Tanzanite hiyoo kama kahawa na pamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzanite hiyoo kama kahawa na pamba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by never, May 22, 2011.

 1. n

  never JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  INASEMEKANA kwamba baadhi ya majumba mazuri na ya kisasa yaliyojengwa mjini Arusha, ni matunda ya tanzanite, magari ya kifahari yanayoendeshwa na matajiri pia ni matunda ya tanzanite.

  Inaaminika pia kwamba wale wanaolima mashamba makubwa ya maua wamepata mtaji kutokana na madini ya tanzanite. Ukihoji anayefaidi matunda hayo ya tanzanite, anayelala kwenye majumba hayo mazuri, anayeendesha magari hayo ya kifahari, utaambiwa ni mawakala na wafanyabiashara wakubwa wa tanzanite.

  Wengine ni wageni wanaojulikana kama wawekezaji na Watanzania wenye asili ya India. Baadhi ya viongozi wa serikali wenye ubia kwenye makampuni ya uchimbaji nao wanafaidi matunda ya tanzanite.

  Lakini wachimbaji wa tanzanite, wale wanaoonja suluba ya mgodini na wakati mwingine kuhatarisha maisha yao, wanaambulia kiduchu kama ilivyo kwa wakulima wanaoshinda shambani wakilima, wakipanda na kuvuna na mwishowe kuambulia kiduchu wanapoyauza mazao yao.

  Mbali na wachimbaji, hata wenyeji wa Mererani ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi juu ya madini haya, wakiyalinda na kuyatunza hawafaidi matunda ya madini yao. Wanawashuhudia wageni wakija kuvuna na kuondoka na utajiri.

  Hali ya Mererani haina tofauti na sehemu nyingine za Tanzania zinazozalisha madini kwa wingi. Kule Geita kilio ni kile kile, Mwadui ni kile kile, Kahama, Nzega, Buzwagi na sehemu nyingine zenye dhahabu na Almasi ni hivyo hivyo.

  Wawekezaji wanachimba madini na kuacha mashimo nyuma yao. Ni wazi serikali itakuwa inatoza ushuru na malipo mengine; swali la kujiuliza ni kwa nini fedha hizi zinazopatikana kutokana na madini zisirudishwe kwenye maeneo husika ili kuchangia maendeleo?

  Kwa nini fedha inayotokana na tanzanite isichangie maendeleo ya mji mdogo wa Mererani na maeneo yanayouzunguka? Kwa nini, kutokana na fedha hizo, serikali isiwawezeshe wachimbaji wadogo kununua vifaa vya kisasa na kufanya uchimbaji wa kisasa kinyume na wanavyofanya sasa? Kwa nini wageni waendelee kuifaidi nchi yetu wakati wazawa wanaendelea kusota kwenye umasikini?

  Dhahabu imechangia kiasi kikubwa kuuendeleza mji wa Mwanza, lakini maendeleo hayo ni ya kundi dogo la watu. Walio wengi, na hasa wenyeji wa mji wa Mwanza, bado wanaishi katika umasikini. Wachimbaji wadogo wanaendelea kuishi kwenye machimbo maisha yao yote.

  Dhahabu wanazozichimba zinanunuliwa na wakala na kuuzwa kwa matajiri wakubwa wanaoziuza nje ya nchi na kupata faida kubwa.

  Leo hii majumba mazuri yaliyojengwa jijini Mwanza, mahoteli mazuri na ya kupendeza na magari ya kifahari, ni matunda ya uvuvi wa samaki. Mawakala na matajiri wakubwa wanaoendesha biashara ya samaki (kusindika na kuuza minofu ya samaki nje ya nchi) wametajirika na wanaishi maisha ya kifahari. Lakini maisha ya mvuvi wa kawaida anayeonja suluba ya ziwani na wakati mwingine kuhatarisha maisha yake yanaendelea kuwa duni siku hadi siku.

