawajalipwa fedha tangu mwezi December mwaka jana.

Kodi mbali mbali za serekali hazijalipwa.Nii ajabu wanaojiita wazawa tena wanaodai wanauwezo na ujuzi wa kuchimba madini wanaliingiza taifa katika hatari ya kupoteza ajira za waTanzania zaidi ya 400 kwa mara moja.

Kibaya zaidi wazawa wamefuta idara za usafishaji,ukataji w madini na hivyo madini yote kusafirishwa nje ya nchi hasa India kwaajili ya kuongeza thamani ya madini na kuzalisha ajira India.

Nawasilisha.

Nawasilisha.
 
Mmmhh ngoja tusubiri walioeneo la tukio waseme naona wewe hujakamilisha habari
 
Tatizo wafanyakazi wengi wa Tanzanite One ni wezi wakubwa,, Bora ife tu huku mtaani tuheshimiane
 
No research no right to speak,wazawa wamepewa umeanza kuwasakama duuh!!!
 
Tumeshazoea kuuza juice na viwanda vya pipi,,big investment hatuziwezi,, tumezoea kuishi kiuganga uganga na kuishi kwa favor..
 
Ukiona mzawa kapewa ni sawa na Tulawaka kupewa wazawa ujue mali imeshaisha. Anza kutafuta Plan B ya maisha kama umeajiriwa hapo Job cut itakuhusu na bongo hakuna Bail out yaani imekula kwenu hiyo kama richmond ilivyokula kwetu umeme kila siku unapanda bila ufafanuzi kisingizio Dola ya mnyamwezi.
 
Ngongo Ungewataja hao wazawa walio uziwa kampuni hiyo...
 
Last edited by a moderator:
Baadhi Wazawa wanakurupukaga tuu, hawajui mgodi ni gharama kama huyu hussein gonga amezoe kununua madini yanayoibwa kwenye migodi ya wanaume wa kazi
 
Tatizo wafanyakazi wengi wa Tanzanite One ni wezi wakubwa,, Bora ife tu huku mtaani tuheshimiane

Cha kuiba kikowapi ndugu yangu?waliochukuwa mgodi hata kununua zana hawawezi sijui walijua wamenunua chemchem wao itakuwa ni kukinga tuu.
 
Hussein n faisal ni vibaraka 2 hawajanunua chochote wanatumiwa n prince......toka wamechukua mgodi huo kila m2 anatimu yke ya kupiga bomu n nguzo instead ya kusukuma shaft yani faisal anawatu wake hivyohivyo hussein ana kundi lake.
Fununu wanafanya hivyo kupiga hela ili mwezi wa 11 wasepe hussein kajaza warangi tupu plus wezi wa mawe waliokubu mererani
 
Ngongo Ungewataja hao wazawa walio uziwa kampuni hiyo...

Hussein gonga n faisal ni madealer wa gemstones hapa atwn....ila juu yao yuko prince we2 cz mkataba haujulikani cnc 2014 production imekua haieleweki mana huo mgodi kwa mwezi unatumia karibia 1bn.....kuanzia salary,zana,chakula,umeme,mafuta etc.
Pia shaft nyingi hazifanyi kazi wameshindwa kuhudumia
 
Last edited by a moderator:
Hussein n faisal ni vibaraka 2 hawajanunua chochote wanatumiwa n prince......toka wamechukua mgodi huo kila m2 anatimu yke ya kupiga bomu n nguzo instead ya kusukuma shaft yani faisal anawatu wake hivyohivyo hussein ana kundi lake.
Fununu wanafanya hivyo kupiga hela ili mwezi wa 11 wasepe hussein kajaza warangi tupu plus wezi wa mawe waliokubu mererani
Tanzanite One ilikuwa ni zamani, mimi mwenyewe niliifaidi sana. Sasa hivi imrjaa umbea, majungu, fitina kibao. Walianza kuwafitini viongozi wazungu punde tu serikali ilipoingiza share zake pale. Uswahili ukashamiri mpaka wazungu wa watu wakaanza kunyimwa kuendelea na kazi, isitoshe wakaanza kuwafuatilia baadhi ya wafanyakazi kwa kigezo eti ni wezi, toka waondolewe imekuwa kama gundu yani, hakuna kipya wala chochote cha maana. Wale waliofukuzwa mpaka leo wapo fiti mtaani kuliko waliobaki na majungu yao.
 
Mkuu americana vp mzee D,na Rutta wapo?maana wale ndo watendaji wakuu,hata kupelekea Tanzanite one ifahamike kwa uzalishaji mkubwa.kama waliondolewa kwa majungu,basi ndo mana hata kampuni imeyumba kiutendaji pia.
 
