Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,931
- 31,176
Heshima kwenu wanajamvi,
Habari mbaya kwa machalii & wanaApollo wa miji ya Arusha na Kilimanjaro.Nimepenyezewa taarifa za uhakika kwamba kampuni ya uchimaji wa madini ya vito (Tanzanite) itapunguza wafanyakazi 600 wakati wowote kuanzia sasa ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha uliyoikumba kampuni hiyo tangu ilipochukuliwa na wafanyabiashara wazawa Hussein Gonga na Faisal Shahbhai raia wa Tanzania mwenye asili ya kiasia (Hindi).
Hali ya uzalishaji imezidi kuwa mbaya hasa baada ya wataalam wengi kuondoka baada ya kushindwa kufanyakazi chini ya uongozi mpya uliojaa ubabaishaji na ukosefu wa ujuzi wa kutosha wa kuedesha migodi mikubwa.Huduma nyingi hasa chakula,usafiri na nk zimekuwa zikisuasua kwa muda mrefu.Madeni makubwa ya wazabuni mbali mbali limekuwa tatizo kubwa na kusababisha kuzorota kwa uzaishaji wa madni hao hadimu duniani yanayopatikana Tanzania tu.
Mara kadhaa nimekuwa nikileta mabadiko yanayohusiana na kudorora kwa uzalishaji wa mgodi huo uliokuwa ukiingizia serekali mapato makubwa.
Waziri wa madni kipindi milki ya mgodi ilipohamishiwa kwa wazawa wababaishaji Mheshimiwa Simbachawene alionywa juu ya uwezo na ujuzi wa wamiliki wapya lakini hakutilia maanani kwasababu ambazo anazijua mwenyewe.