  Bei ya kahawa katika soko la dunia ni kubwa ukilinganisha na bei ya mkulima. Bei ya pamba pia ni kubwa katika soko la dunia ukilinganisha na bei ya mkulima. Kama wakulima wa pamba na kahawa wangeweza kuuza kahawa na pamba moja kwa moja kwenye soko la dunia, wangeweza kuyaendesha maisha yao kwa unafuu zaidi.

  Naandika makala hii nikiwa Karagwe, nashuhudia jinsi mavuno ya kahawa yalivyo mazuri na watu wamepata kahawa nyingi. Nashuhudia malori yakisomba kahawa usiku na mchana. Swali ni je, bei ya kahawa mwaka huu inaridhisha?

  Nchi jirani ya Uganda bei ya kahawa iko juu, hapa kwetu bei iko chini kiasi cha kutomsaidia mkulima kuyabadilisha maisha yake kwa kasi ya kutosha. Labda kama mkulima angepata mfumo wa kumsaidia kuuza kahawa yake moja kwa moja kwenye soko la dunia; ukulima wa kahawa ungeweza kuyabadilisha maisha ya Mtanzania.

  Vinginevyo itakuwa ni hadithi ile ile ya wakulima kufanya kazi kwa nguvu zote na kuendelea kushuhudia wakala, matajiri na vyama vya ushirika wakifaidi matunda ya kahawa.

  Naandika makala hii kwa uchungu mkubwa baada ya kuutembelea mji mdogo wa Mererani na kulala siku tatu. Nimeshuhudia mwenyewe yale yote yaliyokuwa yakiandikwa kwenye vyombo vya habari juu ya Mererani na watoto wa Mererani.

  Wakati matunda ya tanzanite inayochimbwa Mererani kuonekana Arusha mjini, Afrika ya Kusini, India na kwingineko, watu wa Mererani wanaendelea kuishi kwenye dimbwi la umasikini.

  Barabara ya vumbi inayoelekea Mererani kutokea uwanja wa Kimataifa wa KIA, ni ishara tosha kwamba utajiri wa Mererani unawanufaisha watu wengine. Kwamba mji mdogo wa Mererani hauna huduma ya maji yaliyo safi na salama, ni ushahidi mwingine kwamba tanzanite haijawanufaisha watu wa Mererani.

  Nilianza kufuatilia na kuandika juu ya Mererani mwaka 2002. Nilikuwa natokea Arusha kwenda Machame kumtembelea rafiki yangu Mheshimiwa Freeman Mbowe. Kijana aliyekaa nyuma yangu kwenye basi la kutoka Arusha -Moshi ambaye alionekana kulewa kupindukia alinitapikia!

  Kijana huyu alikuwa na kundi la vijana wengine wengi waliokuwa pia wamelewa, wamevaa nguo chafu na ngozi ya miili yao ikiwa myeusi kupindukia; kana kwamba hawajaoga zaidi ya mwaka mmoja.

  Nilipoonyesha kushangaa na kuchukizwa kwa tendo la kijana kunitapia, msafiri mwenzangu alinituliza kwa kunielezea maisha magumu ya vijana hao wanaoitwa Wana Apolo kutoka katika machimbo ya tanzanite – Mererani.

  Baada ya mkasa huo niliandika makala juu ya Watoto wa Mererani. Nilianza kufuatilia katika magazeti habari za Mererani, niliwasiliana na mashirika yanayotetea haki za wachimbaji na kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na wakereketwa wa Mererani.

  Nilikuwa sijapata bahati ya kuitembelea Mererani hadi mwaka huu mwezi wa sita nilipokuwa nafanya utafiti wa huduma majumbani. Nilikaa Mererani siku tatu. Nilijionea mwenyewe maisha ya Wana Apolo ambao wengi wao wameamua kuishi maisha ya aina yake; ulevi, madawa ya kulevya na ngono.

  Wakitoka machimboni wanakuwa na hali fulani ya kukata tamaa. Wakishapitia Kijiweni na kufanikiwa kuuza tanzanite kwa bei ya chini inayopangwa na wakala, wanaamua kuzitumia fedha kwa starehe.