Ruta aliacha mda sana anahisa kwenye migodi kma minne ya wazawa na anapiga hela tu....mzee d alifukuzwa mwaka jana nae kaanzisha mgodi block d yuko na mullah
 
Last edited by a moderator:
Hussein n faisal ni vibaraka 2 hawajanunua chochote wanatumiwa n prince......toka wamechukua mgodi huo kila m2 anatimu yke ya kupiga bomu n nguzo instead ya kusukuma shaft yani faisal anawatu wake hivyohivyo hussein ana kundi lake.
Fununu wanafanya hivyo kupiga hela ili mwezi wa 11 wasepe hussein kajaza warangi tupu plus wezi wa mawe waliokubu mererani

Mkuu kwa hiyo WARANGI ndio wamesababisha mgodi ushindwe kujiendesha? UKABILA si mzuri kaka.
 
Tanzanite One ilikuwa ni zamani, mimi mwenyewe niliifaidi sana. Sasa hivi imrjaa umbea, majungu, fitina kibao. Walianza kuwafitini viongozi wazungu punde tu serikali ilipoingiza share zake pale. Uswahili ukashamiri mpaka wazungu wa watu wakaanza kunyimwa kuendelea na kazi, isitoshe wakaanza kuwafuatilia baadhi ya wafanyakazi kwa kigezo eti ni wezi, toka waondolewe imekuwa kama gundu yani, hakuna kipya wala chochote cha maana. Wale waliofukuzwa mpaka leo wapo fiti mtaani kuliko waliobaki na majungu yao.

Mkuu wengi wamechoka asikwambie m2 wameuza nyumba mana walijua mgodi w baba yao ila wenye akili wako njema....hussein n faisal wanapiga nguzo n bomu kma apolo instead y kusukuma shaft wanazidiwa n migodi y wazawa
Tanzanite bado ipo sana migodi inayofanya kazi kiuhakika wanapata tu
 
Mkuu kwa hiyo WARANGI ndio wamesababisha mgodi ushindwe kujiendesha? UKABILA si mzuri kaka.

Mkuu hatuwasemi kwa ubaya ila ndio hvyo hussein kachukua warangi wenzie kibao kajaza pale ili waibe mawe instead y kusukuma shaft......then hao warangi ndio mateam leader hata cheti cha std 7 hawana.
Kuna jamaa anaitwa bob ally ni mpiga bomu maarufu nae mkuu kazi yake ni kupiga bomu n nguzo 2,wana mda mrefu hawajatoa production y maana wakati apolo za kawaida wa2 wanatoa mzigo wa haja
 
Basi mkuu tatizo si warangi ila ni wenye mgodi, kwanza mgodi wenyewe walipeana kinyemela na huyo prince, tenda ya kuuza haikutangazwa popote walipeana kwa hati ya dharura wacha mgodi usiteme, kwani shida gani? Waliopata wakachezea ndio basi tena. Acha wanaapolo wapate mzigo warudishe heshima A town. Haaa nimemkumbuka Elisante enzi zile bado nafaa uniform alisumbua kichizi A town ilikuwa tamu kweli.
 
Mkuu tweenty4seven wewe kweli ni mdau wa Tanzanite One Mining mambo ulisema ni kweli 100%.Mimi ni mdau mkubwa enzi za Makaburu nikuwanafanya biashara kubwa ya lubricants lakini walipoingia Hussein Gonga na Faisal ulipaji ukawa wa kusuasua nilipolipwa fedha zangu nikaacha kufanya biashara na nao.Walijaribu kunitumia order kadhaa nikagoma kusupply.Nikawawekea conditions wakashindwa CWO wanataka mkopo kulipa mpka uende kama mara kumi ulie kilio cha mbwa ndio wakufikirie ukimpgia simu Finance Manager Bwana Saitoti wala hapokei ndio nikawapiga chini sitaki biashara yao kabisa.

Ni kweli Bwana Hussein Gonga kawajaza warangi wenzake utafikiri anakwenda kugombea ubunge Kondoa.Idadi ya wafanyakazi walioajiriwa kipindi anakabidhiwa mgodi haiendani na kazi zilizopo pamoja na huduma za wachimbaji kama matundu ya vyoo,mabafu ya kuogea na nk.

Jambo baya zaidi ni kitendo cha kulipua nguzo ambazo ni muhimu kwa usalama wa mgodi.jambo hili linafanyika kw maksudi kabisa huku maafisa usalama wakiangalia kuna siku utasikia maafa makubwa yametokea ndio utasikia tume za kibabaishaji zinaundwa ihali ukweli unajulikana.

Vifaa vingi havifanyikazi hasa shaft zimewashinda kabisa ndio maana wanakimbilia kulipua nguzo kukwepa gharama za kuendesha shaft.

Wataalamu wengi hasa wazungu toka South Afrika wametimuliwa kwasababu walikuwa wanakula nguruwe wakaonekana hawafai kabisa utaalamu wao ukawekwa kando.Waongoza njia vi vibaka wa porini hasa Merereni ambao wanafanyakazi kwa uzoefu tu pasipo ujuzi wowote,kibaya zaidi wengi ni wezi wa mawe waliokubuhu matokeo yake mawe mengi yanaishia njia matajiri wanaolipa mishahara,chakula na gharama kubwa za mgodi wanaambulia mawe machache sana huku wakibebeshwa gharama kubwa za kuendesha mgodi.

Back
Top Bottom