  ‘Jeuri’ yao ni kwamba kesho watarudi migodini na kupata tanzanite nyingine. Wanakunywa pombe kama wendawazimu na kutumia fedha hizo kuendekeza ngono bila kinga. Hawana habari na maisha ya kesho, hawana habari na kizazi kijacho, hawana habari kwamba jasho lao linawaneemesha matajiri wa Arusha mjini, India na Afrika ya Kusini, na wala hawana habari kwamba wakiishi kwa utaratibu mzuri wanaweza kuchangia kiasi kikubwa cha maendeleo yao binafsi na jamii inayowazunguka.

  Wanapumbazwa na fedha ya haraka. Na bahati mbaya hakuna mfumo wa jamii wa kuwaelekeza na kuwashauri. Mbali na Wana Apolo, nilijionea pia maisha ya watu wote wa Mererani. Watu wanaoishi juu ya utajiri mkubwa, lakini wao ni masikini wakubwa!

  Badala ya tanzanite kuleta neema, imeleta balaa kubwa. Ardhi inachukuliwa na matajiri wakubwa wanaoitafuta tanzanite. Magonjwa ya kusendeka kama ukimwi yameenea kwa kasi baada ya kugundulika tanzanite katika maeneo ya Mererani.

  Watu wengi walihamia Mererani kutoka kila upande na kusababisha msongamano na ukosefu wa maadili. Ndoa za watu zimevunjika; maana matajiri wa tanzanite wanatumia fedha nyingi walizonazo kuzivuruga ndoa za watu.

  Niliweza kuongea na baadhi ya Wana Apolo. Ni vijana wadogo kati ya miaka kumi na minane hadi thelathini. Wengi wao wamemaliza darasa la saba. Wengine walikuwa sekondari wakaacha ili waingie mgodini kupata fedha ya haraka: Ni mawazo kama ya vijana wengine wanaoingia serikalini kwa lengo la kupata fedha haraka na matokeo yake wanajiingiza kwenye udanganyifu, rushwa na ufisadi.

  Mawazo ya Wana Apolo ni fedha. Wanaamini kisomo hakileti fedha! Hawana imani na serikali, hawana imani na viongozi wa dini, na kusema kweli hawana imani na mtu yeyote yule. Wana imani na fedha! Wanaamini fedha ni kila kitu. Hawaogopi kufa! Wako tayari kwa lolote .

  Kila wakati wanasema machimboni ni hatari kubwa na mtu anaweza kufa wakati wowote ule; anayepona ni lazima kuhakikisha anayafurahia maisha. Na kwao, kufurahia maisha ni ulevi na ngono! Kwa vile hawaogopi kufa, hata suala la kinga ya ukimwi kwao ni hadithi na wala hawataki kusikia.

  Wanaendelea kufanya ngono bila kinga na kuendelea kusambaza virusi vya ukimwi. Pamoja na uwazi mkubwa wa watu wa Mererani juu ya ugonjwa wa ukimwi; maana wagonjwa hawajifichi, bado ugonjwa huo si tishio kwa Wana Apolo.

  Ni wazi Wana Apolo hawana mfumo wa kuyaongoza maisha yao. Jamii yetu imeshindwa kubuni mifumo ya kuwasaidia watu kama hao na kuzuia mazingira kama hayo kutokea. Serikali imeshindwa kutengeneza mifumo ya kuwaongoza vijana na kuwaelekeza katika maadili mema.

  Viongozi wa dini nao wameshindwa kabisa kutengeneza mifumo ya kufundisha maadili mema kwa vijana na kwa Watanzania wote. Vijana wanapokata tamaa ya maisha kama ilivyo kwa Wana Apolo, wanashindwa mahali pa kukimbilia zaidi ya ulevi na ngono.

  Hivyo basi tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni muhimu sana kuwa makini wakati tunawachagua viongozi wetu. Kuna haja ya kuwachagua viongozi wanaoguswa na maisha ya Watanzania.

  Kuna haja ya kuwachagua viongozi watakaohakikisha kwamba wananchi wanakunywa maji kutoka kwenye visima vyao wenyewe; kwamba wakulima wa kahawa wanapata bei nzuri inayoweza kubadilisha maisha yao; kwamba wakulima wa pamba wanafaidika na kilimo hicho; kwamba wachimbaji wadogo wa madini na watu wote wanaoishi kwenye maeneo ya madini wananeemeka kwa madini hayo.

  Kuna haja ya kuwachagua viongozi wenye upeo na mwelekeo wa kutamani kuunda maadili ya Kitaifa.

  Tukifanikiwa kuwapata viongozi walio makini, viongozi wanaojali ustawi wa wananchi wa Tanzania; viongozi wenye uwezo wa kulinda na kutunza vizuri rasilimali za taifa letu; viongozi wenye kuhakikisha watu wanakunywa maji kutoka kwenye visima vyao wenyewe; viongozi wenye uwezo wa kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo; viongozi wa kuhakikisha madini yanaleta maendeleo katika maeneo ya migodi na katika taifa zima, ni wazi kabisa kwamba umasikini katika Taifa letu itakuwa ni historia.
   
 2. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Tanzania ina matatizo makuu matatu ambyo bila ya kuyapatia ufumbuzi hakuna maendeleo yeyote yatakayofikiwa 1-education 2-education 3-education
   
 3. v

  valid statement JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Nini kifanyike kubadili hali hii ?
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  we produce what we do not consume and we cpnsume what we do not produce
   
 5. Mc Tilly Chizenga

  Mc Tilly Chizenga JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 3,694
  Likes Received: 805
  Trophy Points: 280
  mkuu,umeongea mengi mazuri lakini ni yaleyale tunayofundishwa shule toka babu yako mpaka mjukuu wako atafundishwa hivyohivyo bila kuwapo mabadiliko!mabadiliko yataanza tukiukubali ukweli huu!

  Rasimali sio mali!rasimali sio utajiri,utajiri ni mali!tanzania sio nchi tajiri,hatujaweza kuvuna rasimali zetu na kuzigeuza kuwa mali!ukijenga na kuishi ktk nyumba ya udongo iliyo juu ya tani za dhahabu zilizoko ardhini nyumba yako itaendelea kubakia ya udongo na ndio itakuwa level yako ya maisha!you are never the rich unless unavuna dhahabu hizo na kuziuza!

  mitaji ama capital ipo ya namna nyingi!pesa,akili,kipaji na nguvu yote ni mitaji,mitaji mi 3 ya mwanzo ndiyo inayolipa zaidi ktk dunia unayoishi leo!messi,etoo,ronaldo,mwanamuziki diamond hao mitaji yao ni kipaji,wametoka kivyao!watu kama marehemu steve jobs,dogo wa facebook mark zuckerberg,wataalamu walioajiliwa ktk migodi ya tanzanite hao wamewekeza ktk akili wote hao lazima wafaidike ktk uwekezaji wao!na kundi la mwisho la uwekezaji wa pesa wote tunajua uwezo wa pesa!kundi la mwisho la uwekezaji wa kutumia nguvu..popote walipo duniani lazima wawe daraja la mwisho ktk jamii(labda ktk ndondi au mieleka na kwenyewe pia utakuta promota anavuta ndefu kuliko bondia).

  Kwa ufafanuzi huo hapo juu,hakuna jinsi ya kubadili hali kama uwekezaji wetu mtaji wetu ni nguvu!itakuwa hivyo mpaka mwisho wa dunia,ukweli ndio huu,tujipange basi ni vipi tutawekeza kwa kutumia aina nyingine za mitaji nilizoeleza hapo juu
   
 6. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  sera bovu za watawala ndio zinaleta haya yote,bila mabadiliko ya sera hamna kitu .
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sera mbovu, mimi nilitegemea fedha tunazopata kwenye madini angalau asilimia ndogo tungewekeza kuwasaidia wananchi kwenye kilimo kwakuwa madini yakupita na kilimo ndio maisha ya mwananchi wa Tanzania na itabaki hivyo.
   
Loading...